Tafuta

Papa,Tokeo la Bwana:Tuwe na mtazamo kuelekeza katika nyota kama Mamajusi

Papa Francisko ameadhimisha Misa Takatifu ya Tokeo la Bwana katika Kanisa la Mtakatifu Petro,mbele ya waamini elfu sita,huku akitafakari namna mamajusi walivyokabiliana na safari ndefu ya kumfikia Yesu:hatumpati Mungu kwa kubaki katika itikadi fulani nzuri ya kikanisa,bali kwa kutafuta ishara za uwepo wake katika hali halisi ya kila siku,hasa kwa kugusa maskini na Kanisa linatafuta na kumpenda Mungu katika mwili na damu ya ubinadamu.

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Tarehe 6 Januari ya kila mwaka, Mama Kanisa anaadhimisha Siku Kuu ya Tokeo la Bwana, ambapo katika muktadha huo, Baba Mtakatifu Francisko ameongoza Ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Petro, mjini Vatican mbele waamini na mahujaji waliofika katika kusheherekea siku kuu hii. Katika mahubiri yake, Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa Mamajusi walijiweka njia katika safari ya Kumtafuta Mfalme aliyezaliwa. Wao ni sura ya watu katika safari ya kutafuta Mungu, wageni ambao sasa walipelekwa juu ya mlima wa Bwana (Is 56, 6-7), wa mbali ambao sasa wanaweza kusikilia tangazo la wokovu (Is 33, 13) wa wote waliopotea ambao wasikia mwaliko wa sauti rafiki. Kwa sababu sasa, katika nyama yam toto wa Betlhemu, utukufu wa Bwana umejionesha kwa watu wote (Is 40,5) na kima mtu ataona wokovu wa Mungu.”(Lk 3,6).“Ni hija ya kibinadamu ya kila mmoja wetu, kutoka umbali hadi ukaribu.” Mamajusi waliyainua macho yao mbinguni, lakini miguu yao ikitembea katika ardhi, na nyoyo zao ziliinama kwa kusujudu. Papa amesema ngoja arudie tena kusema: macho yao yaliinuliwa mbinguni, miguu yao ikitembea ardhini na nyoyo zao zikiinama kwa kusujudu.”Kwa njia hiyo kwa kwa macho yaliyoinuliwa kuelekea mbinguni. Mamajusi walijawa na hamu ya kile kischo  na mwisho, na kwa hivyo walitazama nyota za anga ya jioni. Hawakupitia maisha yao wakitazama miguuni mwao, wakiwa wamejikunyata, wamefungwa na upeo wa kidunia, wakisonga mbele kwa kujiuzulu au kuomboleza. Wanliinua vichwa vyao juu na kungojea nuru inayoweza kuangazia maana ya maisha yao, wokovu unaopambazuka kutoka juu. Kisha waliona nyota, yenye kung'aa zaidi kuliko nyingine zote, ambayo iliwavutia na kuwafanya waanze safari.

Mahubiri ya Papa 6 Januari 2024
Mahubiri ya Papa 6 Januari 2024

Papa Mtakatifu Francisko amesema  kuwa “Hapa tunaona ufunguo wa kugundua maana halisi ya maisha yetu: ikiwa tutabaki kufungwa katika mipaka finyu ya mambo ya kidunia, tukiharibika, vichwa vimeinamishwa, mateka wa kushindwa kwetu na majuto yetu; ikiwa tuna kiu ya mali na starehe za kidunia - ambazo ziko hapa leo na zimetoweka kesho,  badala ya kuwa watafutaji wa maisha na upendo, maisha yetu polepole yatapoteza nuru yake. Mamajusi, ambao bado ni wageni na bado hawajakutana na Yesu, wanatufundisha kuelekeza macho yetu juu, na kuinua macho yetu mbinguni, na milima ambayo msaada wetu utatoka, kwa maana msaada wetu unatoka kwa Bwana (Zab 121:1-2). Papa amesisitiza kuwa “ tuyainue macho yetu mbinguni! Tunahitaji kuinua macho yetu juu, ili kuweza kuona ukweli kutoka juu. Tunahitaji hili katika safari yetu ya maisha, tunahitaji kujiruhusu kutembea katika urafiki na Bwana, tunahitaji upendo wake ututegemeze, na nuru ya neno lake ituongoze, kama nyota ya usiku. Tunahitaji kuanza safari hii, ili imani yetu isipunguzwe kuwa mkusanyiko wa ibada za kidini au sura ya nje tu, bali iwe moto unaowaka ndani yetu, na kutufanya tuwe watafutaji wa uso wa Bwana kwa shauku na mashahidi wake. Injili.”

Papa amekazi kusema kuwa “ Tunahitaji hili katika Kanisa, ambapo, badala ya kugawanyika katika makundi kulingana na mawazo yetu wenyewe, tunaitwa kumweka Mungu katikati. Tunapaswa kuachana na itikadi za kikanisa ili tuweze kugundua maana ya Mama Kanisa, tabia ya kikanisa. Itikadi za kikanisa, hapana; wito wa kikanisa, ndiyo na  Bwana, na sio mawazo yetu wenyewe au miradi yetu wenyewe, lazima Bwana awe katikati.” Papa ametoa mwaliko  kwamba “ tujiweke kwa  upya kutoka kwa Mungu; tutafute kutoka kwake ujasiri wa kutokata tamaa mbele ya magumu, nguvu ya kushinda vikwazo vyote, furaha ya kuishi katika ushirika wenye maelewano.” “Mamajusi hawakutazama nyota tu, vitu vilivyo juu; - Papa amesema, pia walikuwa na miguu inayotembea juu ya ardhi. Wakaondoka kwenda Yerusalemu na kuuliza, “Yuko wapi Mtoto aliyezaliwa Mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake katika kuchomoza kwake, nasi tumekuja kumsujudia” (Mt 2:2). Jambo moja: miguu yao inahusishwa na kutafakari. Nyota inayong'aa angani huwatuma kusafiri katika njia za ulimwengu.” Wakiinua macho yao juu, walielekezwa kushuka kwenye ulimwengu huu. Wakimtafuta Mungu, wanaelekezwa kumpata ndani ya mwanadamu, ndani ya Mtoto mdogo amelala horini. Kwa maana hapo ndipo Mungu ambaye ni mkuu usio na kikomo amejifunua: katika kidogo sana. Tunahitaji hekima, tunahitaji msaada wa Roho Mtakatifu, ili kuelewa ukuu na udogo wa udhihirisho wa Mungu.”

Misa ya tarehe 6 Januari 2024
Misa ya tarehe 6 Januari 2024

Papa Francisko ameendelea na tafakari hiyo akiwemba tujiruhusu kuendelea kutembea kwenye dunia hii! “Karama ya imani ilitolewa kwetu ili tusiendelee kutazama mbingu (rej. Mdo. 1:11), bali tusafiri katika njia za ulimwengu kama mashahidi wa Injili. Nuru inayoangazia maisha yetu, Bwana Yesu, ilitolewa joto si  kwetu tu  joto  la usiku wetu, bali  kuruhusu miale ya mwanga ipite  katika vivuli vya giza  na  kufunika hali nyingi katika jamii zetu. Tunampata Mungu anayeshuka kututembelea, si kwa kuegemea katika nadharia fulani ya  itakadi za kidini, bali kwa kuanza safari, kutafuta ishara za uwepo wake katika maisha ya kila siku, na zaidi ya yote kwa kukutana na kugusa mwili wa kaka na dada zetu. Kumtafakari Mungu ni kuzuri, lakini kunazaa matunda tu, ikiwa tunajihatarisha, hatari ya huduma ya kumpeleka Mungu kwa wengine. Mamajusi walikwenda kumtafuta Mungu, Mungu mkuu, wakapata mtoto. Hili ni muhimu: kumpata Mungu katika mwili na mifupa, katika nyuso za wale tunaokutana nao kila siku, na hasa katika maskini. Mamajusi wanatufundisha kwamba kukutana na Mungu daima hutufungua kwa ukweli mkuu zaidi, ambao hutufanya kubadili njia yetu ya maisha na kubadilisha ulimwengu wetu. Kwa maneno ya Papa Benedikto wa kumi na sita: “Tumaini la kweli linapokosekana, furaha hutafutwa katika ulevi, katika kupita kiasi, na ujuu juu na tunajiangamiza wenyewe na ulimwengu… kwa hiyo ulikuwa ni ujasiri mkuu wa Mamajusi, waliofunga safari ndefu kufuatia nyota, na waliweza kupiga magoti mbele ya Mtoto na kumpa zawadi zao za thamani” (Mahubiri ya Papa Benedikto XVI, 6 Januari 2008).

Siku Kuu ya Tokeo la Bwana

Hatimaye, Baba Mtakatifu amekazia kusema kuwa “tuzingatie pia kwamba Mamajusi wana nyoyo zilizoinamishwa kwa kuabudu. Wanatazama nyota mbinguni, lakini hawakimbilii ibada ya ulimwengu mwingine; wanatoka, lakini hawatangi-tangi, kama watalii wasio na marudio. Walifika Bethlehemu, na walipomwona mtoto, “wakapiga magoti na kumsujudia” (Mt 2:11). Kisha wakafungua masanduku yao ya hazina na kumtolea dhahabu, ubani na manemane. “Kwa vipaji hivi vya fumbo walijulisha utambulisho wa yule wanayemwabudu. Kwa dhahabu, walitangaza kwamba yeye ni Mfalme; pamoja na ubani, kwamba yeye ni Mungu; Na manemane, kwamba yeye  amekusudiwa kufa.” (Mtakatifu Gregory Mkuu katika Mahubiri ya X, 6).  Baba Mtakatifu amebainisha kuwa “Mfalme aliyekuja kututumikia, Mungu aliyefanyika mwanadamu. Kabla ya fumbo hili, tunaitwa kuinama mioyo yetu na kupiga magoti katika kuabudu: kumwabudu Mungu anayekuja katika udogo, anayekaa katika nyumba zetu, ambaye anakufa kwa ajili ya upendo. Mungu ambaye, “ingawa alidhihirishwa na ukuu wa mbingu na ishara za nyota, alichagua kupatikana… chini ya dari ndogo.

Misa tarehe 6 Januari 2024
Misa tarehe 6 Januari 2024

Katika mwili dhaifu wa mtoto mchanga, aliyevikwa nguo za kitoto, aliabudiwa na Mamajusi na kusababisha hofu kwa waovu” (MTAKATIFU AUGUSTINE, Mahubiri. 200).) Ndugu, tumepoteza tabia ya kuabudu, tumepoteza uwezo unaotupatia kuabudu. Kwa hiyo tugundue tena ladha yetu ya sala ya kuabudu. Hebu tumtambue Yesu kama Mungu na Bwana wetu, na kumwabudu. Leo Mamajusi wanatualika kuabudu. Siku hizi kuna ukosefu wa kuabudu kati yetu.” Kwa hiyo Papa amesema kuwa “ kama Mamajusi, tuyainue macho yetu mbinguni, tuanze kumtafuta Bwana, tuinamishe mioyo yetu kwa kuabudu. Kuangalia mbinguni, kuweka safari na kuabudu. Na tuombe neema ili tusipoteze ujasiri: ujasiri wa kuwa watafutaji wa Mungu, wanaume na wanawake wa matumaini, waotaji ndoto wasio na ujasiri wanaotazama mbinguni, ujasiri wa uvumilivu katika kusafiri kwenye barabara za ulimwengu huu kwa uchovu wa ulimwengu. safari ya kweli, na ujasiri wa kuabudu, ujasiri wa kumtazama Bwana ambaye huangaza kila mwanamume na mwanamke. Bwana atujalie neema hii, kuliko neema yote ya kujua kuabudu.”

Watawa wa ndani Wabenedikti waliofika katika Nyumba ya Mater Ecclesiae
Watawa wa ndani Wabenedikti waliofika katika Nyumba ya Mater Ecclesiae

Papa amesalimia watawa wa ndani wa Argentina

Dakika chache baada ya kuhitimisha Misa Takatifu, taarifa kutoka vyombo vya habari Vatican imbanishwa kuwa kabla ya Maadhimisho ya Misa Takatifu, baba Mtakatifu alisalimia kikundi cha wamonaki wa Kibenedikini kutoka nchini Argentina ambao wamefika hivi karibuni kuishi katika Monosteri ya Mater Ecclesiae.

06 January 2024, 11:00