Tafuta

Conventi Takatifu na Kanisa  la Mtakatifu Francis wa Assisi Conventi Takatifu na Kanisa la Mtakatifu Francis wa Assisi 

Papa katika jarida la Mtakatifu Francis:'madaraja ya amani kwa ulimwengu ulio katika vita'

Baba Mtakatifu ametoa mahojiano katika jarida la kila mwezi la Wafranciskani wa Konventi Takatifu ya Assisi na kuwaalika kuwa "mitume wa upatanisho na msamaha katika ulimwengu ambao haujaacha kupigana kila mahali.Bwana hachoki kusamehe,Mtakatifu Francis alikuwa na moyo mkuu na yeye pia hakuchoka kutoa msamaha."

Vatican News.

“Kuna ukatili mwingi, ndiyo maana ninaomba kwa ajili ya madaraja ya amani!” Alisema hayo  Baba Mtakatifu  Francisko katika mahojiano yaliyotolewa kwenye jarida la kila mwezi la ‘San Francesco Patrono d'Italia’ yaani (Mtakatifu Francis, Msimamizi wa Italia), linalochapishwa na mapadre wa Konventi Takatifu ya Waconventuali wa  Assisi. Katika toleo la mwezi Januari 2024, kwa hiyo  Papa kwa mara nyingine tena aliomba "tuwe vyombo vya amani katika kujenga madaraja na kufungulia mikono yetu kwa kaka na dada zetu wenye mahitaji." Kwa mijubu wake "Tangu mwisho wa Vita vya Kidunia vya pili, alibainisha, kuwa - ulimwengu haujaacha kufanya vita kila mahali: tunaona Palestina na Ukraine vizuri kwa sababu wako karibu na sisi. Baba Mtakatifu pia aliongeza kusema kwamba "nyakati tunazoishi ni tete na kwamba kuna watu wengi wamefungwa kwa sababu za kisiasa". "Tunapokabiliwa na ukatili kama huo, tunahitaji kujenga madaraja. ‘Jenga madaraja’" Papa alisisitiza.

Katika mahojiano yaliyofanyika tarehe 29 Desemba 2023, baada ya kukutana na Mkuu wa Wafransiskani Waconventuali, Ndugu Carlos Trovarelli; Ndugu Marco Moroni; na Mkurugenzi wa Ofisi ya Mawasiliano ya Konventi Takatifu, Ndugu Giulio Cesareo, (OFMConv), Papa Francisko aliulizwa  swali kuwa ‘Mtakatifu Francis’ ni nani kwake’, ambapo swali hilo alijibu akisema kwamba "yeye ni mtakatifu maalum, ambaye aliiga Kristo kwa namna ya pekee". Yeye ni mtakatifu wa unyenyekevu na wema", alieleza Papa; "ni mvumilivu na haombi chochote kwa yeyote huku akijitoa kikamilifu kwa kila mtu." Kwa kuongeza: "Hii ni jinsi  gani Mtakatifu Francis alichagua kumwiga Bwana na alifanya hivyo hadi mwisho.” Papa alielezea.

Hatimaye Baba Mtakatifu aliweza kuakisi hata zawadi ambayo Roho Mtakatifu anataka kulipatia Kanisa kwa njia ya Wafranciskani ile ya wema. Papa Francisko alieleza kuwa wema maana yake ni ushuhuda na msamaha. “Mfransiskani lazima awe mkarimu sana katika sakramenti ya upatanisho, kusamehe kila kitu”, alisisitiza Papa. Kwa kuongeza kwamba: “Bwana hachoki kusamehe na kwamba Mtakatifu Francis alikuwa na moyo mkubwa na yeye pia hakuchoka kutoa msamaha.” Anachotarajia kutoka kwa Wafransiskani ni kwamba: “wawe mitume wa upatanisho na msamaha.” Alihitimisha Papa.

Mahojiano ya Papa na Ndugu Waconventuali Takatifu
05 January 2024, 11:14