Papa Francisko ametoa wito kuombea nchi ya Nicaragua
Na Angella- Rwezaula.
Uwanja wa Mtakatifu Petro, mjini Vatican katika mwanzo wa Mwaka, tarehe Mosi Januari 2024, Baba Mtakatifu Francisko akiwa katika dirisha la Jumba la Kitume, mara baada ya kumaliza misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na baada ya sala ya Malaika wa Bwana alisema: “Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Italia kwa matashi mema aliyoniandikia katika ujumbe wake wa mwisho wa mwaka; Ninawajibu kwa moyo wote kuomba baraka za Bwana juu ya utumishi wake kwa nchi.”
Papa ameombea Nicaragua
Baba Mtakatifu Francisko akiendelea amesema: “Ninafuatilia kwa wasiwasi mkubwa kile kinachotokea Nicaragua, ambako Maaskofu na mapadre wamenyimwa uhuru wao. Ninawaeleza wao, familia zao na Kanisa zima nchini ukaribu wangu katika maombi. Pia ninawaalika ninyi nyote mliopo hapa na Watu wote wa Mungu kusali kwa bidii, huku nikitumaini kuwa kutafuta daima njia ya mazungumzo ili kuondokana na matatizo. Hebu leo tuiombee Nicaragua."
Salamu kwa mahujaji mbali mbali
Papa Francisko amewatakia heri wapendwa Warumi na mahujaji wote waliokuwapo katika uwanja wa Mtakatifu Petro. “Nawasalimu washiriki wa hafla ya "Amani katika nchi zote", iliyoandaliwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, pia katika miji mingine ya ulimwengu; pamoja na Harakati la Matendo ya kupinga Vurugu la Ulaya. Aidha Papa Na amekumbuka kwa shukrani mipango mingi ya sala na kujitolea kwa amani ambayo inafanyika Siku hii katika mabara yote, ikikuzwa na jumuiya za kikanisa; hasa alipenda kutaja ile ya kitaifa iliyofanyika huko Gorizia katika usiku wa tarehe 31 Desemba 2023. Papa kwa kuongeza: " Na tafadhali, tusisahau Ukraine, Palestina, Israel, ambazo ziko vitani. Tuombe amani ije, sote kwa pamoja….."
Kwaya ya Watoto wa Kipoland na kiukraine
Papa amewasalimia kwaya ya watoto wa Poland na Kiukreni walioleta ujumbe wa amani kwenye Madhabahu ya Kifransiskani huko Toscana, Umbria na Lazio nchini Italia; pamoja na wanafunzi wa "chuo cha Manhattan cha New York, kikundi cha Fraterna Domus na waamini wa La Valletta Brianza na Casatenovo. Bikira Maria awaunge mkono Mama Mtakatifu wa Mungu, na kwa maombezi yake ya uzazi, nia na dhamira ya kuwa wapenda amani kila siku, kila siku hata ya mwaka mpya, kila siku, wapenda amani. "Na tafadhali msisahau kuniombea. Mlo na Mchana mwema, kwaheri ya kukuona!"