Tafuta

2024.02.03 Papa amekutana na Walimu na wanafunzi wa Chuo cha  Rotondi, cha  Gorla Minore 2024.02.03 Papa amekutana na Walimu na wanafunzi wa Chuo cha Rotondi, cha Gorla Minore  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa amekutana na wanafunzi na walimu wa Chuo cha Rotondi cha Gorla

Papa amekutana na wanafunzi na walimu wa Chuo cha Rotondi cha Gorla Minore(Varese),shule kongwe zaidi ya Kikatoliki nchini Italia na kusisitiza wamba“inapobidi ni muhimu kujua jinsi ya kubadili na kukubali maoni na njia za kufikiri tofauti katika kila kitu ambacho haki maana.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 3 Februari 2024 amekutana na kuwakaribisha  watoto, wazazi na walimu wa Chuo cha Rotondi di Gorla ambayo ni shule kongwe zaidi ya Kikatoliki nchini Italia. Amemsalimu Mkuu wa Shule hiyo Padre Andrea Cattaneo.  Wamekutana katika fursa ya  kumbukumbu ya miaka 425 tangu kuanzishwa kwa shule yao, iliyoanzishwa mnamo mwaka wa 1599: zaidi ya karne nne za historia, na inaonekana inabebwa vizuri. Papa amefuarahi kuwaona ha ona hasa  watu, ambao kwa nyuso zao  changa na changamfu, na ndoto, miradi na matamanio wanayobeba moyoni mwao hutoa maana na thamani kwa urithi wa zamani kama huo. Kwa uwepo wao, unashuhudia jinsi ambavyo Chuo cha  Rotondi, aminifu kwa utamaduni wake wa kielimu, kilivyokua kwa wakati, kikibadilika na kubadilika mara nyingi ili kukidhi mahitaji ya nyakati tofauti za kihistoria.

Papa na watto kutoka Rotondi
Papa na watto kutoka Rotondi

Kwanza kutoka katika asili na mchango wa Giovanni Terzaghi, hadi mabadiliko yaliyofanyika chini ya serikali ya Austria na Savoy, ya mwisho na Gambera Rotondi - ambaye wanachukua jina la shule hiyo sasa - kwa shida za vita viwili vya dunia, kwa changamoto za baada ya vita, hadi kuwa leo shule kongwe ya Kikatoliki ya faragha nchini Italia. Na haya yote yana ujumbe muhimu, ambao Papa Francisko amewaalika kutafakari: ni muhimu kujua jinsi ya kubadilika ili kubaki mwaminifu kwa utambulisho na utume wa mtu.

Walimu , wazazi na wanafunzi wa shule ya Rotondi
Walimu , wazazi na wanafunzi wa shule ya Rotondi

Papa amewatia moyo wa  kujitolea kwa bidii kwa shughuli zao za shule, lakini kila wakati kwa nia iliyo wazi kwa mambo mapya. Hasa,  hao  watu, kutafuta ukweli katika kila kitu, bila kujiruhusu kuathiriwa na mitindo ya sasa au kwa mawazo ya kawaida, na kupenda au makubaliano ya wafuasi: haya sio mambo muhimu sana, kiukweli kuyategemea sana kunaweza kutuondolea uhuru wetu. Wakati huo huo, hata hivyo, wasiogope, inapobidi, kubadili na kukubali maoni na njia za kufikiri tofauti na zao katika kila kitu ambacho sio muhimu: kuwa wapenzi wa kweli wa ukweli, na kwa hiyo daima kupatikana kusikiliza na kujadili. Yesu alitufundisha kwamba ukweli hutuweka huru (taz Yohana 8:32), na alisema hivi kwa watu ambao walijitahidi kukubali njia yake mpya ya kusoma Maandiko, kwa sababu kiukweli hawakuyajua vya kutosha (taz Marko 12:24). -27) na waliogopa kubadilisha mifumo yao. Je, mnaona? Ujinga huzaa woga na woga huzaa kutovumiliana.

Walimu, wazazi na wanafunzi wa shule ya Rotondi
Walimu, wazazi na wanafunzi wa shule ya Rotondi

“Ninyi msifanye hivyo. Jifunze kuwa kama timu, pamoja, na kila wakati kwa furaha! Ujuzi, kiukweli, hukua kupitia kushiriki na wengine. Tunasoma ili kukua, na kukua kunamaanisha kukomaa pamoja, kuwasiliana: mazungumzo na Mungu, na walimu na waelimishaji wengine, na wazazi; mazungumzo na kila mmoja na pia na wale wanaofikiria tofauti, ili kila wakati kujifunza mambo mapya na kuruhusu kila mtu kutoka  akiwa bora zaidi yake mwenyewe. Baada ya yote, hivi ndivyo kauli mbiu ya shule yenu inavyosema: ‘Erudire et edocere’, yaani ni, kutoa kila mtu zana zinazohitajika kusoma ukweli na kujieleza kwa uhuru wa ubunifu.” Papa Francisko amesisitiza. Kwa kuhitimisha Papa amewashukuru tena kufika kwao na kwa kujitolea kwao katika kuendeleza jumuiya yao ya elimu. Amewaomba waendelee huvyo huki wakilinda na kusasisha urithi waliopokea. Amewabariki kwa moyo wote. Na ikiwapendeza wasisahau kusali kwa ajili yake.

Papa na watoto wa shule, walimu na wazazi wao
03 February 2024, 16:22