Mji wa Vatican Mji wa Vatican   (Marcello Leotta)

Papa arekebisha sheria za mikataba na gharama zisizo za kawaida

Maamuzi ya Papa Francisko yaliyomo katika barua mbili binafai za motu proprio zilizotolewa tarehe 16 Januari 2024.Tarehe ya mwisho wa matumizi imewekwa ambapo matumizi ya zaidi katika miundo ya Vatican lazima iombe idhini kutoka Sekretarieti ya Uchumi.

Vatican News

Hatua mbili zimefafanuliwa vyema juu ya usimamizi wa matumizi ya idara binafsi za mabaraza ya Kipapa, Vatican na kuboresha uwazi katika sekta ya manunuzi. Haya ni maneno ambayo Papa Francisko amebainisha katika  hati mbili zilizotolewa tarehe 16  Januari 2024 na Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican. Katika muktadha wa kwanza ni barua ya kitume ya mfumo wa motu proprio ambayo  Baba Mtakatifu Fransisko anabainisha “mipaka na mbinu” za usimamizi wa kawaida wa Mabaraza ya Kipapa Vatican. Katika vifungu vitatu, kwenye mwongozo wa upyaishaji wa Katiba ya Praedicate Evangelium, yaani Hubirini Injili, kimsingi imethibitishwa kwamba Baraza lolote la Kipapa la Vatican linatakiwa kuomba idhini ya mkuu wa Sekretarieti ya Uchumi wakati kitendo cha matumizi kinazidi asilimia 2% ya gharama zote za Baraza lenyewe, pamoja na takwimu zilizotolewa kwa wastani bajeti ya mwisho ya miaka mitatu iliyopita.

Katika hilo kwa hiyo, imeanzishwa kwamba:  “Kwa hali yoyote idhini haihitajiki kwa thamani yake ambayo ni chini ya euro 150,000.” Hatua nyingine ya hati iliyoweka kikomo cha kupokea kibali kwa siku 30, zaidi ya ambayo hata kushindwa kujibu ni sawa na kukubali ombi, na kwa hali yoyote inaelezwa kuwa utaratibu huu “lazima uhitimishwe kabla ya siku arobaini.”

Sheria ya manunuzi

Katika barua ya pili katika mfumo wa motu proprio, Baba Mtakatifu  anaingilia kati ili kutoa ufafanuzi zaidi kwa sheria inayodhibiti kanuni ya ununuzi wa Vatican iliyotangazwa mwaka 2020. Pia katika mkutadha huo kulingana na Katiba ya  Praedicate, Evangelium, Papa Francisko anasisitiza kwamba motu proprio inataka kuendelea katika “hotuba iliyofanywa ili kukuza uwazi, udhibiti na ushindani katika taratibu za kutoa kandarasi za umma, kwa ajili ya “matumizi yenye ufanisi zaidi” ya sheria ambazo pamoja na marekebisho ya hivi karibuni huzingatia “uchunguzi wa Taasisi zilizounganishwa na Vatican na uzoefu uliopatikana kwa miaka hii.”

Kifungu cha kwanza katika aya ya 2 hasa kinabainisha, kuzifafanua tena katika mambo manne kuhusu mwaka 2020, madhumuni yaliyofuatwa na sheria, kulingana na kanuni za Mafundisho  Jamii ya Kanisa, ya utaratibu wa kisheria wa Makao makuu na Mji wa Vatican na Waraka wa Laudato si.'”.Mambo manne hayo yanahusu: “matumizi endelevu ya fedha za ndani, “uwazi wa utaratibu wa manunuzi”, “kutendewa kwa usawa na kutobaguliwa kwa wazabuni” na “kuhamasisha ushindani mzuri kati ya wazabuni, hasa kupitia hatua zenye uwezo wa kupambana na mikataba isiyo halali ya ushindani na ufisadi.”

Barua 2 za Papa za Motu Proprio
16 January 2024, 18:18