Visiwa vya Kanari,barua za wahamiaji kwa Papa:saidia kuwa na uelewa wa Ulaya
Salvatore Cernuzio – na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika tukio la mkutano Baba Mtakatifu alipokea ujumbe kutoka kwa kwa Mamadou Malal Diallo aliyeomba katika barua yake kwa Papa kumtaka azungumze kwa niaba yake na kwa ajili ya wahamiaji wengine wa kiafrika ambao wametua katika Visiwa vya Kanari. Katika barua hiyo inabainisha kuwa: “Mimi sio mtu wa kumwomba chochote Baba Mtakatifu, lakini kama angeona inafaa na inafaa, angeweza kutoa maneno machache ya kutia moyo kwa watu wa Afrika, kwa kuwa kutokana na nafasi ya upendeleo aliyonayo angesikika duniani kote kama kipaza sauti kikubwa kuleta misimamo karibu, kati ya Afrika na Ulaya, kuzungumza kiutamaduni, kukuza uelewa na kuueneza."
Kwa njia hiyo ujumbe huo katika ukurasa ulioandikwa kwenye kompyuta, ukiwa na tarehe ya tarehe 15 Januari na sahihi katika mwandiko wa karibu wa kitoto, uliwasilishwa kwa Papa Francisko asubuhi tarehe 15 Januari 2024 na rais wa serikali ya Visiwa vya Kanari, Fernando Clavijo Batlle, aliyepokelewa kwa kwa Mkutano katika Jumba la Kitume mjini Vatican. Pamoja naye makamu wa rais Manuel Domínguez González na wasaidizi wake, ikiwa ni pamoja na maaskofu watatu: Bernardo Álvarez, José Mazuelos na Cristóbal Déniz, wanaowakilisha Kanisa la Kanari lililohusika sana katika dharura ya uhamiaji na vituo vya mapokezi na usambazaji wa chakula na nguo.
Ujumbe wa wahamiaji
Mkutano wao ulidumu kama dakika 40 na, mwisho, barua mbili ziliwekwa mikononi mwa Papa Francisko ambapo ile ya Mamadou, raia wa Guinea, ambaye anasimulia historia yake tangu alipowasili mnamo 2008, kizuizi cha lugha, mshtuko wa kiutamaduni na ukosefu wa fursa zilizopo kwa watu kama yeye, hadi kazi yake ya sasa kama mpatanishi na mkalimani wa kiutamaduni. Na wakati huo huo barua nyingine kutoka kwa kundi la wahamiaji wa kiafrika, ambao baadhi pia ni watoto wadogo, wanaoishi El Hierro, kinachojulikana kama ‘Isla del Meridiano’kwa lugha ya Kihispania yaani Kisiwa cha Kusini. Hiki ni, kisiwa kidogo zaidi kati ya visiwa vilivyomo ambacho hata hivyo kimekuwa mahali pa kuwasili kwa wahamiaji kinachotafutwa moja kwa moja na wale ambao wanakabiliwa na ‘Njia ya Atlantiki’ ya hatari na ambayo huona mtiririko unaoendelea wa kutua kwenye mwambao wake, inakabidiriwa walikuwa zaidi ya 1,100, mnamo Oktoba 2023, kwa masaa 48 siku ya Jumamosi tarehe 13 Januari 2024 walikuwa ni 650.
Kisiwa kimejaa, lakini kiko tayari kukaribisha
Ni janga halisi kweli, kwa nchi na idadi ya watu ambao wanasema ‘wamejaa lakini bado wanapatikana ili kuonesha ukarimu, mshikamano na ujasiri kwa watu wanaokimbia njaa, kiu na kifo. Watoto wenyewe wanasema katika barua wakati, wakielezea jinsi walivyo paswa kuondoka nyumbani na familia kwamba “tunakosa mengi” (Haikuwa rahisi kuwaacha, lakini tuko katika hatarini huko, hatuwezi kujifunza, hakuna kazi ya kulisha familia, ni ngumu sana kuendelea huko bila mioyo yetu kuacha kuamini fursa hiyo”, waliandika katika barua), kwa herufi kubwa huandika “ASANTE SANA” kwa watu wote wa El Hierro “wanaotuunga mkono, kutusaidia na kututia moyo tuendelee kupambana ili kutimiza ndoto zetu. Tunataka kuwa na uwezo wa kusoma na kisha, tutakapokuwa wakubwa, tufanye kazi ili kusaidia familia zetu.”
Ushirikiano na maendeleo kwa Afrika
Rais aliripoti haya yote kwa Papa, ambaye alionekana kuwa makini, kupendezwa na kusikitishwa sana na hali hii, kama ilivyoripotiwa na Clavijo mwenyewe kwa kundi la waandishi wa habari waliokutana katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mara baada ya mkutano huo huko Jumba la Kitume mjini Vatican. ‘Mimi na makamu wa rais tuliweza kuzungumza juu ya ukweli kwamba tatizo la uhamiaji kutoka Afrika linaweza kutatuliwa huko Afrika, kwamba tunahitaji ushirikiano na sera za maendeleo, “alielezea rais, huku akihakikishia kwamba “ubinadamu hautasahaulika kamwe, yaani, ufahamu kwamba kuna watu wanaojaribu kutoroka njaa, kifo na umaskini na kwamba watu wa Visiwa vya Kanari pia siku moja walikuwa wahamiaji.”
Msaada wa Papa
Rais Clavijo aliripoti kwamba Papa Francisko, ambaye tayari katika barua iliyoandikwa mnamo tarehe 20 Novemba 2023 aliwashukuru maaskofu wa Visiwa vya Kanari na wakazi wote “kwa kuwafungulia milango ya mioyo yenu kwa wale wanaoteseka, na kwamba si tu kutambua mshikamano wa watu wa Kanari, kujitolea kwake kuelekea walio dhaifu na wasiojiweza zaidi, lakini pia alituambia kwamba anaomba tatizo hilo litatuliwe.” Na hiyo ni kwa pande zote mbili kutoka kwa mtazamo wa mtiririko wa watu wanaoingia kwenye Njia ya Atlantiki ya hatari sana, na kutoka kwa mtazamo wa msaada wa mapokezi. “Tunazungumza juu ya watu elfu 40 ambao wamefika kwenye ufukwe wetu mnamo 2023, asilimia 70% ya wahamiaji wote wanaofika Hispania, na kila siku watu 16 wanakufa wakijaribu kutafuta maisha bora ya baadaye, alisisitiza mkuu huyo.
Kufanya kazi pamoja
“Hatuna uwezo wa kudhibiti hali kama hii peke yetu,” alisitiza Makamu wa Rais Domínguez. “Tumejaza sana, tunafanya kila tuwezalo kuwasaidia, kuna mshikamano.” Matumaini ya viongozi wa Visiwa hivyo ni kwamba ziara yao kwa Papa inaweza “kusaidia taasisi za Ulaya, serikali ya Hispania na nchi nyingine za Ulaya kufahamu ukweli wa Afrika, bara ambalo kwa ukame, vita, Machafuko ya kisiasa ni tatizo ambalo tunalifanyia kazi kwa dhati kwa ushirikiano au litaendelea kwa muda mrefu,” alisema Clavijo.
Janga la watoto ambao hawajasindikizwa
Papa Francisko mwenyewe, kama ilivyoripotiwa na viongozi wa Visiwa vya Kanari kwa waandishi wa habari, ni kwamba amewafahamisha kwamba ni muhimu na muhimu kufahamu kwamba sera za maendeleo lazima zitumike katika Afrika ili kuzuia watu kukimbia kutafuta njia bora zaidi. baadaye. Badaye aytaimbea na watamshukuru, walisema. Papa - ambaye siku zote aliomba kutofunga milango lakini, wakati huo huo, kutathmini uendelevu wa kila nchi inayotua - alikuwa akifahamu vyema kile tulichokuwa tunateseka katika eneo letu kuhusu suala la watoto wadogo wasiokuwa na mtu wa kuwasindikiza. Moja ya matatizo makubwa zaidi kwa sasa katika Visiwa vya Canary, kutokana na kuongezeka kwa idadi ambayo inafanya kuwa karibu haiwezekani kuhakikisha haki zao za ushirikiano, utoto na mipango ya maisha. Ilikuwa mshangao mkubwa kwamba Papa alikuwa makini sana kwa suala fulani kama letu,” alisema.
Mwaliko wa kutembelea visiwa
Katikati ya salamu, baraka na zawadi kati ya hizo, kulikuwa na Hati ya 1462 ya kuwapatia mamlaka ya kiaskofu wa Visiwa vya Kanari kwa ajili ya kumtenga mtu yeyote aliyewafanya watu wa Asili wa Guanches kuwa watumwa na kifurushi cha pipi kutoka Katika Kisiwa cha la Laguna. Na Makamu rais hakukosa kutoa mwaliko kwa Papa ili kutua angalau katika visiwa hivyo: “Tulimwalika na ningependa iwe hivyo. Pia niliwaomba maaskofu kumwalika.”
Visiwa vya Kanari viko wapi?
Ikumbukwe Visiwa vya Kanari (kwa Kihispania: Islas Canarias) ni funguvisiwa la Afrika ya Kaskazini katika bahari ya Atlantiki. Viko baharini km 150 magharibi kwa Moroco. Umbali na Hispania ni masaa mawili tu kwa ndege. Visiwa vikubwa ni saba ambavyo ni:El Hierro, La Gomera, La Palma na Tenerife ambavyo vinaunda mkoa wa Mtakatifu Cruz waTenerife, pia kuna Gran Canaria , Fuerteventura na Lanzarote ambavyo vinaunda mkoa wa Las Palmas, na tena kuna visiwa vidogo sita vya Alegranza, Kisiwa cha Lobos, La Graciosa, Montaña Clara, Roque del Este na Roque del Oeste, vyote vya mkoa wa Las Palmas. Kisiasa visiwa hivyo ni kati ya maeneo ya kujitawala ndani ya ufalme wa Hispania. Miji mikubwa ni Las Palmas de Gran Canaria (wakazi 378.628), SMtakatifu Cruz de Tenerife (wakazi 221.567), Mtakatifu Cristóbal de la Laguna (wakazi 141.627), Telde (wakazi 96.547) na Arona (79.377). Miji mikuu ni Mtakatifu Cruz de Tenerife na Las Palmas de Gran Canaria. Makao ya mkuu ya serikali ya eneo huhamahama kati ya miji hiyo miwili kila baada ya miaka minne.Kutokana na uzuri wa nchi na hali ya hewa ambayo ni nzuri kwa mwaka mzima utalii umekuwa nguzo ya uchumi wa visiwa hivyo vya Kanari pamoja na kilimo cha mazao ya biashara yanayopelekwa Ulaya, hasa ndizi na tumbaku.