Tafuta

Papa Paolo VI con Athenagoras Papa Paolo VI con Athenagoras 

Papa Francisko akumbuka mkutano kati ya Paul VI na Athenagoras

Mara baada ya sala ya Malaika Bwana katika siku ya Epifania,Papa alizungumzia juu ya miaka 60 tangu mkutano kati ya Kiongozi wa Kanisa katoliki na la Kiorthodox,kuwa ni ishara ya kihistoria ya udugu iliyofanywa huko Yerusalemu na hakusahau kutaja migogoro inayomwaga damu huko Palestina,Israel,Ukraine na maeneo mengine ulimwenguni.Ametoa rambirambi kwa shambulio la Iran na salamu kwa Utoto Mtakatifu wa Kimisionari katika siku yao 6 yao.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Ilikuwa mnamo tarehe 5 Januari 1954 ambapo huko Yerusalemu kulitokea tukio la Mkutano kati ya Papa Paulo VI na Patriaki wa Kiekumeni Athenagoras, mkutano ambao uliashiria mabadiliko katika uhusiano kati ya Wakatoliki na Waorthodox baada ya milenia ya kutengwa kwa pande zote. Ni katika Mutadha huo ambapo Baba Mtakatifu Francisko, mara baada ya Tafakari na sala ya Malaika wa Bwana, manamo arehe 6 Januari 2024 kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican kusali na kusheherekea Siku Kuu Epifania, yaani Tokeo la Bwana. Baba Mtakatifu Francisko  kwa njia hiyo alianza kusema kuwa: “Miaka 60 iliyopita, katika siku  kama hizi hizi, Papa Mtakatifu Paulo wa Sita na Patriaki wa Kiekumeni Athenagoras walikutana huko Yerusalemu, wakivunja ukuta wa kutoweza kuungana ambao kwa karne nyingi ulikuwa umewatenga Wakatoliki na Waorthodox. Tujifunze kutokana na kukumbatiana wale wakuu wawili wa Kanisa kwenye njia ya umoja wa Kikristo, huku tukiomba pamoja, tukitembea pamoja, na tukifanya kazi pamoja.” Baba Mtakatifu ameongeza kusema “Na tukifikiria ishara hiyo ya kihistoria ya udugu iliyofanywa huko Yerusalemu, tusali kwa ajili ya amani katika Mashariki ya Kati, Palestina, Israel, Ukraine, na ulimwenguni kote. Ni wahanga wengi wa vita, vifo vingi, na uharibifu mwingi... Tuombe amani.”

Shambulio la kigaidi Kerman nchini Iran

Baba Mtakatifu Francisko aidha alielezea tena “ukaribu wangu kwa watu wa Iran, hasa kwa familia za waathrika wengi wa shambulio la kigaidi lililotokea Kerman, kwa majeruhi wengi na wale wote walioathiriwa na maumivu haya makubwa.”

Siku ya Utoto Mtakatifu wa kimisionari

Epifania ni Siku ya Utoto ya wa Kimisionari. Kwa njia hiyo Papa amewasalimia watoto wamisionari na vijana wa dunia nzima, “ninawashukuru kwa kujitolea kwao katika sala na msaada thabiti kwa ajili ya kutangaza Injili na, hasa, kwa ajili ya kukuza vijana katika nchi za utume. Asante, asante sana!”

Salamu kwa mahujaji mbali mbali

Papa amewakaribisha kwa furaha washiriki wa msafara wa kihistoria-folkloric, ambao mwaka huu wamejitolea kwa eneo la Bonde la Mto Tiber, kwa maadili yao ya kibinadamu na ya kidini. Amewasalimia waliotoka Ujerumani, vijana wa harakati ye  “Tra Noi”, “Marafiki wa historia na utamaduni wa Carovilli, kikundi cha AVIS cha Paderno Franciacorta.”  Kwa kuongezea ametoa Nami baraka zake kwa washiriki wa Maandamano makubwa ya Wafalme Watatu yanayofanyika  huko Warsaw na katika miji mingi ya Poland. Na aliwatakia kila mmoja Siku kuu njema ya Tokeo la Bwana. Aliwaomba waendelee kumuombea na kusonga mbele kwa ujasiri. “Bwana awabariki. Mlo mwema na mchana mwema.”

08 January 2024, 11:16