Papa Francisko tarehe 12 Januari 2024 amekutana na Kamati ya Kisayansi ya Mfuko wa Kumbukumbu ya Sauti na Picha za Kikatoliki. Papa Francisko tarehe 12 Januari 2024 amekutana na Kamati ya Kisayansi ya Mfuko wa Kumbukumbu ya Sauti na Picha za Kikatoliki.  (ANSA)

Umuhimu wa Kuhifadhi Sauti na Picha za Kikatoliki Kama Amana na Utajiri wa Kanisa

Baba Mtakatifu katika hotuba yake amewapongeza wajumbe wa Kamati hii; fedha kwa ajili ya Maadhimisho ya Jubilei ya Mwaka 2025 ya Ukristo; Umuhimu wa kujenga mahusiano na ushirikishwaji wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu, umuhimu wa pango hifadhi ya sauti sanjari na kuanza kuweka mpango mkakati wa kisayansi kwa ajili ya sauti na video! Papa amewapongeza wana kamati kwa kazi kubwa ya kulinda, kutunza na kuthaminisha kumbukumbu na amana hii.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Kamati ya Kisayansi ya Mfuko wa Kumbukumbu ya Sauti na Picha za Kikatoliki “Comitato Scientifico della Fondazione Memorie Audiovisive del Cattolicesimo” MAC, iliundwa kunako mwezi Machi 2023, kujibu dharura ya kitamaduni, ili kurejesha, kuhifadhi na hatimaye, kuimarisha amana na urithi wa kihistoria wa sauti na video zinazohusianishwa na Ukatoliki. Wajumbe wa Kamati hii, Ijumaa tarehe 12 Januari 2024 walikutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican. Baba Mtakatifu katika hotuba yake amewapongeza wajumbe wa Kamati hii; fedha kwa ajili ya Maadhimisho ya Jubilei ya Mwaka 2025 ya Ukristo; Umuhimu wa kujenga mahusiano na ushirikishwaji wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu, umuhimu wa pango hifadhi ya sauti sanjari na kuanza kuweka mpango mkakati wa kisayansi kwa ajili ya sauti na video! Baba Mtakatifu anawapongeza kwa kazi kubwa waliyokwisha kuifanya kama sehemu ya kulinda, kutunza na kuthaminisha kumbukumbu ya amana na urithi wa sauti na video. Huu ni mradi mkubwa unaohusishwa na hesabu ya watu, vyanzo vya sauti na video mintarafu maadhimidho ya Jubilei na historia ya Kanisa, kama kuanzishwa kwa Hospitali ya “Bambino Gesù, Mfuko wa Don Carlo Gnocchi ni ushuhuda wa utashi wa utekelezaji wa malengo ya Kamati hii.

Kamati imefanya kazi kubwa ya kulinda na kuhifadhi
Kamati imefanya kazi kubwa ya kulinda na kuhifadhi

Baba Mtakatifu anasikitika kusema kwamba, hakuna kituo kikuu ambacho kimetengwa maalum kwa ajili ya kuhifadhi na hatimaye kurithisha amana na utajiri huu kwa vizazi vijavyo, lakini kumbukumbu ya Video za Mababa Watakatifu na za Kanisa ni matukio rejea yanayoweza kuongoza mafundisho ya Kanisa yaliyohifadhiwa na yanayoshirikisha matukio muhimu ili kupata mwelekeo mpana zaidi. Mfuko wa Kumbukumbu ya Sauti na Picha za Kikatoliki ni mkakati ulioanzishwa na Baba Mtakatifu Francisko na kwamba, unapaswa kukuzwa na kuendelezwa zaidi, kwa kushirikisha Vyuo vikuu pamoja na Taasisi za Elimu ya juu pamoja na wadau wengine, ili kulinda na kuhifadhi audio-video amana na utajiri wa Kanisa. Hii inawezekana ikiwa kama watashirikiana na Maktaba ya Kitume pamoja na Pango Hifadhi la Nyaraka za Vatican.

Ushirikiano na vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu ni muhimu
Ushirikiano na vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu ni muhimu

Kazi ya Mfuko wa Kumbukumbu ya Sauti na Picha za Kikatoliki unahitaji mageuzi makubwa ya kitamaduni ya mapango hifadhi ya Kanisa pamoja na fedha inayohitajika kuwekeza ili kuweza kuratibisha maisha na utume wa Kanisa; Kuhifadhi amana na utajiri huu kwani, taasisi nyingi kutokana na ukwasi zinateseka sana kuhifadhi nyaraka hizi, kutokana na uhaba wa rasilimali fedha na watu, lakini kwa njia ya ushirikiano changamoto hizi zinaweza kupatiwa ufumbuzi. Kumbe, kuna haja ya kuwekeza katika uwanja huu na malipo yatafanyika mintarafu watalii wanapotembelea maeneo haya kihistoria, kitamaduni, kiuchumi na kidini. Washirikiane na Kumbukumbu ya Filamu za Vatican “Filmoteca Vaticana” kwani ina amana na utajiri mkubwa mintarafu changamoto hizi. Baba Mtakatifu Francisko anawashukuru viongongozi wote wa MAC, kwa kuanza kukarabati Sinema za Jubilei, kumbe, zinapaswa kushirikishwa taasisi za tafti ili kuweza kuunga mkono juhudi hizi. Kama sehemu ya maandilizi ya Jubilei ya Miaka 2025 za Ukristo hii ni njia inayoonesha kuthamini amana na utajiri wa Kanisa.

Kamati ya Sayansi
16 January 2024, 08:22