Papa:Sikilizeni kilio cha watu wanataka amani
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mara baada ya Tafakari na Sala ya Malaika wa Bwana Dominika tarehe 28 Januari 2024, Baba Mtakatifu Francisko, kupitia katika dirisha la Jumba la Kitume amewambia waamini walikusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Vatican kuwa :“Kwa miaka mitatu sasa, kilio cha maumivu na kelele za silaha zimechukua nafasi ya tabasamu inayowatambulisha wakazi wa Myanmar. Kwa hiyo ninaungana na sauti ya baadhi ya Maaskofu wa Birimania “ili silaha za uharibifu zigeuzwe kuwa zana za ukuaji wa kibinadamu na haki.” Amani ni njia na ninazikaribisha pande zote zinazohusika kuchukua hatua za mazungumzo na kujivika uelewano, ili ardhi ya Myanmar ifikie lengo la upatanisho wa kidugu. Na upitishaji wa misaada ya kibinadamu unaweza kuruhusiwa kuhakikisha mahitaji ya kila mtu.”
Vita nyingine ukraine, Palestina na Israel
Baba Mtakatifu Francisko akiendelea pia amegeukia vita nyingine na kusema: “Na hali hiyo hiyo inafanyika Mashariki ya Kati, Palestina na Israel, na kila mahali kuna mapigano: heshimu idadi ya watu! Daima ninawaza kwa moyo wote waathirika, hasa raia, waliosababishwa na vita vya Ukraine. Tafadhali sikiliza kilio chao cha amani: kilio cha watu, ambao wamechoshwa na vurugu na wanataka vita ikome, ambayo ni maafa kwa watu na kushindwa kwa ubinadamu!”
Kuachiliwa mateka huko Haiti
Baba Mtakatifu akigeukia huko Visiwa vya Carribien ameonesha: “furaha ya kuachiliwa huru kwa Waamini watawa na watu wengine waliotekwa nyara pamoja nao huko Haiti Juma lililopita. Ninaomba wale ambao bado wametekwa nyara waachiliwe na kila aina ya vurugu ikome; kila mtu atoe mchango wake kwa maendeleo ya amani ya nchi, ambayo msaada mpya kutoka kwa jumuiya ya kimataifa unahitajika.”
Ukaribu na walioshambuliwa huko Instanbul, Uturuki
Baba Mtakatifu ameeleza: “ukaribu wangu kwa jumuiya ya Kanisa la Mtakatifu Maria Draperis huko Istanbul, ambalo lilipata shambulio la silaha wakati wa Misa iliyosababisha kifo cha mtu mmoja na majeraha kadhaa.”
Siku ya Ukoma kimataifa
Akikumbuka siku ya Kimataifa ya Ukoma, Baba Mtakatifu amesema: “Leo ni Siku ya Ukoma Duniani. Ninawatia moyo wale wanaohusika na uokoaji na ujumuishaji wa kijamii wa watu walioathiriwa na ugonjwa huu ambao, licha ya kupungua, bado ni miongoni mwa wanaoogopwa zaidi na unaathiri watu masikini na waliotengwa zaidi.”
Salamu kwa mahujaji wote
Baba Mtakatifu aidha ameendelea na salam una kusema kuwa: “Nawasalimu ninyi nyote mliotoka Roma, Italia na sehemu nyingi za dunia. Hasa, wanafunzi wa Taasisi ya ‘Puente Ajuda’, ya Olivenza (Hispania), na wale wa Taasisi ya ‘Mtakatifu Michelangelo Refalo’ ya Gozo.
Chama cha Viajana wakatoliki
Katika uwanja wa Mtakatifu Petro na juu ya Dirisha, Papa Francisko alikuwa na Wawakilishi wa Watoto wa Chama cha Vijana wa Matendo Katoliki walioandamana kwenye “msafara wa amani”. Baba Mtakatifu kwa njia hiyo akiwageukia amesema: “Sasa ninawageukia ninyi, wavulana na wasichana wa Chama cha Matendo ya vijana wakatoliki wa parokia na shule za Kikatoliki za Roma. Mmefika mwisho mwa “Msafara wa Amani”, ambapo mlitafakari juu ya wito wa kuwa walinzi wa uumbaji, zawadi kutoka kwa Mungu. Asante kwa uwepo wenu! Na asante kwa kujitolea kwenu kujenga jamii iliyo bora. Sasa tusikilize ujumbe ambao hawa marafiki zenu waliopo karibu yangu watatusomea.”
Katika ujumbe wa vijana hao unasema kuwa: walikuwa ni Wasichana na wavulana wa kanisa lwalisoma barua iliyoandaliwa kwa ajili ya Baba Mtakatifu Francisko, ambamo wanakumbuka kwamba kila mwaka wakiwa pamoja naye, wanafanya upya hamu yao ya amani kwa jiji zima na dunia nzima. “Siku hizi ni vigumu kufikiria kuhusu amani, vita vingi vinafanyika karibu na sisi pia: inaonekana kwamba hakuna anayejali kuhusu kufanya amani. Sisi, hata hivyo, tunataka kuwa upande wa amani, tukijaribu kuzima, kwa njia yetu ndogo, moto wa chuki na jeuri.” Wameeleza walivyopanda “mmea kuchanua lakini vita ni kama mti mkavu na usiso na kitu. Hii inawakumbusha kwamba dunia ni zawadi kutoka kwa Mungu: hatupaswi kuiharibu kwa chuki bali tuache ujumbe wa Yesu wa upendo ushamiri na Upendo hauwezi kuwepo bila Amani! Na lazima kutnza sayari kwa amani na kwamba “lazima sote tuitunze kama katika hifadhi ya asili.”
Kwa Msafara huu wa Amani, kwa hakika, watoto wa chama wameamua kuunga mkono mipango ya Legambiente na mpango wa Caritas ya Roma Io, ‘noi, tutti’. Nyumba yetu ni ya jumuiya. “Mpendwa Papa, sisi daima tunakuombea na kwa ajili ya mambo haya ambayo ni ya thamani kwetu. Tunakukabidhi wewe familia zetu, waelimishaji na wale wote wanaotutunza. Tunakupenda!” Mara baada ya ujumbe kusomwa na watoto hao, Baba Mtakatifu amewatakia Dominika njema. Tafadhali wasisahau kumuombea. Wameonavijana, watoto wa Chama cha Matendo katoliki ni wazuri! Wawe wajasiri! Mlo mwema, mchana mwema na kwaheri ya kuonana.