Papa amehimiza Harakati ya CL kudumisha Umoja
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Baada ya Mkutano wa Davide Prosperi, Rais wa Harakati ya Comunione e Liberazo na Askofu Filippo Santoro, Baba Mtakatifu Francisko alimtumia barua rais hiyo katika fursa ya kifo cha Padre Giusani na miaka 70 ya harakati hiyo, ambapo Tunachapisha barua ya Papa aliyomwandikia rais wa Haraka hiyo iliyowekwa saini tarehe 30 Januari 2025 katika nyumba ya Mtakatifu Marta mjini Vatican.
PAPA FRANCISKO
Ndugu mpendwa, kwa moyo wa shukrani kwa ziara yako ya hivi karibuni, katika tarehe 15 Januari, ambapo wewe na Monsinyo Santoro, mmenijuza kuhusu maisha ya Harakati ya Comunione na Liberazione na wa Memores Domini ningependa kukutia moyo. Ninamshukuru Bwana kwa uchangamfu ambao harakati hiyoinaendelea kudhihirisha katika kazi yake ya uinjilishaji na upendo kwa wanaume na wanawake wa leo hii. Inanifariji sana kuona jinsi ambavyo harakati hiyo imekubali kwa umakini na kwa manufaa maneno niliyowaambia wakati wa Mkutano wa tarehe 15 Oktoba 2022, pamoja na yale ya Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha. Ninakuhimiza kuendelea na njia hiyo, na ninakuthibitisha katika kazi uliyofanya katika kipindi hiki.
Katika hafla ya sherehe za kuzaliwa Mbinguni Mtumishi wa Mungu, Padre Luigi Giussani na kumbukumbu ya miaka sabini ya kuzaliwa kwa Harakati nina shauku sana kupendekeza kwenu na kwa wafuasi wote ili kutunza Umoja kati yen una siyo kipekee kwani kiukweli, katika kufuata wachungaji wa Kanisa mnaweza kuwa kwa wakati malezi ya kuzaa matunda ya karama ambayo Roho Mtakatifu alimpatia Padre Giussani: “Nawapeni amri mpya, kwamba mpendane; kama vile nilivyowapenda ninyi, vivyo hivyo nanyi pendaneni. Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.” Ili kulinda umoja na kuhakikisha kwamba karama ina uwezo wa kufasiri zaidi na vya kutosha nyakati ambazo mmeitwa kutoa ushuhuda wa imani yetu katika Yesu Kristo, ni muhimu kwenda zaidi ya tafsiri za kibinafsi, kwa bahati mbaya ambazo bado zipo, ambazo zinaweza kuashiria hatari ya maono ya upande mmoja wa karama.
Kwa hivyo ninakuhimiza wewe, pamoja na washirika wako, kuendeleza kazi iliyofanywa ambayo inalenga kuhifadhi maono muhimu. Njia ya elimu iliyopendekezwa na wewe na wale wanaokusaidia katika kuongoza harakati pia inasaidia kusahihisha baadhi ya kutoelewana na kuendeleza utume wako kwa uaminifu kwa karama iliyotolewa kwa Kanisa kupitia Padre Giussani. Katika kipindi hiki ambacho ni muhimu sana kwa historia yenu baada ya kifo cha mwanzilishi, kwa hiyo ninatoa mwaliko kwa washiriki wote wa harakati kufuata njia iliyofanywa, chini ya uongozi wa Kanisa na kushirikiana na kupatikana na uaminifu na wale ambao wameitwa kuongoza Harakati. Ni utii huu tu, unaoendelea kugunduliwa na kumwilishwa, utaweza kuhakikisha miongoni mwenu uzoefu mzuri zaidi wa maisha ya Kikristo na kufanywa upya kwa uwepo wenu ulimwenguni, kwa manufaa ya Kanisa zima. Bwana awabariki na Mama yetu akulinde. Na tafadhali msisahau kuniombea.
Barua ya Rais wa Harakati ya ‘Comunione e Liberazione’
Kwa upande wa Rais wa Harakati hiyo aliwaandikia waamini wake na kuichapisha barua ya Papa kuwa: “Marafiki wapendwa, Januari 15 iliyopita Askofu Filippo Santoro na mimi tulipata fursa ya kukutana na Papa Francisko katika hadhara ya faragha. Tuliweza kumwambia kuhusu hatua zilizochukuliwa na Udugu na Memores Domini katika mwaka huu uliopita, na kufanya upya imani yetu katika ubaba wake katika safari ya kumfuata Kristo na Kanisa. Kwa furaha kubwa ninashirikisha nanyi nyote barua ambayo Papa alitaka kututumia wakati wa kumbukumbu ya kifo cha Padre Giussani na kwa miaka 70 tangu kuzaliwa kwa Harakati. Ni maneno yaliyojaa maana kwa wakati tunaoishi. Tunaikaribisha kwa kupatikana kwa moyo ili kutambua na mtazamo wa Papa juu ya uzoefu wa imani ya kila mmoja wetu na jumuiya zetu. Pamoja na Askofu Filippo Santoro, ninahisi shukrani za dhati kwa ishara hii ya heshima na upendo kwa upande wa Baba Mtakatifu. Ninawaalika, kama anavyotuomba, tuendelee kumuombea, ninawakumbatia. Davide Prosperi.