2024.01.19 Papa akutana na Wawakilishi wa Kiekumeni wa Finland. 2024.01.19 Papa akutana na Wawakilishi wa Kiekumeni wa Finland.  (Vatican Media)

Papa na wawakilishi wa kiekumene wa Finland:kukuza umoja wa kikristo

Kama washiriki wa jumuiya ya wabatizwa,tuko kwenye safari na lengo letu la pamoja ni Yesu Kristo.Na lengo hili haliko mbali,haliwezi kutofikiwa kwa sababu Mungu wetu alikuja kukutana nasi kwa huruma zake,akawa karibu katika Umwilisho na yeye mwenyewe.Ni katika Hotuba ya Papa alipokutana na Wawakilishi wa Kiekumene kutoka Finland.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican na wawakilishi wa kiekumene kutoka Finland,Ijumaa tarehe 19 Januari 2024 ambapo katika hotuba yake amewakaribisha wote na kuanza na kifungu cha Mtakatifu Paulo kwa Warumi kisemacho : “Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo” (Rm 1:7). Nina furaha kwamba mwaka huu pia wamekuja Roma kama mahujaji kusherehekea sikukuu ya Mtakatifu Henry pamoja, katika mfumo wa kiekumene uliojaribiwa sasa. “Nawasalimu hasa wale ambao wanashiriki katika hija hii kwa mara ya kwanza; na wakati kwa mara ya kwanza amemkaribisha, Mpendwa Raimo, kama Askofu mpy Katoliki wa Helsinki: Bwana aibariki huduma yako!”

Akimwelekea Askofu Åstrand, Papa amemkushukuru sana kwa tafakari ambazo wanashiriki vizuri kila wakati, zenye marejeo ya ushuhuda wa watakatifu na katika roho ya kiekumene. Na pia amemshukuru kwa zawadi, ambazo zimefikiriwa vizuri sana. Papa alivutiwa na tafakari yake juu ya thamani ya safari na juu ya Kanisa la Hija. Kama “washiriki wa jumuiya ya wabatizwa, tuko kwenye safari na lengo letu la pamoja ni Yesu Kristo. Na lengo hili haliko mbali, haliwezi kutofikiwa, kwa sababu Mungu wetu alikuja kukutana nasi kwa huruma zake, akawa karibu katika Umwilisho na yeye mwenyewe akatengeneza Njia, ili tutembee kwa usalama, katikati ya njia panda na kwa dalili za uwongo za ulimwengu wa uwongo mara nyingi.”

Papa na kikundi kutoka Finland
Papa na kikundi kutoka Finland

Watakatifu ni kaka  na dada ambao wamesafiri barabara hii hadi mwisho na kufikia lengo lao. Wanatusindikiza kama mashahidi walio hai wa Kristo Njia, Kweli na Uzima wetu. Wanatutia moyo kubaki kwenye njia ya ufuasi hata tunapohangaika, na tunapoanguka. Kama taa zinazowashwa na Mungu, zinaangaza mbele yetu ili zisitufanye tupoteze lengo. “Tumaini kwa neema ya Mungu! - wanatuambia  kuwa  Anawapenda ninyi na anawaita ninyi pia kuwa watakatifu,” (rej.Rm 1:7). Baba Mtakatifu aidha alisema “Niliposikia ukizungumza na kusikia juu ya ukweli wako, nilimshukuru Mungu, kwa sababu kulikuwa na wakati ambapo ibada ya watakatifu ilionekana kugawanyika badala ya kuunganisha waamini wa Kikatoliki na Waorthodox, kwa upande mmoja, na waamini wa kiinjili, kwa upande mwingine. Lakini hii haipaswi kuwa hivyo na, kiukweli, haijawahi kuwa katika imani ya watu watakatifu, waaminifu wa Mungu.

BabaMtakatifu amesema katika Liturujia ya Ekaristi tunasali hivi, tukimwambia Baba wa mbinguni: “Wingi wa watakatifu wanatangaza ukuu wako; ili katika kutawazwa kwa wema wao ukaitie taji kazi ya neema yako” (Dibaji ya Watakatifu I). Na zaidi ya hayo, Katika ungamo la Agostino, katika kifungu cha 21, kinasema kwamba: “watakatifu lazima wakumbukwe, ili kuimarisha imani yetu, tunapoona jinsi walivyopokea neema na jinsi walivyosaidiwa kwa imani; na kuwa kielelezo katika matendo yao mema. Baba Mtakatifu Francisko amewaeleza wote kuwa wameekumbuka baadhi ya Watakatifu wakuu wa Kaskazini: Brigida, Enric na Olav. Hii inatufanya tufikirie kile ambacho Papa Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili aliandika katika Wosia wake wa:  Ut unum sint yaani ili wote wawe na umoja Papa akinukuu amesema: “Ningependa kukumbuka mkutano wa maombi ambao uliniunganisha, katika Basilica ya Mtakatifu Petro yenyewe, kwa sherehe ya Masifu ya jioni na Maaskofu wakuu wa Kilutheri, wa  Sweden na Finland, katika maadhimisho ya miaka mia moja ya kutawazwa kwa Mtakatifu Bridget. […].

Papa na wawakilishi kutona Finland
Papa na wawakilishi kutona Finland

 

Huu ni mfano, kwa sababu ufahamu wa wajibu wa kuombea umoja umekuwa sehemu muhimu ya maisha ya Kanisa” (n. 25). Ikiwa kumbukumbu ya miaka elfu moja ya kifo cha Mtakatifu Olav, mnamo 2030, inaweza kutia moyo na kuhamaisha sala yetu ya umoja, na pia safari yetu ya pamoja, hii itakuwa zawadi kwa harakati nzima ya kiekumene.” Papa Francisko kwa njia hiyo amewashukuru, kwa sababu  ya mkutano hu ona wao  ni ishara hai katika muktadha wa  Juma la  Kuombea Umoja wa Wakristo lililoanza tarehe 18 januari 2024.  Kwa hiyo amehimiza “tuhakikishe kwamba uteuzi huu wa kiekumene haupunguzwi na utimizo na kwamba haujielekezi mwenyewe: kwamba daima una damu ya uzima wa Roho Mtakatifu na kwamba uko wazi kwa ajili ya kuwakaribisha ndugu walio maskini zaidi na waliosahauliwa zaidi, na pia wale walio maskini zaidi, wanaojisikia kuachwa na Mungu, ambao wamepoteza njia ya imani na matumaini. Na kwa kuhitimisha, papa Francisko aliwakaribisa kusali kwa Pamoja sala ya Bwana mmoja. Na hivuo aliomba kila mmoja kusali kwa lugha yake: “Tunamwomba Baba yetu wa mbinguni: “Baba yetu…”.

Salamu kutoka kwa Askofu 

Baada ya  hotuba ya Baba Mtakatifu Salamu kutoka kwa Askofu mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Finland; ambaye limshukuru Papa kwa kuwakaribisha mahujaji wa Kidini. Ujumbe huo ni wa kiekumene: pamoja na Walutheri na Wakatoliki, pia unajumuisha wawakilishi wa Kanisa la Kiorthodox. Amemshukur kwa hotuba na salamu: "Maneno yake, kuwa , yatabaki mioyoni mwao na yatapasha moto, leo na siku zijazo". “Tumejifunza kwamba unathamini kiasi kuliko kutia chumvi, unyenyekevu kuliko ukuu. Ndiyo maana leo tunaleta zawadi mbili, moja tofauti kidogo na moja rahisi.

Zawadi hizi mbili hazichukui nafasi nyingi, lakini tunatumaini zinaweza kukupa joto katika mwili na roho na kukupa furaha na ustawi. Kanisa letu limetoa mchango kwa shirika la Finn Church Aid: kwa pesa hizo zitawezekana kununua mablanketi mia moja kwa watoto katika maeneo magumu. Mablanketi haya yatawapa joto na kuwapa matumaini mapya. Zawadi ya pili ni jozi ya glavu iliyopambwa kwa nembo ya Mtakatifu Olav, kwa sababu mikono yake ya baraka inarudisha kwa furaha katika ulimwengu huu baridi ambao unahitaji kuhisi upendo, amani na ukombozi wa Mungu. Bwana akubariki na kukulinda kila siku.  Tumeunganishwa katika utume ambao Yesu Kristo ametukabidhi.”

19 January 2024, 18:33