Tafuta

2024.01.28 Angelus 2024.01.28 Angelus  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa atoa onyo:usizungumze kamwe na shetani

Kabla ya Sala ya Malaika,Papa Fransisko katika takafakari yake ameonya juu ya kile kinachokandamiza uhuru,matumizi kupitia kiasi,mitindo ya kisasa,hofu,kuabudu miungu ya mamlaka inayozalisha migogoro na kukimbilia silaha zinazoua.Mwaliko ni kumwomba Roho Mtakatifu ili penye vilio vya chuki kuwe na uhuru na amani.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Katika Dominika ya 4 ya  kipindi cha kawaida cha Mwaka B wa Kanisa  tarehe 28 januari 2024, baba Mtakatifu Francisko ametoa tafakari yake, kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, mjini Vatican. Akianza tafakari hiyo Papa amesema katika Injili ya siku inatuwakilisha Yesu wakati anampnya mtu aliyepegawa na pepo mbaya (Mk 1,21-28). Ambaye alikuwa ana msumbusha na kuendelea kupiga kelele (Mk 1,23.26). Shetani anafanya hivyo: anataka kumiliki kwa kutufunga mioyo.”

PAPA ALIKUWA NA WAGENI WAWILI WAKATI WA SALA YA MALAIKA WA BWAN
PAPA ALIKUWA NA WAGENI WAWILI WAKATI WA SALA YA MALAIKA WA BWAN

Na tunapaswa kuwa makini katika “minyororo” ambayo inatusonga uhuru. Kwa sababu shetani anakuondolea daima uhuru. Baba Mtakatifu kwa hiyo ameongeza kusema basi “Tujaribu kuipa majina baadhi ya minyororo ambayo inaweza kutufunga moyo kwani shetani anataka kutufunga moyo na mnyororo: “ninafikiria mitindo inayotawala ambayo inasukuma katika ukamilifu usiowezekana, matumizi kupita kiasi, na matamanio ya kuongeza raha na kupunguza maumivu, lakini kwa kuharibu mahusiano yao.  

WAKATI WA SALA YA MALAIKA WA BWANA

Na bado, kuna minyororo mingine, kuna vishawishi na masharti ambayo yanahatarisha kutojiamini, utulivu na uwezo wa kuchagua na kupenda maisha, na kuna minyoro mingine kama hofu ambayo inakufanya utazame wakati ujao kwa ugumu na mateso ambayo yanatupia makosa kwa wengine daima na baadaye kuna minyororo mingine mbaya sana  ya  kuabudu miungu ya madaraka ambayo yanazaa migogoro na mbio za silaha ambazo zinaua au hutumia dhuluma ya kiuchumi na upotoshaji wa mawazo. Kuna minyororo mingi katika maisha yetu, Papa amesisitiza.

WAAMINI WAKATI WA SALA YA MALAIKA WA BWANA
WAAMINI WAKATI WA SALA YA MALAIKA WA BWANA

Yesu alikuja kutukomboa na minyoyoro hiyo yote. Na leo hii anachangamotisha na shetani anayepaza sauti: “Tuna nini nawe (…)? Umekuja kutuangamiza (Mk 1,24), Yesu anajibu “Fumba kinywa! umtoke(Mk 1,25). Yesu anakumboa dhidi ya uwezo wa mabaya na tuzingatie vema. Tusifanya mzungumzo kamwe na shetani! Papa amekazia kusema kuwa: “Kamwe Yesu hakuzungumza na shetani; na alipojaribiwa huko jangwani, majibu yake yalikuwa maneno kutoka katika Biblia, kamwe si mazungumzo naye. Ndugu, hakuna kufanya mazungumzo na shetani! Mue waangalifu: msiongee  na shetani, kwa sababu ukianza kuzungumza naye, yeye hushinda kila wakati. Muwe waangalifu.” Kinyume chake sisi mara nyingi tunajiachia minyororo yake inafutunga kiasi kwamba hadi tusikie maumivu makali na hivyo inakuwa vigumu kujikomboa naye. Kinyume chake Yesu leo hii anatufundisha kuwa, hakuna kamwe kufanya mchakato wa mazungumzo na shetani.”

PAPA WAKATI WA SALA YA MALAIKA WA BWANA
PAPA WAKATI WA SALA YA MALAIKA WA BWANA

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea amesema, je ni jinsi gani ya kufanya ikiwa tunahisi kishawishi na kukandamizwa?  Tufanye mchakato na shetani? Hapana tusizungumze naye. Tunapaswa kumuomba Yesu: kuomba mahali ambapo tunahisi kwamba mnyororo wa mabaya umetufunga na hofu za kufungwa kwa nguvu zaidi. Bwana kwa nguvu za roho yake, anatamani kurudia hata leo hii na shetani akisema: “Ondoka, mwache kwa amani, moyo ule, usigawanye ulimwengu, familia, jumuiya zetu, ziache ziishi kwa utulivu, kwa sababu yachanue kwao matunda ya Roho yangu na siyo ya kwako.” Ndivyo Yesu anasema.” Papa alikazia kusema.  Kwa sababu kati yao utawala upendo, furaha, upole na katika nafasi ya vurugu na sauti za chuki kuwepo uhuru na amani, heshima na utunzaji wa wote”. Hiyo ndiyo anataka Yesu na kukabidhi ndoto hii ya uhuru kwetu, kwa ulinzi wetu na siyo kuzungumza na shetani na sala zetu ambazo zinaruhusu Yeye kutuponesha. Baba Mtakatifu Francisko ameomba kwa hiyo: “kujiuliza: Je ninataka kweli uhuru kutoka katika minyororo ambayo imenifunga moyo? Na baadaye, ninajua kusema“hapana” kwa vishawishi vya ubaya, kabla havijanisonga katika roho? Hatimaye ninamwomba Yesu, ninamruhisi atende kwangu ili kuniponesha ndani? Bikira Mtakatifu atulinde na mabaya.

TAFAKARI YA PAPA WAKATI WA ANGELUS 28 JANUARI
28 January 2024, 15:07