2024.01.03 Papa Francisko wakati wa katekesi yake ametoa wito wa kuombea amani duniani. 2024.01.03 Papa Francisko wakati wa katekesi yake ametoa wito wa kuombea amani duniani.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa Francisko awakumbuka wahanga wa migogoro:vita ni wazimu na kushindwa

Mara baaada ya katekesi yake Papa kwa waamini na mahujaji katika ukumbi wa Paulo VI ametoa maombi yake tena kwa ajili ya maeneo maeneo ya moto wa silaha na uharibifu duniani unaozidi kuongezeka.Amewakumbuka Wapalestina,Waisraeli na Waukraine.Vile vile ni kwa Warohingia na waathirika wa tetemeko la ardhi na ajali ya ndege huko Japan.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, mara baada ya Katekesi yake ya kwanza kwa mwaka huu 2024, akiwasalimu watu mbali waliofika katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican, tarehe 3 Januari, ametoa wito wa kuombea zawadi ya amani duniani. Kwa namna hiyo ameomba kusali kwa namna ya pekee kwa ajili ya kile kinachoendelea katika Nchi za Mashariki na katika moyo wa Ulaya. Na mwishowe wazo kwa idadi ya watu ambayo amezungumza mara kadhaa. ‘Tunawaombea watu wa Palestina, Israeli, Ukraine na maeneo mengine mengi ambapo kuna vita. Na tusiwasahau ndugu zetu wa Rohingya wanaoteswa. Tusiwasahau watu walio vitani. Vita ni wazimu. Vita siku zote ni kushindwa, daima ni kushindwa” Na tuombe kuwa na  moyo nyeti kuelekea maskini na wakimbizi.

Kama kawaida yake Papa kusalimiana na wote katika ukumbi wa Paulo VI
Kama kawaida yake Papa kusalimiana na wote katika ukumbi wa Paulo VI

Baba Mtakatifu akitoa salamu za mahujaji wa Poland, ametoa mwaliko wa  kumwomba Mwenyezi Mungu, “atujalie moyo unaojali mahitaji ya maskini, wakimbizi na wahanga wa vita. Kwa maombezi ya Maria, Mama wa Mungu, “Ninamwomba Bwana zawadi ya amani, na niwakubariki kutoka ndani ya moyo wangu!” Zaidi ya hayo, katika kutoa salamu za upendo pia kwa watakaoshiriki kipaimara na vijana wa Jimbo la Latina, aliwahimiza kutunza, kama Maria, kutafakari na kufuata Neno lililofanyika mwili huko Bethlehemu, ili kueneza miongoni mwa marafiki na wasindikizaji  wao ujumbe wa heri na amani. Papa akizungumza tena kuhusu amani kwa waamini wanaozungumza Kiarabu alitoa mwaliko kwamba, na “mwanzo wa mwaka mpya,  uwe wa kudumisha sala na toba ili waweze kupata ndani yake amani na furaha ambayo Mungu anataka kwa ajili yetu. Bwana awabariki wote  na kuwalinda daima kutoka kwa uovu wote.”

Kusalimia watoto na kuwakumbatia watoto
Kusalimia watoto na kuwakumbatia watoto

Katika salamu zake kwa mahujaji wanaozungumza Kiingereza, Papa pia amewaombea wahanga na waokoaji wa tetemeko la ardhi huko Japan, pia akielekeza wazo kwa wale wanaofanya kazi ili kukabiliana na uharibifu na vifo vilivyosababishwa na ajali ya ndege  huko jijini Tokyo nchini Japan. Idadi ya waliopoteza maisha katika tetemeko la mwaka mpya imeongezeka na kufikia watu 64, lakini hali ni mbaya mno huku mitetemeko mingine kadhaa ikiendelea kutikisa eneo hilo. Ukubwa uliorekodiwa kwa saa 4.54 za ndani  ikiwa ni saa (8.54 usiku wa manane nchini Italia) katika mkoa wa Noto, katika mkoa wa Ishikawa, kwa kina cha kilomita 10 ulikuwa wa ukubwa wa 5.5.  Hata hivyo hakuna maonyo ya tsunami yaliyotolewa.  Japokuwa “ karibu hakuna nyumba iliyosimama. Zote zimeharibiwa kwa kiasi au kabisa,” alisema Masuhiro Izumiya, meya wa jiji la Suzu, ambalo lilipata uharibifu mkubwa.

Wito wa Papa kwa wanaoteseka na vita duniani 3 Januari 2024
03 January 2024, 12:51