Papa akimsikiliza Kardinali Simoni akiwa katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican 14 Februari 2024. Papa akimsikiliza Kardinali Simoni akiwa katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican 14 Februari 2024.   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa amshukuru Kardinali Simoni kwa ushuhuda wake

Kardinali mwenye umri wa miaka 95,shuhuda aliye hai wa udikteta nchini Albania alikabiliwa na vitisho vya kufungwa jela,mateso na kifo kwa takriban miaka 28 wakati wa utawala wa kikomunisti,ambaye alikuwa katika Katekesi ya Papa.Papa:'Namshukuru kwani hata leo anaendelea kushuhudia na kulifanyia kazi Kanisa,bila kukata tamaa.'

Salvatore Cernuzio  na Angella Rwezaula- Vatican.

Kwa  mara ya kwanza ulimwengu ulimuona Papa Francisko analia, Papa ambaye alikuwa amechaguliwa mwaka mmoja na nusu , ilikuwa ni tarehe 21 Septemba 2014 , wakati katika safari yake ya kwanza ya kimataifa nchini Albania, katika  mkutano na Mapadre  huko Tirana, nchini Albania alisikiliza ushuhuda wa Padre  Ernest Simoni Troshani. Padre  huyo mzee mwenye sauti nyembamba, akitoka jimbo la Shkodrë-Pult, alikuwa atimize miaka 88 siku chache baadaye;  na alikuwa amekaa karibu miaka 28 gerezani, mateso, vitisho vya kifo na kazi ya kulazimishwa wakati wa mateso ya serikali ya Enver Hoxha, ambaye alitangaza Albania  kuwa “nchi ya kwanza isiyoamini Mungu duniani.” Siku hiyo, Padre huyo  alimwambia Papa kuhusu kipindi kikatili kwa nchi yake, ambayo yeye ndiye padre pekee aliye hai.  Papa Francisko, baada ya kusikiliza ushuhuda wake kwa ukimya na kutoa miwani yake alikausha macho yake,  na alikuwa amemkumbatia kwa muda mrefu, huku akiweka paji la uso wake kwenye paji la padri huyo. Miaka miwili baadaye, wakati wa kuwateua makardinali wapya 2016, Baba Mtakatifu alimuunda kuwa Kardinali kama ishara ya shukrani kwa ushuhuda huu wa “kuuawa kwa imani.”

Mashahidi wengi wa siku hizi

Kwa njia hiyo Jumatano tarehe 14 Februari 2024, Kardinali Simoni alikuwepo kwenye katekesi ya Papa  akiwa ameketi kati ya viti vya pembeni vya jukwaa katika Ukumbi wa Paulo VI sehemu iliyotengwa kwa ajili ya maaskofu na makardinali. Papa Fransisko baada ya katekesi wakati wa salamu za lugha mbalimbali, alielekeza macho yake kwake ili kumsalimia “kwa namna ya pekee” na kumsifu mbele ya maelfu ya waamini waliohudhuria. Papa Francisko bila kusoma maandiko alisema: “Sisi sote tumesoma, tumesikia, historia za wafia dini wa kwanza wa Kanisa, wengi wao. Hata hapa, tulipo Vatikani kuna makaburi na wengi walinyongwa hapa na kuzikwa hapa. Unapochimba, unakuta makaburi haya.” Lakini hata leo kuna wafia imani wengi duniani kote, wengi, labda zaidi ya hapo mwanzo. Kuna wengi wanaoteswa kwa ajili ya imani yao.”

Papa akisalimiana na Kardinali Ernest Simoni (95) 14 Februari 2024
Papa akisalimiana na Kardinali Ernest Simoni (95) 14 Februari 2024

Bado anafanya kazi kwa ajili ya Kanisa

Baba Mtakatifu aliendelea kusema, kuwa  “ leo ninachukua fursa ya kumsalimia kwa namna ya pekee shahidi aliye hai”, Kardinali Simoni. Yeye, akiwa Padre, askofu, aliishi gerezani kwa miaka 28, katika gereza la kikomunisti ya Albania, labda mateso ya kikatili na ya kikatili zaidi.” Leo hii kardinali wa Albania “anaendelea kutoa ushuhuda. Na kama yeye,  kuna wengi, wengi, wengi.” Akimgeukia yeye alisema “Sasa ana umri wa miaka 95, na anaendelea kufanya kazi kwa ajili ya Kanisa bila kukatishwa tamaa. Ndugu mpendwa, ninakushukuru kwa ushuhuda wako. Asante.

Maneno ya Papa akirudi kutoka Tirana

Maneno ya kutia moyo kutoka kwa Papa mwishoni mwa katekesi yake yaliambatana na wito mpya ya dhati ya kutosahau, hasa wakati wa Kwaresima, ‘Ukraine iliyoteswa na Palestina na Israel ambayo inateseka sana na wale wanaoteseka na vita ambao wamekumbuka wale waliotamkwa kwenye ndege wakirudi kutoka Tirana.

Papa na Kardinali Ernest Simoni wakati wa Ziara ya Kitume huko Albania 21 .09.2014
Papa na Kardinali Ernest Simoni wakati wa Ziara ya Kitume huko Albania 21 .09.2014

Wakati wa mahojiano ya kawaida, Papa  Francisko alishiriki na waandishi wa habari hisia zake kwa kusikia historia ya Simoni moja kwa moja kutoka kwenye midomo yake: “Kiukweli kusikia shahidi akiongea kuhusu kifo chake cha imani ni jambo la nguvu. Nadhani sote tuliguswa na mashahidi hawa ambao walizungumza kwa kawaida. unyenyekevu, na karibu walionekana wakisimulia historia za maisha ya mtu mwingine.”

Mons. Simoni Aliteuliwa kuwa Kardinali 2016
Mons. Simoni Aliteuliwa kuwa Kardinali 2016

Kukamatwa, vitisho, mateso

Padre  Ernest alikamatwa usiku wa Noeli 1963, mwishoni mwa Misa huko Barbullush. Walikuwa wamemshutumu kuwa adui wa watu pia kwa sababu ya Misa ya ukumbusho iliyoadhimishwa kwa ajili ya roho ya Rais Kennedy ambaye alikuwa amefariki mwezi mmoja kabla. Misa ambayo, yeye mwenyewe alisema, “Niliadhimisha kulingana na maagizo yaliyotolewa na Paulo VI kwa mapadre wote wa ulimwengu.” Katika chumba cha faragha, ambapo alikaa kwa miaka kumi na minane, walimletea rafiki mwenye kazi ya kumpeleleza na kuwaamuru ndugu wengine kurekodi hasira ya kutabiri dhidi ya serikali. Kulikuwa na machache ya kuripoti kuhusu Padre Ernest, maneno tu ya msamaha na maombi yalitoka kinywani mwa kuhani huyo. “Yesu alitufundisha kuwapenda adui zetu na kuwasamehe, na kwamba lazima tufanye kazi kwa manufaa ya watu,”aliendelea kusema. Awali alihukumiwa kifo, hukumu yake ilibadilishwa kuwa kazi ya kulazimishwa. Miaka ishirini na mitano ya kazi ya kulazimishwa katika vichuguu giza vya migodi ya Spac na kisha kwenye mifereji ya maji taka ya Scutari.

Misa na maungamo kwa siri ndani jela

Wakati wa kifungo chake, Padre Simoni alisema kwamba aliadhimisha Misa ya Kilatini kutoka katika kumbukumbu, kwamba alithibitishwa kwa wafungwa wengine, kuwa baba wa kiroho wa baadhi yao, na kusambaza Komunyo, pamoja na mwenyeji aliyezitengeneza kwa siri kwenye majiko madogo na divai iliyotengenezwa kwa juisi ya zabibu. Kila kitu daima kwa siri. Mara baada ya kuwa huru, tarehe 5 Septemba 1990, alithibitisha msamaha wake kwa watesi wake, akiomba huruma ya Baba kwa ajili yao.

Utambuzi wa Heshima wa Kardinali Ernest Simoni nchini Albania
Utambuzi wa Heshima wa Kardinali Ernest Simoni nchini Albania

Kisha alianza kutumika katika vijiji, zaidi ya yote akiwasaidia watu kulipiza kwa msalaba wa Kristo” kupatanisha na kuondoa chuki mioyoni mwao. Ibada ambayo haikukatizwa kamwe, si kutokana na umri wake wala kuteuliwa kwake kuwa Kardinali. Ambapo, Kardinali alikuwa na hamu ya kusema, si kitu kingine isipokuwa kutambuliwa kwa wafia dini na Wakatoliki wote walioteswa katika ardhi yake. Ikiwa ni pamoja na pia kadinali wa kwanza wa Kialbania katika historia, aliyeundwa mwaka 1994 na Mtakatifu Yohane  Paulo II: Mikel Koliqi (1902-1997), raia mwenzake wa Scutari na kama Simoni aliyefungwa kwa muda mrefu katika magereza ya serikali, ambapo alitumikia kifungo cha miaka 31.

Papa na Kardinali Simoni (95) kutoka Albania
14 February 2024, 16:19