Papa:katika vita kuna ukatili,kilio cha wahanga kiinue mipango ya amani
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kilio chao cha uchungu na kiguse mioyo ya viongozi wa Mataifa". Kisha Papa alishutumu ukatili wa migogoro kwamba: "Tunaomba amani kutoka kwa Bwana ambaye daima ni mpole, asiye na ukatili” Hakuna wakati, hakuna nafasi, lakini ni msururu mrefu wa damu na maumivu tu unaounganisha zama mbili: ile ya vita vya dunia na ile ya sasa ya migogoro ya kipande kidogo inayosambaratisha ubinadamu. Baba Mtakatifu Francisko aliinya sala zake kwa wale waliouawa vitani leo na jana, mwishoni mwa Katekesi yake Ukumbi wa Paul VI, Jumatano tarehe 31 Januari 2024 wakati wa salamu kwa lugha Kiitaliano na kukumbusha Siku ya Kitaifa ya Wahanga wa Kiraia.
Kila tare 1 Januari ni kumbukumbu ya wahanga wa vita
Hii ni siku ambayo uadhimishwa nchini Italia kila tarehe 1 Februari ya kila mwaka. Ni siku iliyoanzishwa kwa sheria ya tarehe 25 Januari 2017 katika ibara ya 9 ambayo tunataka kuhifadhi kumbukumbu ya mizozo ya zamani na kuteka fikira kwenye mchezo wa kuigiza unaowapata raia ulimwenguni kote waliohusika katika mizozo ya kivita: Vifo elfu 33 mwaka jana katika viwanja vya mapambano 31 vya vita zinazoendelea hivi sasa ulimwenguni. “Idadi ya juu zaidi kwa miaka kumi na tatu sasa. Katika kumbukumbu ya maombi ya wale waliokufa katika migogoro miwili ya dunia, pia tunashirikisha kuwambumbuka wengi sana, raia, waathiriwa wasio na ulinzi wa vita ambavyo kwa bahati mbaya bado vinavuja damu kwenye sayari yetu, kama inavyotokea Mashariki ya Kati na Ukraine.”
Tuombe amani kwa Mungu ambaye si mkatili bali mpole
Habari zinazowasili saa hizi kutoka maeneo mawili ya vita yaliyotajwa na Papa Francisko ni ya kushangaza: zaidi ya raia kumi walikufa wakati wa kulipuliwa kwa nyumba huko Deir al-Balah, katikati mwa Ukanda wa Gaza; mashambulizi ya ndege zisizo na rubani, nyumba kuharibiwa, raia kujeruhiwa na kuuawa, huko Karkhiv, Bakhmut na maeneo mengine ya Ukraine. Baba Mtakatifu alisema, Kilio cha uchungu cha watu hawa, "kinaweza kugusa mioyo ya viongozi wa Mataifa na kuhamasisha mipango ya amani". Kwa hivyo, maneno kadhaa ya nje: uchunguzi mkali wa mipaka ya unyama ambayo vita hubomoa kwa utaratibu. Ukisoma historia za siku hizi, vitani kuna ukatili mwingi sana... Tumwombe Mungu amani ambayo siku zote ni ya upole, si ya kikatili.
Kumbukumbu ya Don Bosco
Akiwasalimia waamini kwa lugha ya Kiarabu, Papa amekumbuka tarehe 31 Januari kumbukumbu ya kiliturujia ya Don Bosco, Padre mwanzilishi wa Wasalesiani, kielelezo cha elimu, matunzo na makaribisho ya vijana: Leo, kwa kumbukumbu ya Mtakatifu Yohane Bosco, aliwatunza sana vijana, nawaalika muige yeye, kuwaelimisha vijana katika imani na kuwazoeza katika sayansi na taaluma mbalimbali, kwa mustakabali mwema, ambamo wanadamu wanaweza kufurahia amani, udugu na utulivu.