Burkina Faso,Papa aonesha huzuni kufuatia mashambulizi ya Kanisa na Msikiti
Vatican News
Katika Telegramu iliyotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican Jumatatu tarehe 26 Februari 2024 iliyoelekezwa kwa Askofu Laurent Dabiré, Rais wa Baraza la Maaskofu Nchini Burkina Faso na Niger, huko Ouagadougou, Papa Francisko anatoa rambi rambi kwa ajili ya waathirika wa mashambulizi mawili ya kigaidi nchini Burkina Faso, yaliyotokea Dominika tarehe 25 Februari 2024
Uchungu kwa kupoteza maisha ya binadamu
Baba Mtakatifu akiwa bado anapumzika kutokana na mafua alieleza “uchungu wa kina alioupata baada ya kupata taarifa mbaya za kigaidi katika Kanisa Katoliki la Essakane na vile vile dhidi ya Msikiti wa Natiaboani. Papa Francisko anaungana na maombolezo ya familia, akielezea ukaribu wake na uchungu wa kupoteza maisha ya binadamu. “Huzuni humo ndani ya roho yake kwa wazo la wale wote ambao walikabiliwa wa Jumuiya ya kiislamu.”
Kuheshimu maeneo matakatifu
Katika Telegramu hiyo inasomeka kuwa: “Papa anasali kwa ajili ya pumziko la milele marehemu na kuwakabidhi kwa huruma ya Mungu, na kwa ajili ya uponyaji wa majeruhi." Na anakumbusha kwamba: “chuki siyo suluhisho la migogoro.” Na wakati huo huo anawaalika: “kuheshimu maeneo matakatifu na kupambana dhidi ya vurugu kwa ajili ya kuhamasisha thamani za amani.”
Bwana alete nguvu na faraja kwa waliokumbwa na mkasa
Kwa Bwana Papa amemwomba “alete nguvu na faraja kwa wale wote ambao wamekumbwa na mikasa hiyo.” Baba Mtakatifu anaomba baraka nyingi za Mungu ziwashukie Wana na mabinti wa Burkina Faso na taifa zima."