2024.01.29 Papa amekutana na wakuu na wafanyakazi wa TV2000 na wa "Radio in Blu." 2024.01.29 Papa amekutana na wakuu na wafanyakazi wa TV2000 na wa "Radio in Blu."  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa kwa TV2000 na Radio In blu:Ukaribu,moyo na uwajibu katika kazi ya mwandishi

Ukaribu,moyo na wajibu,ndiyo mambo matatu aliyofafanua Papa Francisko akikutana na wakuu na wafanyakazi wa TV2000 na Radio inblu,Jumatatu 29 Januari 2024 mjini Vatican.Kama waandishi amekumbusha kwenda kinyume na mawazo ya ulimwengu:“Sio kwa ukubwa wa matendo yetu kuwa tunampendeza Mungu,lakini ni upendo tunaofanya nao.”

Na Angella Rwezaula- Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu tarehe 29 januari 2024 amekutana na Wakuu na wafanyakazi wa Vyombo vya habari vya Habari vya Kanisa la Italia. Baba Mtakatifu amesema “Nina furaha kuwakaribisha kwenye hafla ya kumbukumbu ya miaka 25 ya kuzaliwa kwa TV2000 na mzunguko wa inBlu2000. Papa amemsalilia Askofu Giuseppe Baturi, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Italia, (CEI) na Monsinyo Piero Coccia, Rais wa Mfuko wa Mawasiliano na Utamaduni na wa “Rete Blu”, na kwa wote wanaofanya kazi katika vyombo hivi vya habari. Miaka kumi imepita tangu mkutano wao uliopita na mengi yamebadilika katika mazingira ya vyombo vya habari. Ubunifu wa kiteknolojia umebadilisha mbinu za uzalishaji wa maudhui, pamoja na matumizi yao; na sasa akili mnemba pia inabadilisha kwa kiasi kikubwa habari na mawasiliano na, kupitia kwao, baadhi ya misingi ya kuishi pamoja kiraia.(Ujumbe wa LVIII wa Siku ya Mawasiliano kijamii).

Papa amekutana na wakuu na wafanyakazi wa TV2000 na Radio In blu
Papa amekutana na wakuu na wafanyakazi wa TV2000 na Radio In blu

Katika hali hii, ambayo inaonekana kuwavuta sio tu waendeshaji katika sekta hii bali sisi sote, hata hivyo kuna baadhi ya kanuni ambazo hazibadiliki, kama vile nyota za kutazama ili kujielekeza na kutopoteza njia yetu. Na hii inahusu hasa wao ambao , pamoja na gazeti ‘Avvenire’ na Shirika la Sir,  vyote vinamilikuwa na Baraza la Maaskofu Italia. Hiki si kikomo, hakika ni kielelezo cha uhuru mkubwa, kwa sababu kinatukumbusha kwamba mawasiliano na habari huwa na mizizi yake kwa binadamu. Na, tena, inasisitiza umuhimu wa kumwilisha imani katika utamaduni, hasa kwa njia ya ushuhuda, kusimulia historia ambazo giza linalotuzunguka halizimi nuru ya matumaini. Ni muhimu kukumbuka na kuishi mali hii. Kwa sababu hiyo Baba Mtakatifu amependa kuakisi maneno matatu ili waendelee kwenye njia ya kazi yao.

Awali ya yote ni ukaribu, yaani kuwa karibu. Kila siku - kupitia televisheni au radio -wanakuwa karibu na watu wengi, ambao hupata ndani yao marafiki ambao wanaweza kupokea habari kutoka kwao, ambao wanaweza kutumia wakati mzuri nao, au kugundua ukweli mpya, uzoefu na maeneo. Na ukaribu huu pia unaenea hadi kwenye maeneo na vitongoji wanakoishi watu.  Papa ameongeza kusema: “Ninapenda kufikiri kwamba ukaribu ni mojawapo ya sifa za Mungu ambaye alikuja kuwa karibu nasi. Kuna mambo matatu yanayotufanya tumwone Mungu: ukaribu, na wengine; huruma, kwani  Mungu ni mpole - na  mwenye huruma. Kusamehe kila wakati.  Wasisahau: ukaribu, huruma na upole.” Baba Mtakatifu Francisko amewahimiza kuendelea kuunda mitandao, kusuka mitandao, kueleza uzuri na wema wa jamii zetu - kwa ukaribu -, kuwafanya wahusika wakuu ambao kwa kawaida huishia kuwa nyongeza au hata kutozingatiwa. Mawasiliano  kama tujuavyo yako katika hatari ya kuanguka chini kwa mantiki fulani kuu,  hasa ya kuingia kwenye mamlaka au hata kuunda habari za uwongo. Papa ametoa onyo kuwa wasiingie kwenye kishawishi cha  kuanguka kwenye mtego huo na hivyo waende  kinyume na mtiririko,  na daima wakivaa nyayo za viatu vyao na kukutana na watu. Ni kwa njia hiyo tu wanaweza kuwa watu halisi kwa wito, kama moja ya kauli mbiu yao ya zamani inavyosema. Na wasisahau kamwe wale walio pembezoni, watu masikini, watu wapweke na, mbaya zaidi, watu waliotupwa.

Papa amekutana na wakuu na wafanyakazi wa TV2000 na Radio in blu
Papa amekutana na wakuu na wafanyakazi wa TV2000 na Radio in blu

Neno la kwanza lilikuwa ukaribu, la pili ambapo Papa Francisko ameachia   ni moyo, katika umuhimu wa maana yake ya kibiblia na mapokeo ya Kikristo. Katika miaka ya hivi karibuni Papa Francisko umezipatia mara nyingi Jumbe za Siku ya Mawasiliano Duniani. “Inaweza kuonekana kuwa haifai kuweka moyo wao katika ulimwengu wa kiteknolojia, kama ulimwengu wa sasa wa mawasiliano, lakini kila kitu huanza kutoka hapo. Huwezi kuchunguza ukweli, huwezi kumhoji mtu, huwezi kusema kitu isipokuwa kutoka moyoni. Kiukweli, kuwasiliana hakusababishi upitishaji wa nadharia au utekelezaji wa mbinu, lakini ni sanaa ambayo katikati yake ina uwezo wa moyo ambao hufanya ukaribu uwezekane” (rej. Evangelii gaudium, 171).

Hii inatuwezesha kutengeneza nafasi kwa ajili ya nyingine - kupunguza ile ya ubinafsi kidogo na  kujikomboa kutoka katika minyororo ya ubaguzi, kusema ukweli bila kuutenganisha na upendo. Kamwe tusitenganishe ukweli na moyo! Na kisha, kuwa na ujasiri. Sio kwa bahati mbaya kwamba ‘ujasiri’ hupata kutoka katika moyo. Wale walio na moyo pia wana ujasiri wa kuwa mbadala, bila hata hivyo kuwa na mabishano au fujo; kuaminika, bila kudai kulazimisha maoni ya mtu; kuwa wajenzi wa daraja. “Na hii ni muhimu sana. Mwasilianaji,  anaweza kujifikiria kama daraja, kwa sababu mwasilianaji lazima awe mjenzi wa daraja.

Papa akizungumza na wakuu wa TV2000 na wafanyakazi wa Radio in Blu
Papa akizungumza na wakuu wa TV2000 na wafanyakazi wa Radio in Blu

Na neno la tatu ni wajibu.  Baba Mtakatifu amefafanua kuwa “Kila mtu lazima afanye sehemu yake ili kuhakikisha kwamba kila aina ya mawasiliano ni lengo, heshima ya utu wa binadamu na makini kwa manufaa ya wote. Kwa njia hiyo, tutaweza kurekebisha mipasuko, kubadilisha kutojali katika kukubalika na uhusiano. Wao ni mojawapo ya taaluma ambazo zina tabia ya wito: wameitwa kuwa wajumbe wanaojulisha kwa heshima, kwa umahiri, kupinga migawanyiko na mifarakano. Na kila wakati kukumbuka kuwa katikati ya kila huduma, katikati ya kila kifungu, katikati ya kila programu kuna mtu.” Papa amekazia kusema kuwa “Msisahau hii. Ndiyo hasa inayotoa maana ya mawasiliano.”

Baba Mtakatifu akiendelea amesema “miaka kumi iliyopita mlianza awamu ya kufikiria upya na kupanga upya kazi zenu; katika siku za hivi karibuni mmeongeza kipande zaidi na uzinduzi wa ‘Programu yenu. Ninaomba pia ichangie katika kuwasiliana kwa ukaribu, moyo na uwajibikaji. Kusonga mbele kwenye njia hii, wakikumbuka kile ambacho Mlinzi wao Mtakatifu Francis de Sales alisema kuwa: “Sio kwa ukubwa wa matendo yetu kwamba tunampendeza Mungu, lakini kwa upendo ambao tunafanya” (Ushauri wa Kiroho). Katika hilo Papa Francisko amekazia na kuwabariki kutoka ndani ya moyo wake na kuwaomba tafadhali wasali kwa ajili yake na kuhitimisha.

Hotuba ya Papa kwa wakuu na wafanyakazi wa TV2000 na wa Radio in Blu
29 January 2024, 14:57