Papa Francisko:kufuata,kukaa na kutangaza Neno la Bwana kwa wengine

Kumfuata Yeye,kukaa na Yeye na kumtangaza Yeye ndiyo maneno matatu ya wito kutoka katika Injili ya Yohane ambayo Papa Francisko amefafanua kwenye tafakari yake,kabla ya sala ya Malaika wa Bwana.Hata sisi tufanye kumbu kumbu ya mkutano wa kwanza wa Bwana.Na tujiulize kama bado sisi ni wafuasi wapendwa.

Na Angella Rwezaula- Vatican.

Katika Dominika ya Pili ya kipindi cha Kawaida cha Mwaka B, tarehe 14 Januari 2024, Baba Mtakatifu Francisko ametoa tafakari yake kupitia dirisha la Nyumba ya Kitume mjini Vatican kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro. Akianza tafakari kuhusu Somo la Injili alisema: "Injili ya leo inawakilisha mkutano wa Yesu na wanafunzi wa kwanza (Yh 1,35-42). Picha hii inatualika kufanya kumbu kumbu ya mkutano wa kwanza na Yesu. Kila mmoja wetu alipata kuwa na mkutano wa kwanza na Yesu akiwa mtoto, barubaru, kijana, na mtu mzima Ni lini nilikutana na Yesu mara ya kwanza? Tufanye kumbukumbu. Na baada ya wazo hilo, na kumbukumbu hiyo, tupyaishe furaha ya kumfuata na tujiulize maana ya kuwa mwanafunzi wa Yesu: je ina maana gani ya kuwa mwanafunzi wa Yesu. Kwa mujibu wa Injili, Papa ameongeza: "tunaweza kuchukua maneno matatu: kumtafuta Yesu, kukaa na Yesu, kumtangaza Yesu." Kwa hiyo: "Tafuta, kaa, tangaza." Papa Francisko amesisitiza.

Waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro katika sala ya Malaika wa Bwana 14 januari 2024
Waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro katika sala ya Malaika wa Bwana 14 januari 2024

Baba Mtakatifu akianza kufafanua awali ya yote kutafuta. Mitume wawili shukrani kwa ushuhuda wa Yohane Mbatizaji, walianza kumfuata Yesu na Yeye,“kwa kuona kwamba wao wanafuata aliuliza: “Mnatafuta nini? (Yh 1,38). Yalikuwa ni maneno ya kwanza ya Yesu  aliyowaelekea wao: kwanza aliwaalika kutazama ndani mwao, kujiuliza shauku zao, ndani ya mwoyo wao. Bwana hataki kufanya propaganda, hataki followers , fuasi za kijuu, juu bali watu ambao wanajiuliza na kuacha waalikwe na Neno lake. Zaidi ya hayo, ili kuwa mfuasi wa Yesu lazima kwanza kabisa kumtafuta, kuwa na moyo ulio wazi, kumtafuta na sio kutoshiba au kutosheka. Kwa njia hiyo wanafunzi walikuwa wanatafuta nini,ndipo linakuja neno la pili la kukaa. Baba Mtakatifu amebainisha kuwa "Walikuwa hawatafuti habari au maelezo kuhusu Mungu, wala ishara au miujiza, lakini walitamani kukutana na Yesu, kukutana na Masiha, kuzungumza na Yeye, kukaa na Yeye na kumsikiliza."

Swali la kwanza walilofanya ni lipi: Unaishi wapi? (Yh 1,38). Na Kristo aliwaalika kukaa na Yeye: “Njooni na mwone” (Yh 1,39). Kukaa na Yeye, kubaki na Yeye, ndiyo jambo muhimu zaidi, kwa wanafunzi wa Bwana. Hii  siyo nadharia, hapana ni mkutano, ni kwenda na kuona anakoishi Bwana na kukaa na Yeye. “Kukutana na Bwana na kukaa na Yeye.” Papa amerudia maneno hayo. Wanafunzi walikuwa wakimtafuta Yesu, kisha wakaenda pamoja Naye na kukaa naye jioni nzima.

Licha ya baridi kali, waamini wamesali sala ya Malaika wa Bwana na Papa
Licha ya baridi kali, waamini wamesali sala ya Malaika wa Bwana na Papa

Baada ya kukaa naye walirudi kutangaza. Kwa njia hiyo "Kutafuta, kukaa, kutangaza." Je, ninamtafuta Yesu? Je, ninakaa ndani ya Yesu? Je, nina ujasiri wa kumtangaza Yesu? Mkutano ule wa kwanza na Yesu ulikuwa uzoefu wenye nguvu sana kiasi kwamba mitume wale wawili watakumbuka daima saa: ilikuwa karibu saa kumi kamili za mchana. Hii inaonesha nguvu ya mkutano huo. Na mioyoni mwao walikuwa wamejaa furaha na ambayo walihisi haraka hitaji la kutangaza zawadi waliyoipokea. Kiukweli mmoja wa wawili, Andrea alifanya haraka kumshirikisha  kaka yake Petro na kumpeleka kwa Bwana. Kutafuta Bwana, na kukaa na Yeye

Baba Mtakatifu Francisko ameongeza kusema kuwa , "leo pia tunakumbuka kukutana kwetu na Bwana kwa mara ya kwanza. “Kila mmoja wetu amepata kukutana mara ya kwanza, ndani ya familia na nje yake... Nilikutana na Bwana lini? Ni lini Bwana aligusa moyo wangu?” Na tujiulize: je, sisi bado ni wanafunzi katika upendo na Bwana, tunamtafuta Bwana, au tumetulia katika imani iliyofanywa kwa mazoea? Je! Ninajua kukaa katika maombi na Bwana, kukaa kimya naye? Na kisha tunahisi shauku ya kushiriki, "kutangaza uzuri huu wa kukutana na Bwana." Maria Mtakatifu, mwanafunzi wa kwanza wa Yesu, atupatie shauku ya kumtafuta, shauku ya kuwa Naye na shauku ya Kumtangaza Yeye." Papa Francisko alihitimisha.

Tafakari ya Papa 14 Januari 2024
14 January 2024, 12:30