Papa Francisko ameonesha wasiwasi wa kuzaliwa watoto Italia kuwa ni janga
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Jumamosi tarehe 20 Januari 2024, Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican na Wanachama wa Chama cha Ufadhili na Uboreshaji wa Mamlaka za Mitaa(ASMEL) nchini Italia. Akianza hotuba yake amefutahisi kukutana chama hicho “kilichoanzishwa mwaka wa 2010 ili kuchangia katika utendaji mzuri wa Mamlaka za Mitaa za Italia, kulingana na kanuni ya ufadhili, inayopendwa na mafundisho ya kijamii ya Kanisa.” Papa amesema kwamba maeneo wanayotoka yana uzoefu wa baadhi ya kinzani za jamii ya sasa na muundo wake wa maendeleo. Manispaa ndogo, hasa zile ambazo ni sehemu ya yale yanayoitwa maeneo ya ndani, na ambayo ni mengi, lakini mara nyingi hupuuzwa na kujikuta katika hali ya kuwekwa kando.
Papa amesema kwamba wananchi wanaoishi huko, sehemu kubwa ya idadi ya watu, wanakabiliwa na mapungufu makubwa katika suala la fursa, na hii inabakia kuwa chanzo cha ukosefu wa usawa. Msingi wa mapungufu haya ni ukweli kwamba ni ghali sana kutoa maeneo haya kiasi sawa cha rasilimali kama maeneo mengine ya nchi. Kwa njia hiyo Papa amesema kwamba, hapa tunaona mfano halisi wa utamaduni wa kutupa na hivyo “kila kitu kisichofaa katika faida kinatupwa.” Hii inazua mzunguko mbaya hasa kwa ukosefu wa fursa mara nyingi husukuma sehemu inayovutia zaidi ya idadi ya watu kuondoka na hii inafanya maeneo ya pembezoni kuwa chini na ya kuvutia, zaidi na zaidi kutelekezwa kwao wenyewe. Wale waliosalia hasa ni wazee na ambao wanaohangaika zaidi kutafuta njia mbadala. Na matokeo yake, hitaji la hali ya ustawi linaongezeka katika maeneo hayo, wakati rasilimali za kukabiliana nayo zinapungua.
Kupungua kwa watu katika maeneo ya ndani
Kuna kipengele kingine cha nguvu hii, Papa ameongeza . Ni katika maeneo ya ndani, ya kando ambayo wengi wa urithi wa asili hupatikana (misitu, maeneo ya hifadhi, na kadhalika): kwa hiyo ni ya umuhimu wa kimkakati katika suala la mazingira. Lakini kupungua kwa kasi kwa idadi ya watu kunafanya iwe vigumu zaidi kutunza eneo hilo, ambalo wakazi wa maeneo haya wamekuwa wakitekeleza kila mara. Maeneo yaliyotelekezwa yanakuwa tete zaidi, na kukosekana kwa utulivu kwao kunakuwa sababu ya maafa na dharura, hasa leo hii na matukio makubwa ya mara kwa mara: kwa mfano mvua za msimu, mafuriko, maporomoko ya ardhi; ukame na moto; dhoruba za upepo na kadhalika.
Kusikiliza kilio cha dunia ni kusililiza kilio cha maskini
Kutazama maeneo haya, Baba Mtakatifu amesema tunathibitisha kwamba kusikiliza kilio cha dunia kunamaanisha kusikiliza kilio cha maskini na waliotengwa, na kinyume chake: katika udhaifu wa watu na mazingira tunatambua kwamba kila kitu kimeunganishwa! -, na kwamba utafutaji wa suluhisho unahitaji kujifunza pamoja matukio ambayo mara nyingi hufikiriwa kuwa tofauti. Kwa hiyo kila kitu kimeunganishwa.” Papa amesisitiza. Hata hivyo, Papa amewaeleza jinsi ambavyo hayo yote wanayatambua vizuri. Na kwa hiyo amependa kuwashukuru kwa kujitolea kwao na kwa kazi yao, ambayo inataka kuchangia kulinda hadhi ya utu wa watu na kutunza nyumba yetu ya pamoja, hata kwa rasilimali chache na katikati ya shida elfu. Kuna hitaji kubwa la kujitolea huku, kwa hivyo Papa amewaalika wasiache kuwa makini na wasikatishwe tamaa.
Kitu kikubwa cha ubora wa maisha na utunzaji wa maeneo
Kuna kitu kikubwa kilichopo ambacho ni ubora wa maisha na utunzaji wa maeneo wanayotoka, ambayo pia yanastahili juhudi zote. Siku zote, na hata leo hii, maeneo ya pembezoni ndiyo yanaweza kugeuzwa kuwa maabara za uvumbuzi wa kijamii, kuanzia mtazamo, ule wa pembezoni - unaotuwezesha kuona mabadiliko ya jamii kwa njia tofauti, kugundua fursa ambapo wengine hutazama vikwazo, au rasilimali katika kile ambacho wengine wanakichukulia kuwa ni upotevu. Matendo bunifu ya kijamii, ambayo hugundua upya aina za kuheshimiana na usawa na ambayo huweka upya uhusiano na mazingira katika ufunguo wa utunzaji, kutoka katika aina mpya za kilimo hadi uzoefu wa ustawi wa jamii, zinaomba kutambuliwa na kuungwa mkono, ili kuchochea dhana mbadala kwa manufaa ya wote.
Teknolojia mpya pamoja na akili bandia
Papa akifikiria eneo la kujitokea amependa kupendekeza mojawapo ya maeneo mengi ya kuzingatia: lile la utafutaji wa mahusiano mapya kati ya umma na binafsi, hasa sekta ya kijamii ya kibinafsi, ili kuondokana na mbinu za zamani na kutumia kikamilifu uwezekano ambao sheria hutoa leo hii. Uhaba wa rasilimali katika maeneo ya pembezoni huwafanya watu kuwa tayari zaidi kushirikiana kwa kile kinachoonekana kuwa ni manufaa ya wote; Hii inatoa fursa ya kufungua kazi za ushiriki, kuhimiza kwa upya demokrasia katika maana yake pana. Mwelekeo mwingine unaotia matumaini ni ule wa teknolojia mpya, hasa matumizi ya aina mbalimbali za akili bandia. Tunaweza kugundua jinsi gani nguvu hii inaweza kuwa ya manufaa ikiwa haitumiwi kwa uharibifu, lakini kwa mantiki ya utunzaji, ikiwa na maana ya utunzaji wa watu, utunzaji wa jamii, utunzaji wa wilaya na utunzaji wa nyumba ya pamoja," Papa ameeleza.
Kupungua kwa watoto
Kwa kuongeza Papa Francisko ameonesha hata wasi wasi wake kwamba: “Na kwa kuzungumza juu ya matibabu, nina wasiwasi juu ya kuzaliwa watoto wachache. Kuna utamaduni wa kupunguza idadi ya watu ambao unatokana na kuzaliwa kwa watoto wachache. Ni kweli, mtu yeyote anaweza kuwa na mbwa, lakini tunahitaji kuwa na watoto. Italia, Hispania ... wanahitaji watoto. Hebu tufikiria kwamba moja ya nchi hizi za Mediterania zina wastani wa umri wa miaka 46! Ni lazima tulichukulie kwa uzito tatizo la uzazi, tulichukulie kwa dhati maana mustakabali wa nchi yenu huko hatarini Papa amesisitiza tena “mustakabali huko hatarini.” Katika hili Papa Francisko ameongeza kusema: “Kuwa na watoto ni jukumu la kuishi na kusonga mbele. Fikirieni juu ya hili: sio tangazo la wakala wa kuzaliwa, lakini ninataka kusisitiza juu ya janga la watoto wachache, ambapo mnahitaji kufikiria sana na kwa umakini.” Papa amewatakia kila la heri katika kazi yao na kuwabariki wao na wapendwa wao kwa moyo wote. Na tafadhali, amewaomba wamwombee.