2024.01.01 Sala ya Malaika wa Bwana katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican. 2024.01.01 Sala ya Malaika wa Bwana katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican.  (Vatican Media)

Papa Francisko:Leo hii kuna haja ya kukataa ukandamizaji,umiliki na vurugu

Kabla ya sala ya Malaika wa Bwana katika siku ya kwanza ya mwaka 2024,Papa Francisko amejikita kuelezea Siku Kuu ya Mama wa Mungu.Kwa ukimya wake na unyenyekevu wake,Maria ndiye ‘Kanisa kuu’ la kwanza la Mungu,mahali ambapo Yeye na mwanadamu wanaweza kukutana.Kuna wanawake wengi wa ukimya."

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Tarehe Mosi Januari 2024,  katika siku ambayo ni ya  kwanza ya mwaka mpya, Baba Mtakatifu Francisko, mara baada ya Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, vile vile ametoa tafakari yake kwa waamini na mahujaji waliofika katika kusali Sala ya Malaika wa Bwana katika Siku Kuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu, sambamba na Siku ya 57 ya Amani Duniani 2024. Baba Mtakatifu akianza tafakari amesema: “Katika siku hii ambayo tunasherehekea Maria Mtakatifu  Mama wa Mungu, tuweke wakati mpya ambao tumepewa chini ya mtazano wake. Yeye atuweke salama mwaka huu. Leo Injili inatufunulia kwamba ukuu wa Maria haujumuishi katika kutenda tendo fulani la ajabu; bali, wakati wachungaji, wakiwa wamepokea tangazo kutoka kwa Malaika, waliharakisha kuelekea Bethlehemu (taz. Luka 2:15-16), na yeye alikaa kimya.” Ukimya wa Mama ni sifa nzuri.

Waamini na mabango yao walioshiriki sala ya Malaika wa Bwana
Waamini na mabango yao walioshiriki sala ya Malaika wa Bwana

Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa hii, "sio kukosekana kwa maneno rahisi, lakini ni kimya kilichojaa mshangao na kuabudu maajabu ambayo Mungu anayotenda. “Maria Mtakatifu Luka  alisema kuwa […] aliweka mambo haya yote, akiyatafakari moyoni mwake” (2,19). Kwa njia hiyo alimpatia nafasi yeye aliyezaliwa; kwa ukimya na kuabudu, alimweka Yesu katikati na kumshuhudia kama Mwokozi. Kwa hiyo Maria ni Mama wa ukimya; Maria, ni  Mama wa kuabudu. Alimweka katika nuru, bila kuchukua nafasi yake. Atakaa kimya hata chini ya msalaba, katika saa yenye giza kuu, na ataendelea kumpatia nafasi na kumzaa kwa ajili yetu. Mtawa wa karne ya ishirini na mshairi aliandika: “Bikira, kanisa kuu la Ukimya / […] unapeleka mwili wetu mbinguni / na Mungu katika mwili” (D.M. TUROLDO,  Sifa kwa Bikira. ‘Via pulchritudinis’, Bologna 1980, 35 ).

Hata kundi la Ukraine lilikuwa uwanja wa Mtakatifu Petro
Hata kundi la Ukraine lilikuwa uwanja wa Mtakatifu Petro

Kanisa Kuu la Kimya: ni picha nzuri. Kwa ukimya wake na unyenyekevu wake, Maria ndiye ‘kanisa kuu’ la kwanza la Mungu, mahali ambapo Yeye na mwanadamu wanaweza kukutana. Lakini hata mama zetu, pamoja na utunzaji wao uliofichika, kwa uangalifu wao, mara nyingi ni makanisa mazuri ya ukimya. Wanatuleta ulimwenguni na kisha kuendelea kutusindikiza, mara nyingi bila kutambuliwa, ili tuweze kukua. Tukumbuke hilo: upendo haukandamizi kamwe, upendo hutoa nafasi kwa mwingine. Upendo hutufanya kukua. Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza kuwa, mwanzoni mwa mwaka mpya tunamtazame Maria na kwa moyo wa shukrani, pia tunawaza kuwatazama akina mama, ili tujifunze kwamba upendo unaokuzwa zaidi ya yote katika ukimya, unaojua jinsi ya kutoa nafasi kwa wengine. kuheshimu utu wao, kuacha uhuru wa kujieleza, kukataa kila aina ya milki, uonevu na unyanyasaji. Kuna hitaji kubwa sana  leo hii! Haja kubwa ya ukimya wa  kusikiliza kila mmoja."

Tangazo linasema amani ni wakati ujao
Tangazo linasema amani ni wakati ujao

"Kama vile Ujumbe wa Siku ya Amani ya Ulimwengu unavyokumbusha, Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa: “Uhuru na kuishi pamoja kwa amani kunatishwa wakati wanadamu wanapokubali majaribu ya ubinafsi, maslahi binafsi, tamaa ya faida na kiu ya mamlaka.” Upendo, kwa upande mwingine, unafanywa kwa heshima, unafanywa kwa wema: kwa njia hii huvunja vikwazo na husaidia kuishi mahusiano ya kidugu, kujenga zaidi ya haki, zaidi ya kibinadamu, zaidi ya jamii ya amani. kwa hiyo Papa ameongeza “Tusali leo hii kwa Mama Mtakatifu wa Mungu na Mama yetu, ili katika mwaka mpya tuweze kukua katika upendo huu wa upole, kimya na wa busara unaozalisha maisha, na njia zilizo wazi za amani na upatanisho duniani.”

Tafakari ya Papa wakati wa Angelus 1 Januari 20224
01 January 2024, 12:34