Papa atuma salamu za rambi rambi huko Firenze
Katika telegramu ya Papa iliyotumwa kwa Kardinali Guseppe Beroti,Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Firenze,iliyotiwa saini na Katibu wa Vatican kufuatia na ajali iliyotokea 16 Februari,Papa anaelezea kwa familia za waathiriwa hisia za ukaribu na rambi rambi pamoja na ushiriki hai wake kwa uchungu wa raia wote.
Vatican News
Jumamosi tarehe 17 Februari 2024 Papa Francisko ametuma Telegram iliyotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, kuhusiana na ajali kazini huko Firenze Italia iliyotokea tarehe 16 Februari 2024. Katika telegram hiyo iliyoelekezwa kwa Kardinali Guseppe Beroti, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Firenze, inabainisha kuwa kwa kupokea taarifa ya ajali liyotokea katika ujenzi wa Supamarket asubuhi ambayo ilisababisha vifo vya baadhi ya wanyakazi na kujeruhi wengine, Baba Mtakatifu anakabidhi yeye kuelezea kwa familia za waathiriwa hisia za ukaribu na rambi rambi pamoja na ushiriki hai wake kwa uchungu wa raia wote.
17 February 2024, 15:25