Papa Francisko:Kanisa litambulike kwa matendo mema ya washiriki wake
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Baba Mtakatiru Francisko, Alhamisi tarehe 4 Januari 2024, amekutana wa wakilishi wa Chuo Kikuu Katoliki cha Murcia. Katika hotuba yake anawashukuru kuwepo hapo katika Nyumba ya Petro, kama wawakilishi wa chuo kikuu cha Murcia nchini Hispania katika matazamio ya maadhimisho ya miaka 25 ya kuanzishwa kwa chuo hicho mwanzilishi wake José Luis Mendoza Pérez. Askofu wao alimfafanua kuwa “ndugu, mwamini, shahidi wa upendo wa Mungu, aliyetaka kutenda mema”. Haya ni maneno mazuri, hakuna aliyekamilika, lakini sote tuna uwezo wa kupenda, na kukumbuka kuwa hilo ndilo linatuleta karibu na Mungu na huruma yake.
Baba Mtakatifu amesema kuwa Padre José Luis alitaka kuacha urithi katika chuo kikuu kiwe cha kimisionari, cha uinjilishaji na uwepo wa kina, kilichozaliwa kutoka moyoni mwa Kanisa na kuhuishwa na nguvu ya upendo wa Mungu. Kwa sababu “kila jambo ambalo Mkristo anafanya kama mshiriki wa Kristo, wa Kanisa hilo ambalo ni mama yetu, lazima liwe la kimisionari, kueneza injili, na hasa kwa sababu hii, lazima lihusishwe na ukweli wa kibinadamu, na maswali mazito ya mwanadamu, liwe la kudumu.”
Hili ndilo tumaini la Baba Mtakatifu kwao wote kwamba wanaendelea kufanya kazi kutoka moyoni mwa Kanisa kumpeleka Yesu Kristo kwa kila mtu anayekaribia madarasa yao, maisha yao, ili kuunda watu wenye uwezo wa kumkaribisha Mungu na kutoa ushuhuda kwake katika eneo lolote, kujenga jumuiya ya kidugu ambapo Kanisa linatambulika katika matendo mema ya washiriki wake. Papa Francisko amewashukuru kwa kile wnawachofanya na Yesu awabariki na Bikira wa huruma a walinde. Na tafadhali wasisahau kumuombea.