Papa Francisko:Kuongezeka kwa vita kuna tishia na watoto hawana tabasamu
Salvatore Cernuzio na Angella Rwezaula - Vatican
Katika baadhi ya mada zilizoakisiwa na Papa Francisko katika mahojiano ya kipindi cha Italia kiitwacho: “Che tempo che fa,” kwenye Televisheni kilichotangazwa tarehe 14 Januari 2024 usiku kinachoendeshwa na Fabio Fazio ni pamoja: Baraka kwa wote, miungano ya watu “wasio wa kawaida”, kama Mungu ambaye “hubariki wote, wote, wote”; “hofu” ya kuongezeka kwa vita na uhalifu wa vita ambao umeiba tabasamu za watoto; uthibitisho kwamba hana nia ya kujiuzulu katika kiti cha upapa na tangazo la safari mbili ya kwenda Polynesia, mwezi Agosti na Argentina yake, mwishoni mwa mwaka.
Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko alijibu swali kuhusu hati ya Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa ya ‘Fiducia Supplicans’, ambayo ilifungua uwezekano wa kuwabariki watu wawili “wasio katika hali ya kawaida,” ikiwa ni pamoja na wapenzi wa jinsia moja na ambao wameibua hisia tofauti. Papa alithibitisha tena kwamba: “Bwana hubariki wote, wote, wote”; kwa mapendekezo yake alisema: “sisi lazima tuwashike mikono watu hawa na tusiwahukumu tangu mwanzo.”
Hii “ni kazi ya kichungaji ya Kanisa na ni kazi muhimu kwa waungamishi walioitwa kusamehe kila kitu.” Yeye mwenyewe, alifunua, kuwa katika miaka 54 ya ukuhani mara moja tu alikataa kutoa msamaha, “kutokana na unafiki wa mtu.” Bwana"hadharau dhambi zetu, kwa sababu yeye ni baba, na anatusindikiza, alisema Papa Francisko, huku akiamini kwamba anapenda kutumaini kwamba kuzimu kuwe kutupu."
Kama katika miezi hii ya migogoro ya Mashariki ya Kati na katika miaka hii ya uchokozi dhidi ya Ukraine, Papa Francisko alirudi kuelezea juu ya hofu ya vita: “Ni kweli kwamba ni hatari kufanya amani, lakini pia vita ni hatari zaidi,” alisema. Na alizungumzia mkutano aliokuwa nao Jumatano tarehe 10 Januari 2024 iliyopita na ujumbe wa watoto kutoka Ukraine kwamba: “Hakuna hata mmoja wao aliyekuwa akitabasamu. Watoto hutabasamu moja kwa moja, niliwapatia chokoleti na hawakutabasamu. Walikuwa wamesahau tabasamu lao na kwa mtoto kusahau tabasamu lake ni uhalifu. Hii inaleta vita: inakuzuia kuota.”
“Nyuma ya vita”, alisisitiza Askofu wa Roma, “kuna biashara ya silaha.” Alieleza hofu yake ya kibinafsi ya kuongezeka kwa mzozo huo: “Kuongezeka huku kwa vita kunaniogopesha, kwa sababu hatua hii ya kusonga mbele kwa vita ulimwenguni humfanya mtu ajiulize jinsi tutakavyoishia. Na silaha za atomiki sasa, na kuharibu kila kitu. Tutamaliza vipi. Kama Safina ya Nuhu? Hii inanitisha. Uwezo wa kujiangamiza ambao ubinadamu unao leo hii.”
Nafasi katika mahojiano pia ilijikita katika mada ya wahamiaji, kwa kumbukumbu ya kukumbatiwa kwa Pato, kijana wa Cameroon ambaye alipoteza mkewe na binti yake jangwani kati ya Tunisia na Libya. Papa Francisko alikutana naye mnamo Novemba huko Mtakatifu Marta. “Kuna ukatili mwingi katika kuwatendea wahamiaji hawa wanapoondoka nyumbani kwao na kufika hapa Ulaya,” alisema, huku akisisitiza kwamba “kila mtu ana haki ya kukaa nyumbani kwake na kuhama.” Mwaliko wa Papa Francisko ni wa sera ya uhamiaji “iliyofikiriwa vizuri” ambayo inasaidia “kuchukua mikononi mwetu shida ya wahamiaji” na “kuondoa mafia wote wanaowanyonya wahamiaji.”
Katika mahojiano na maswali kulikuwa na swali kuhusu uwezekano wa kuacha upapa, lakini yeye alijibu kuwa: “Si wazo wala wasiwasi wala hata shauku. Ni jambo linalowezekana, lililo wazi kwa Mapapa wote, lakini kwa sasa haliko katikati ya mawazo yangu na wasiwasi wangu, wa hisia zangu.” Ili kuthibitisha maneno hayo, Papa Francisko alitangaza safari mbili: Polynesia na Argentina. “Ni wakati mgumu kwa nchi. Uwezekano kufanya safari katika nusu ya pili ya mwaka unapangwa, kwa sababu sasa kuna mabadiliko ya serikali, kuna mambo mapya ... ninataka kwenda. Miaka kumi ni sawa, ni sawa, ninaweza kwenda.”