TETEMEKO LA ARDHI HUKO PWANI MASHARIKI YA  JAPAN. TETEMEKO LA ARDHI HUKO PWANI MASHARIKI YA JAPAN.   (AFP or licensors)

Papa atuma salamu za rambirambi huko Japan

Kufuatia na Tetemeko la Ardhi nchini Japan,Papa ametuma salamu za rambirambi kuonesha uchungu na mshikamano wake katika telegramu iliyotiwa saini na Kardinali Parolin,Katibu wa Vatican.Hadi sasa waathrika wamefikia hamsini hivi.Tetemeko lilitokea Januari Mosi huko Ishikawa,pwani mashariki ya Nchi.Papa anatia moyo mamlaka na watoa huduma.

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Katika telegramu iliyotiwa saini na Kardinali Parolin, Baba Mtakatifu Francisko ameonesha masikitiko yake kwa wahanga, karibu hamsini hadi sasa wa tetemeko la ardhi lililoikumba Ishikawa tarehe Mosi Januari 2024, kwenye pwani ya magharibi mwa Nchi ya Japan. Ni mshtuko mkubwa wa aina ambayo Japan hata hivyo unajua vizuri na nchi hiyo imejifunza kwa muda mrefu kukabiliana nayo. Lakini kipimo cha 7.6 cha Richter cha tetemeko la ardhi kwa bahati mbaya liliacha njiani vifusi na  waathirika  48 hivi  kulingana na idadi iliyosasishwa zaidi.

Watu walionusurika katika tetemeko la ardhi huko Japan
Watu walionusurika katika tetemeko la ardhi huko Japan

Katika mkasa huo  umeibua uchungu mkubwa kwa  Baba Mtakatifu Papa ambaye kwa njia ya telegram Kardinali Pietro Parolin anabainisha kuwa anahakikishia “ mshikamano wake kwa wale wote ambao wameathiriwa na janga hili, pamoja na ukaribu wake wa kiroho na sala, kwa ajili ya marehemu, kwa ajili ya wale wanaoomboleza kwa ajili ya hasara na kwa ajili ya kuwaokoa wale ambao bado hawajapatikana.” Kwa hiyo Baba Mtakatifu anawatia moyo kwa kuwatumia baraka kwa mamlaka ya kiraia na wafanyakazi wa dharura ambao wanasaidia manusura.”

Ili kukabiliana na dharura na kuleta msaada kwa walionusurika na tetemeko la ardhi, serikali ya Tokyo ilituma wanajeshi elfu kwenye maeneo yaliyoathiriwa. Waziri Mkuu Fumio Kishida alisema “kuokoa maisha ya binadamu ndio kipaumbele chetu, hasa wale walionaswa kati ya magofu ya nyumba.” Hata hivyo Jumanne tarehe 2 Januari 2024 tetemeko jipya la ukubwa wa 5.6 limetikisa eneo la Ishikawa ingawa mamlaka inayosimamia usimamizi wa nyuklia ilitangaza kuwa mitambo kadhaa katika eneo hilo zinafanya kazi kawaida.

Ajali ya Ndege ya Japan

Tarehe Mosi Januari 2024  Shirika la Utabiri wa Hali ya Hewa wa Japan lilikuwa limetoa onyo kali la tsunami huko Ishikawa na maonyo kama hayo, ingawa yalikuwa na nguvu kidogo, kwa maeneo mengine ya pwani ya kisiwa cha Honshu na pwani ya kaskazini ya Hokkaido. Kengele zilikuwa sikisikika za dharura kwa bahati saa chache baadaye.

Ndege  ya Shirika la Ndege Japan (JAL) imegongana na ndege nyingine ya kuokoa
Ndege ya Shirika la Ndege Japan (JAL) imegongana na ndege nyingine ya kuokoa

Janga jingine linalohusishwa na tetemeko la ardhi ni lile lililotokea tarehe 2 Januari 2024 alasiri huko jijini Tokyo, wakati ndege ya Shirika la Ndege la Japan 516(JAL) ilipoigonga Ndege ya Walinzi wa Pwani ilipokuwa ikitua, iliyokuwa ikienda katika kazi ya uokoaji kwa waathrika wa tetemeko la ardhi. Watu watano kati ya sita waliokuwa kwenye ndege hiyo kwa bahati mbaya walikufa kutokana na athari hiyo, huku abiria 379 waliokuwa kwenye ndege iliyopangwa hawakujeruhiwa, wote wakiwa salama licha ya ndege hiyo kuwaka moto ilipogusa ardhi.

 

02 January 2024, 15:03