Papa apongeza ujasiri wa Chama cha Vajont katika mustakabali wa kumbukumbu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Ijumaa tarehe 19 Januari 2024 amekutana na wawakilishi Jumuiya ya Jimbo la Belluno-Feltre, Pordenone nchini Italia katika kumbukumbu ya miaka 60 ya janga kupasuka kwa Bwawa lililosababisha uharibifu wa miji yote na zaidi ya waathiriwa 1,900 katika mkoa huo. Papa Francisko amewakaribisha kwa furaha na kuwasalimu wote, pamoja na Askofu wao na Mkuu wa Wilaya ya Belluno, ambapo wote wamefika kama mahujaji. Amewakaribisha mapadre na Mkuu wa Wilaya pamoja na Chama cha “Vajont - il futuro della memoria,” yaani Chama cha “Vajont katika mustakabali wa kumbukumbu.” Papa amesema kuwa wao wamefika Roma katika kaburi la Mtume Petro na mzigo mzito sana wa kumbukumbu na mateso.
Kwanza kabisa, Papa amependa kueleza ukaribu wake kwao na kuwashukuru kwa kile wanachofanya na jinsi walivyo kwa uwepo wao tu unaowakilisha wimbi la matumaini. Ikiwa miaka sitini iliyopita, hasa mnamo tarehe 9 Oktoba 1963, wimbi maporomoko lilichukua miji na vijiji vyote, na kusababisha waathriwa 1,910, wao ni wimbi la maisha. Kwa hakika, waliitikia wimbi hilo la maangamizi na uharibifu kwa ujasiri wa kumbukumbu na ujenzi. Papa amefikiria matone yote ya kimya ambayo yaliunda wimbi hili kubwa la wema kuanzia kwa waokoaji, wajenzi, na wengi ambao hawakujiruhusu kufungwa na maumivu lakini waliweza kuanza tena. Wao ndio waumbaji, na wao ni mashahidi wa mbegu hizi za ufufuko, ambazo labda hazifanyi habari nyingi, lakini ni za thamani machoni pa Mungu, aliye “mtaalamu wa kuanzisha upya, Yeye ambaye kutoka kwenye kaburi la kifo ameanzisha historia ya milele, ya maisha mapya. Asante kwa ushuhuda wenu.” Papa aliwapongeza.
Papa Francisko amefikiria teba kilichotokea ni kwamba maumivu hayo yasiyohesabika na yasiyoelezeka, kama karatasi kubwa ya barafu moyoni, kutokana na joto la mshikamano wao, ukaribu wa wengi na msaada wa Mungu, uliyeyuka polepole, kisha kumwagilia jamii. Na, kama asili ya watu wao, wamefanya mema mengi bila maneno mengi, lakini kwa kujitolea sana na uthabiti, ukikunja mikono yao: kwa hivyo wamejenga upya kwa uangalifu ambapo kwa kupuuza kulisababisha uharibifu. Tukitafakari juu ya maafa ya Vajont, kipengele kimoja kinamgusa mtu hasa kilichosababisha mkasa huo si makosa katika muundo au ujenzi wa bwawa, bali ni ukweli wa kutaka kujenga hifadhi ya maji mahali pasipofaa. Na kwa nini haya yote?
Ni kwa sababu ya kuweka mantiki ya faida kabla ya kumjali mwanadamu na mazingira anamoishi na kwa hiyo wimbi lao la matumaini likisukumwa na udugu, wimbi hilo lililoleta kukata tamaa lilisababishwa na uchoyo. Na uchoyo huharibu, huku udugu unajenga. Baba Mtakatifu Francisko amewaeleza kuwa huu ni ni wakati muafaka sana. Na kwamba hatachoka kurudia kusema kwamba utunzaji wa uumbaji sio sababu rahisi ya ikolojia, lakini suala la kianthropolojia: inahusiana na maisha ya mwanadamu, kama vile Muumba alivyofikiria na kupanga, na inahusu mustakabali wa wote, wa ulimwengu, jamii ambayo tumezama ndani yake. Na wao wakikabiliwa na janga linaloweza kutokea kutokana na unyonyaji wa mazingira, wana ushuhuda wa haja ya kutunza uumbaji.
Hili ni muhimu leo, hii kwani nyumba ya watu wote inabomoka, na sababu ni ileile kwa mara nyingine tena ya uchoyo wa faida, mkanganyiko wa kupata na kumiliki ambao unaonekana kumfanya mwanadamu ajisikie mwenye uwezo wote. Lakini hii ni udanganyifu mkubwa, kwa sababu sisi ni viumbe na asili yetu inatuomba kuhamia duniani kwa heshima na uangalifu, bila kufuta, badala ya kuhifadhi hisia ya kikomo, ambayo haiwakilishi kupungua, lakini ni uwezekano wa ukamilifu. Wale ambao hawajui jinsi ya kulinda kikomo kamwe hawataweza kusonga mbele. Papa Francisko vile vile katika hotuba yake amependa tena kushirikisha wazo moja zaidi na wao. “Mwaka huu unaadhimisha miaka mia nane ya utunzi wa Wimbo Viumbe wa Mtakatifu Francis Mtakatifu Msimamizi wa Italia.
Pia ni maandishi ambayo yalizindua fasihi ya Kiitaliano. Katika sifa ile adhimu, Maskini wa Assisi anaita jua, mwezi, nyota, upepo, moto na mambo mengine, kaka na dada, naye anaviita hivyo kwa sababu viumbe hivyo ni sehemu ya “mtandao hai wa wema,” iliyoandaliwa kwa upendo na Bwana kwa ajili yetu. Kwa hakika, mwandishi wa wasifu wa kwanza alimthibitisha Fransis: “Anakumbatia viumbe vyote vilivyoumbwa kwa upendo na ibada ambayo haijawahi kusikika” (Tomaso wa Celano katika, Maisha ya Pili, CXXIV, 165: FF 750). Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa katika Wimbo huo wa Viumbe, anamsifu “Bwana” kupitia Maji, ambayo ni muhimu sana, manyenyekevu, ya thamani na yaliyo safi” (FF 263). Yanafaa na ya unyenyekevu, lakini yamekuwa ya kutisha na yenye uharibifu katika kesi ya Vajont, au yasiyoweza kufikiwa kwa wengi ambao leo hii, ulimwenguni, wanakabiliwa na kiu au hawana maji ya kunywa.
Kwa hiyo Papa Francisko amesema: “Tunahitaji mtazamo wa kutafakari, mtazamo wa heshima wa Mtakatifu Francis ili kutambua uzuri wa uumbaji na kujua jinsi ya kuweka mambo kwa mpangilio sahihi, kuacha kuharibu mazingira kwa mantiki mbaya ya uchoyo na kushirikiana kidugu katika maendeleo ya maisha. Wao wanafanya hivyo, wakihifadhi kumbukumbu na kushuhudia jinsi uhai unavyoweza kufufuka pale pale, ambapo kila kitu kilikuwa kimemezwa na kifo. Papa Francisko amerudia tena shukrani zake kwao kwa hilo na kuvutiwa na uthabiti wa manufaa na thabiti wa muundo wa jumuiya yao. Amewabariki kutoka ndani ya moyo wake. Na pia kuwaomba wasali kwa ajili yake.