2024.01.04  Vijana wa Udugu "Fraternite MIssionnaire des Citas" na Papa. 2024.01.04 Vijana wa Udugu "Fraternite MIssionnaire des Citas" na Papa.  (Vatican Media)

Papa Francisko:Fungueni mioyo,mikono na masikio kwa ukaribisho wa dhati

Papa akikutana na vijana wa “Fraternité Missionnair des Cités”amewakabidhi ujumbe wake ambapo anasema Wachungaji huko Bethelehemu walitangaziwa Injili wakiwa wa kwanza na udugu ni chachu ya amani ambayo vitongoji vyetu vinahitaji.Lazima kuonesha ukarimu mpya wa uso wa huruma ya Mungu kwa wale wanaoishi pembezoni mwa miji,kwani hawazingatiwi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na chama wa Udugu wa Kimisionari wa Miji (Fraternité missionnaire des Cités, Alhamisi tarehe 4 Januari 2024 wakati wa hija yao jijini Roma. Katika Hotuba aliyowakabidhi, Baba Mtakatifu anawaandikia kuwa wamefika kujiimarisha kiroho kwenye makaburi ya Mtakatifu Petro na Mtakatifu Paulo, ili kupata kutoka katika chemchemi hai za Kanisa upendo wa Kristo anayejitoa bila kukoma kwa watu wote. Roho Mtakatifu, kwa mfano na maombezi ya nguzo hizi mbili za Kanisa, afufue ndani yao msukumo wa ukarimu na wa kimisionari wa Kanisa la kwanza. Tukiwa bado tumezama katika mwanga wa Noeli, aidha Baba Mtakatifu anawaalika kutafakari Pango la kuzaliwa kwa Yesu. Tunaona mahali rahisi na maskini, kitongoji, cha pembeni cha wakati huo. Wachungaji wanaliokwenda kumtazama horini, walikuwa ni watu waliofukuzwa na sifa mbaya. Lakini walikuwa wa kwanza kutangaziwa Injili ya wokovu. Ni maskini lakini wana moyo wa kujitolea. Huu pia ni uzoefu wao. Na sio lazima kwenda mbali sana, katika huduma yao kwa moyo wa miji, kugundua sehemu za nje za jamii zetu, ambazo mara nyingi ziko karibu, katika ujirani wao, kwenye kona ya barabara, kwenye barabara kuu za kutua sawa.

Kubeba ujumbe wa wachungaji:"Msiogope

Baba Mtakatifu anabainisha kuwa “Ni juu yao kubeba ujumbe uliotolewa kwa wachungaji ukisema: “Msiogope; tazama, mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote” (Lk 2:10). Kwa hiyo, wasiogope kuacha usalama wao ili kushiriki maisha ya kila siku ya kaka na dada zao. Hata kati yao, wengi wana mioyo wazi na kusubiri, bila kujua, kwa tangazo la furaha.” Baba Mtakatifu Francisko amewaalika aidha kuishi udugu kwa ukarimu katikati ya vitongoji, kufungua mioyo, mikono, masikio, kwa ukaribisho wa dhati. Udugu ni chachu ya amani ambayo vitongoji vinahitaji: inaruhusu kila mtu kujisikia kukaribishwa kama alivyo, mahali alipo.

Kila mkutano gundueni uwepo wa Bwana katika ndugu

Baba Mtakatifu anawasihi, katika kila mkutano, wagundue uwepo wa Bwana Yesu ndani ya ndugu zao, na kuonesha uwepo wa Mungu mwenye huruma, Mungu anayetaka kujieleza na kutenda kupitia ishara zao, maneno yao, uwepo wao rahisi; Mungu mvumilivu anayetembea kwa mwendo wa kila mtu, kwa majeraha yao, maasi yao, hasira yao. Pia Papa Francisko anajua ni kiasi gani cha vurugu, kutojali na chuki wakati mwingine vinaweza kuashiria ujirani wao kwa sababu  leo hii wana utume wa ujasiri na muhimu wa kuleta ukaribu wa Mungu, huruma na huruma kwa watu ambao mara nyingi wamenyimwa utu na upendo. Baba Mtakatifu Francisko, amewashukuru kwa kile wanachofanya na kuwatia moyo waendelee. Amewakabidhi kila mmoja wa na washiriki wote wa Udugu wao kwa maombezi ya Bikira Maria na amewabariki kutoka ndani ya moyo wake. Na wasisahau kusali kwa ajili yake.

Udugu wa Kimisionari wa Barabarani
04 January 2024, 16:50