Makambi ya wakimbizi huko Gaza. Makambi ya wakimbizi huko Gaza.  (AFP or licensors)

Papa:vita ni uhalifu dhidi ya ubinadamu,tuelimishe kwa ajili ya amani

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana,Papa kwa mara nyingine tena alizindua wito wake dhidi ya migogoro,hasa nchini Ukraine,Palestina na Israel:"vita vinapanda kifo kati ya raia na kuharibu miji na miundombinu."Papa amemnukuu Padre Ibrahim Faltas,wa Nchi Takatifu:'amani lazima ielimishwe na pia kuwageukia wale walio na mamlaka kutafakari kwamba vita si njia ya kuleta suluhisho.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, mara baada ya Tafakari na Sala ya Malaika wa Bwana kwa Mahujaji na waamini waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, Dominika tarehe 14 Januari 2024 amesema: “Ninatoa salamu zangu kwenu ninyi nyote, Warumi na mahujaji wanaotoka Italia na kutoka sehemu nyingi za dunia. Hasa ninawasalimu washiriki wa Ndugu wa Sakramenti ya Mama Yetu wa  Villarrasa (Hispania). Tusisahau kuwaombea wahanga wa maporomoko ya ardhi yaliyotokea nchini Colombia, ambayo yalisababisha wahanga wengi.”

Papa Francisko ametoa wito kwa wahusika kusiitiza vita kila eneo lenye migogoro duniani
Papa Francisko ametoa wito kwa wahusika kusiitiza vita kila eneo lenye migogoro duniani

Baba Mtakatifu akiendelea aidha alisema: “Na tusiwasahau wale wanaokabiliwa na ukatili wa vita katika sehemu nyingi za dunia, hasa Ukraine, Palestina na Israel. Mwanzoni mwa mwaka tulitakiana matashi mema ya amani, lakini silaha ziliendelea kuua na kuharibu. Tunaomba wale walio na mamlaka juu ya migogoro hii watafakari ukweli kwamba vita sio njia ya kutatua, kwa sababu inapanda vifo kati ya raia na kuharibu miji na miundombinu.”

Pamoja na hali kuwa mbaya ya baridi, waamini walikuja kwa wingi kwenye sala
Pamoja na hali kuwa mbaya ya baridi, waamini walikuja kwa wingi kwenye sala

“Kwa maneno mengine, leo vita yenyewe ni uhalifu dhidi ya ubinadamu. Tusisahau hilo kwamba: vita yenyewe ni uhalifu dhidi ya ubinadamu. Wananchi wanahitaji amani! Dunia inahitaji amani! Dakika chache zilizopita, katika kipindi cha A Sua Immagine yaani "Katika Picha Yake", nilimsikia Padre Faltas, Padre  Msimamizi wa Nchi  akatifu huko Yerusalemu, alizungumza juu ya kuelimisha amani. Ni lazima tuelimishe juu ya amani.” Tunaona kuwa bado hatujawa na elimu ya kutosha-ubinadamu wote-kukomesha kila vita. Tuombe daima neema hii: kuelimisha amani.Ninawatakia Dominika njema. Tafadhali Msisahau kuniombea. Mlo Mwema mchanana kwaheri ya kuonana!" Papa Francisko amehitimisha.

Papa ametoa wito kwa wahusika wa vita kukomesha. maana vinaleta vifo na uharibifu tu
14 January 2024, 13:06