Kitabu cha Kardinali Semeraro kuhusu Papa  Paolo VI. Kitabu cha Kardinali Semeraro kuhusu Papa Paolo VI. 

Mtakatifu Paulo VI Mwalimu wa Mafumbo ya Kristo!

Januari 18 Nyumba ya vitabu Vatican itachapisha kitabu:Paulo VI,Mwalimu wa fumbo la Kristo”kinachokusanya mahubiri ambayo Kardinali Marcello Semeraro,Mwenyekiti wa Baraza la kipapa la Kuwatangaza Watakatifu alitoa 6 Agosti 2008 hadi 2014 katika kumbukuzi ya kifo cha Papa Montini.Kitabu kina dibaji ya Papa ambayo tunaichapisha.

Na Angella Rwezaula, - Vatican

Nina furaha kwamba Kardinali Marcello Semeraro ameamua kuchapisha mfululizo wa mahubiri yaliyofanyika katika Siku ya Kung’ara kwa Bwana, ambayo pia ni kumbukumbu ya kuaga dunia kwa Mtakatifu Paulo wa VI kutoka katika "nchi hii chungu, ya ajabu na adhimu" kama alivyoitoa kwenye Wasifu wake katika nyumba ya Baba. Nina furaha pia kwamba alichagua kufanya hivyo mwaka wa 2023, kwani ni miaka sitini imepita tangu alioituwa Yohane Battista Montini katika huduma ya Petro. Paulo VI! Mara nyingi nimekuwa nikijiuliza iwapo Papa huyu hapaswi kuchukuliwa kuwa "mfia dini"! Wakati mmoja, katika mkutano wa faragha karibu na ibada ya kutangazwa Mwenyeheri Papa Montini, pia nilimwambia Askofu Marcello. Nilimuuliza, kwa utani nusu-utani, ikiwa nilipaswa kuvaa nguo nyekundu au nyeupe za kiliturujia katika ibada. Yeye hakunielewa na aliona kuwa rangi nyekundu ndiyo iliyoagizwa katika ibada ya mazishi ya Mapapa... Nilimweleza nilichomaanisha na akabaki akifikiria pamoja nami. Kwa hakika, tarehe 15 Desemba 1969, katika fursa ya mabadilishano ya kawaida ya salamu za Noeli na Baraza la Makardinali na Curia Romana, Paulo VI alitaja ukweli kwamba Mtaguso wa II wa Vatican "ulikuwa umetoa hali ya umakini, na, katika nyanja fulani, mvutano wa kiroho “, ikiwa ni pamoja na mgogoro wa makuhani wengi. Katika muktadha huo alisema: "Hii ni taji letu la miiba." Ushauri wa kulipenda Kanisa ulikuwa kati ya maneno ya mara kwa mara na yaliyorudiwa mara kwa mara katika majisterio ya Paulo VI. Aliiona kama kioo cha kumwona Kristo, nafasi ya kukutana na Kristo na hii ilikuwa, kwake, jambo moja muhimu.

Sisi sote tunakumbuka maombi yake kwa Kristo, pekee ya lazima! Na ni upendo huu wa kipekee na kamili  kwa Kristo ambao Kardinali Semeraro alikusudia kusisitiza na mahubiri yake, aliyaweka katika muktadha katika fumbo la Kugeuza Sura. Mtakatifu Paulo VI alikuwa mtafakari, mhubiri na shahidi wa Kristo aliyegeuka sura. Inaweza kusemwa kwamba alitaka kuingia katika eneo hilo la kiinjili kama msindikizaji wa mitume watatu waliochaguliwa na Yesu. Zaidi ya hayo: hamu yake ya ndani na ya siri imekuwa daima kuwa "cum ipso in monte" na hii imefanya maisha yake yenyewe kugeuzwa sura. Nina furaha kwamba tafakari hizi zimechapishwa, kwa sababu sura ya Mtakatifu Paulo VI imekuwa ya kuvutia kwangu pia. Tayari nimesema katika tukio lingine jinsi gani baadhi ya hotuba za Papa huyo- kama zile za Manila, Nazareth... zimenipa nguvu za kiroho na kufanya mengi mazuri katika maisha yangu. Inajulikana kwamba Wosia wangu wa kwanza wa Kitume Evangelii gaudium ulikusudiwa kuwa kidogo kama upande mwingine wa sarafu ya  Wosia wa  Evangelii nuntiandi, hati ya kichungaji ambayo ninaipenda sana. Kila mtu, kwa upande mwingine, mara nyingi amenisikia nikirudia usemi ulioanguka moyoni mwangu kutoka hapo: furaha tamu na ya kufariji ya kueneza Injili. Nilirudia nilipokuwa Askofu wa Buenos Aires na ninarudia leo.

Kichwa kilichochaguliwa kwa mkusanyiko huo kinachukua maneno ya Marie-Joseph Le Guillou, Mtaalimungu mkuu Mdominikani ambaye pia ninamthamini sana. Aliiandika katika kitabu maalumu kwa ukuu wa kinabii, kiroho, kimafundisho, kichungaji na kimisionari wa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vaticani. Kutokana na hili pia, basi, ningependa kupata msukumo kabla ya kuhitimisha mistari hii ya uwasilishaji. Tukio la Jubilei ya mwaka 2025 linapokaribia, kwa hakika nimemwomba kila mtu kujiandaa kwa hilo kwa kuchukua maandiko msingi ya Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican. Sasa, katika kitabu chake, Padre Le Guillou anaelezea Mtaguso wa II wa Vatican, kama kitendo cha kutafakari Uso wa Kristo. Pia katika mwanga huu wa majisterio ya Mtaguso wa II wa Vatican, lazima isomwe tena, ichunguzwe na itekelezwe.

Kwa Mjesuit ambaye, wakati wa mkutano huko Vilnius, Lithuania, aliniuliza jinsi gani angeweza kunisaidia, nilijibu: “Wanahistoria wanasema kwamba inachukua miaka 100 kwa Mtaguso kutekelezwa. Tuko katikati. Kwa hiyo, kama mnataka kunisaidia, fanyeni kwa njia ya kuendeleza Mtaguso katika Kanisa.” Kutafakari uso wa Kristo! Katika Evangelii gaudium niliandika kwamba kila mhubiri “ni mtu wa kutafakari Neno na pia ni tafakari ya watu”. Ningependa kusema kwamba hivi ndivyo ilivyo pia kwa Kanisa la Sinodi. Kutafakari Neno na pia kutafakari kwa watu watakatifu waaminifu wa Mungu. Ninatumaini kwa dhati kwamba tafakari iliyoandikwa katika kurasa hizi pia inatia moyo kwa hili.

Dibaji ya Papa katika Kitabu kuhusu Paulo VI

Imesasishwa tarehe 18 Januari 2024 saa 9.45

17 January 2024, 16:56