Tafuta

Papa Francisko: Tuabudu Kama Mamajusi Ili Kuboresha Maisha Yetu

Katika tafakari kabla ya sala ya Malaika wa Bwana inayohusu maadhimisho ya Tokeo la Bwana, Papa amesisitizia umuhimu wa kupata muda wa kuwaangalia watoto, kama Mamajusi walivyomtazama Yesu:watoto wadogo ambao pia wanazungumza nasi juu ya Yesu,kwa imani yao,upesi wao,mshangao wao,udadisi wao wa afya,uwezo wao wa kulia na kucheka kwa hiarina kuota.Mungu alijifanya hivyo:Mtoto,mwaminifu,rahisi,mpenda maisha.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, mara baada ya Misa Takatifu, aliyoingoza katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, mjini Vatican ameendelea na tafakari nyingine kabla ya sala ya Malaika wa Bwana,  Jumamosi tarehe 6 Januari 2024 kwa mahujaji na waamini waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, kuadhimisha Siku Kuu ya Epifania yaani Tokeo la Bwana. Baba Mtakatifu akianza tafakari hiyo amesema: “Leo tunaadhimisha Epifania ya Bwana, yaani maenonesho ya Mamajusi kwa watu wote (Mt 2, 1-12). Wao walikuwa ni watafiti wenye hekima ambao baada ya kujiuliza juu ya nyota iliyokuwa imejitokeza, walianza safari na kufika Bethlehemu. Hapo walikumta Yes una “Mama yake, ambapo walimwambudu na kumtolea “dhahabu, uvumba na manemane (Mt 2,11). Wenye hekima waliotambua uwepo wa Mungu kwa urahisi wa mtoto: sio mfalme au mtu maarufu, lakini mtoto maskini wa Watu, na walimsujudia mbele yake na kumwabudu. Nyota iliwaongoza huko, mbele ya Mtoto; na wao, kwa macho yake madogo na yasiyo na hatia, walipokea nuru ya Muumba wa Ulimwengu, ambaye wamejikita kwa ajili ya utafutaji wa uwepo wake.

Sala ya Malaika wa Bwana
Sala ya Malaika wa Bwana

Ni uzoefu wa kuamua kwao na muhimu kwetu pia: katika Mtoto Yesu, kiukweli, tunaona Mungu aliumba mwanadamu. Na kisha tumtazame, tustaajabie unyenyekevu wake. Kumtafakari Yesu, kubaki mbele zake, kumwabudu katika Ekaristi: si kupoteza muda, lakini ni kutoa maana ya muda. “Papa ameomba warudie neno hilo kwamba kuabudu sio kupoteza muda. Hiyo ni muhimu kwamba sio kupoteza bali ni kutoa maana ya muda.” Papa ameongeza kusema “Ni kutafuta njia ya uzima tena katika urahisi wa ukimya unaorutubisha moyo. Na pia tunapata wakati wa kuwaangalia watoto, kama Mamajusi walivyomtazama Yesu: watoto wadogo ambao pia wanazungumza nasi juu ya Yesu, kwa imani yao, upesi wao, mshangao wao, udadisi wao wa afya, uwezo wao wa kulia na kucheka kwa hiarina  kuota. Mungu alijifanya hivyo: Mtoto, mwaminifu, rahisi, mpenda maisha (rej. Hek 11:26).

Siku ya Utoto Mtakatifu wa Kimisionari
Siku ya Utoto Mtakatifu wa Kimisionari

Ikiwa tutajua kukaa mbele ya Mtoto Yesu na katika kuwasindikiza watoto, tutajifunza kushangaa na tutaanzia hapo zaidi utashi na kuboreka kama Mamajusi. Na tutajua jinsi ya kuwa na mitazamo mipya na  mitazamo bunifu mbele ya matatizo ya ulimwengu. Baba Mtakatifu kwa hiyo amesema tujiulize: katika siku hizi tumeacha kuabudu, je tumemtengenezea Yesu nafasi kwa ukimya, tukiomba mbele ya pango la kuzaliwa kwake? Je, tumejitolea kutoa nafasi kwa watoto, kuzungumza na kucheza nao? Na hatimaye, je, tunaweza kuona matatizo ya ulimwengu kupitia macho ya watoto? Maria, Mama wa Mungu na wetu, atuzidishie upendo wetu Mtoto Yesu na kwa watoto wote, hasa wale waliojaribiwa kwa vita na dhuluma.

Mamajusi
Mamajusi
06 January 2024, 15:54