Tafuta

Maandalizi ya kikao cha pili cha Mkutano Mkuu wa XVI utafanyika kuanzia Jumatano tarehe 2 Oktoba hadi Dominika tarehe 27 Oktoba 2024. Maandalizi ya kikao cha pili cha Mkutano Mkuu wa XVI utafanyika kuanzia Jumatano tarehe 2 Oktoba hadi Dominika tarehe 27 Oktoba 2024.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa azindua vikundi vya mafunzo juu ya mada zilizojitokeza katika Sinodi ya 2023

Katika maelezo ya maandishi ya Mkoni wa Papa juu ya uundaji wa vikundi vya mafunzo vitaratibiwa na Sekretarieti Kuu inayoshirikisha mabaraza yenye uwezo.Kikao cha pili cha Sinodi kitafanyika kuanzia tarehe 2 hadi 27 Oktoba 2024 na kitatanguliwa na siku mbili za mafungo (30 Septemba-1 Oktoba).

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Sekretarieti kuu ya Sinodi imetaarifu kwamba Baba Mtakatifu Francisko ameweka tarehe za kikao cha pili cha Mkutano Mkuu wa XVI utakaofanyika kuanzia Jumatano tarehe 2 Oktoba hadi Dominika  tarehe 27 Oktoba 2024, ili kuendeleza kazi ya Sinodi ya Kisinodi yenye kauli mbiu: “Kwa ajili ya Kanisa la Sinodi:ushirika, ushiriki na utume.” Kikao hiki cha pili, kama kilivyofanyika tayari mnamo Oktoba 2023, pia kitatanguliwa na siku mbili za mafungo ya kiroho, kuanzia tarehe 30 Septemba hadi 1 Oktoba (na washiriki watawasili tarehe 29 Septemba 2024). Wakati huo huo kama taarifa hiyo, iyoandikwa kwa mkono (chirograph) kutoka kwa Papa pia ilichapishwa, ambayo itaanzisha vikundi vya mafunzo ili kuzama zaidi katika baadhi ya mada zilizoibuka katika kipindi kilichopita. Vitaanzishwa vikundi kati ya Mabaraza ya Kipapa ya Curia Romana vyene uwezo  na Sekretarieti Kuu ya Sinodi, ambayo itaratibu.

Papa anataja Hati ya Mtaguso ya Lumen Gentium

Katika barua ya mkono wake (chirograph), iliyowekwa kwa ushirikiano kati ya mabaraza ya Curia na Sekretarieti ya Sinodi, Papa Francisko anataja katiba ya Mtaguso wa Vatican, ya  hati ya Lumen Gentium ili kukumbuka kwamba Kanisa linaonesha uwepo wake, “katika Kristo, kwa njia fulani sakramenti, ambayo ni ishara na chombo cha 'muungano wa karibu sana na Mungu na umoja wa jamii nzima ya binadamu' na kwamba “inajidhihirisha kwa uwazi zaidi na uaminifu kwa ulimwengu katika tamaduni mbalimbali kama fumbo la ushirika wa kimisionari, Mwili mmoja, unaoshiriki katika Roho wake anayeufanya upya na kuuongoza katika kutangaza Injili kwa watu wote.” Katika mwanga huu, katika katiba Mpya ya  Curia Romana ya  Praedicate Evangelium, tunasoma kwamba “maisha ya ushirika hulipatia Kanisa sura ya kisinodi. Hasa kusikiliza kwa pande zote na nguvu ya usawa katika kujiweka katika huduma ya utume wa watu wa Mungu kuhitimu kazi ya usaidizi wa Curia Romana kwa huduma ya Askofu wa Roma, ya mtu binafsi, maaskofu na Baraza la  maaskofu. Ustadi wa kichungaji unaoutekeleza hupata madhumuni na ufanisi wao katika huduma ya ushirika wa kiaskofu na ushirika wa kikanisa katika muungano na chini ya uongozi wa Askofu wa Roma.

Mabaraza ya Curia Romana na ushirikiano na Sekretarieti kuu ya Sinodi

Ni kwa mantiki hiyo ndipo jukumu la Sekretarieti Kuu ya Sinodi linawekwa, ambalo linamtegemea Papa moja kwa moja na ambalo “linaunga mkono na kuambatana na mchakato wa sinodi ulioanzishwa mara kwa mara, kukuza kwa moyo wa sinodi mahusiano ya maaskofu na Makanisa hasa kati yao na katika ushirika na Askofu wa Roma. Maandishi ya Mkono wake Papa (Chirograph) yanahitimisha kwa kusema kwamba “ Mabaraza ya Curia Romana hushirikiana, kulingana na uwezo wao maalum, katika shughuli ya Sekretarieti Kuu ya Sinodi, kuanzisha vikundi vya mafunzo ambavyo vinaanza, kwa njia ya sinodi, uchambuzi wa kina wa baadhi ya mada zilizojitokeza” katika kikao cha kwanza cha Sinodi ya Maaskofu. Vikundi hivi vya mafunzo vinapaswa kuanzishwa kwa makubaliano ya pande zote kati ya Mabaraza ya Curia Romana yanayofaa na Sekretarieti Kuu ya Sinodi, ambayo uratibu umekabidhiwa.”

Hati ya maandalizi ya Sinodi Oktoba 2024

Tayari katika hati ya maandalizi ya “Kuelekea Oktoba 2024” ya Sekretarieti Kuu ya Sinodi, iliyochapishwa  mnamo tarehe 11 Desemba 2023, ilisisitizwa jinsi mkutano ujao ungezingatia mada ya ushiriki, kuhusiana na utekelezaji wa mamlaka, kama usemi wa ushirika katika huduma ya utume. Kwa hiyo  yangechunguza jinsi ya kuishi sinodi katika ngazi zote za Kanisa. Sasa uamuzi wa Papa unaweka wazi kwamba baadhi ya dhamira muhimu zaidi zilizoibuka kutokana na kusikiliza Makanisa zinahitaji muda mwingi kwa ajili ya mafunzo ya kitaalimungu, kanuni na kichungaji kadiri ya utaratibu wa sinodi inayohusisha wataalam kutoka mabara yote na mbaraza ya Curia  Roman kulingana na uwezo wao.

Maandishi ya Papa kwa mkono ni nyenzo kwa kutafakari Kanisa zima

Kwa hiyo kwa sasa, inafafanuliwa ni vikundi vipi vya mafunzo  vya kuanzisha na juu ya mada gani. Ripoti ya muhtasari iliyopigiwa kura mwishoni mwa kikao cha Oktoba mwaka 2023 ilionesha baadhi yake, kama vile kusasishwa kwa baadhi ya kanuni za kanuni, mafunzo ya wahudumu waliowekwa wakfu, mahusiano kati ya maaskofu na viongozi wa kidini, utafiti wa kitaalimungu na kichungaji kuhusu ushemasi. Michango ya vikundi vya mafunzo, kama inavyoweza kuonekana kutoka kwa hati ya Sekretarieti Kuu iliyochapishwa mnamo Desemba na kutoka katika maandishi  (chirograph) ya tarehe 17 Februari  2024 ya Papa, itakuwa nyenzo muhimu kwa kutafakari kwa Kanisa zima lakini haitajumuisha moja kwa moja suala la majadiliano na utambuzi wa Kanisa, kikao kijacho cha Sinodi, ambacho kitazingatia - kama ilivyosemwa tayari - juu ya sinodi kama hivyo, usemi wa ushirika katika maisha ya kikanisa. Hatimaye, inapendeza kuona jukumu lililokabidhiwa kwa Sekretarieti Kuu ya Sinodi inayoongozwa na Kardinali Mario Grech, ambaye ataratibu kazi na mabaraza. Kiungo ambacho si sehemu ya Curia Romana, lakini pia iko chini ya Papa moja kwa moja.

Papa ametua Washauri wapya 6 wa Sekretarieti ya Sinodi

Jumamosi 17 Februari 2024, Papa Francisko amewateua washauri wapya 6 kwenye Sekretarieti Kuu ya Sinodi, pamoja na kumi ya sasa. Washauri wapya ni: Askofu Alphonse Borras, wa Jimbo la Liège (Ubelgiji); Gilles Routhier, profesa wa Taalimungu katika Chuo Kikuu cha Laval (Canada); Ormond Rush, profesa mshiriki wa Taalimungu katika Chuo Kikuu katoliki cha Australia; Sr. Birgit Weiler, M.M.S., profesa wa Taalimungu katika Chuo Kiukuu cha Kipapa,  Perú; Profesa Tricia C. Bruce, rais mteule wa Chama cha Sosholojia ya Dini, na Maria Clara Lucchetti Bingemer, profesa wa Taalimungu katika Chuo Kikuu katoliki cha Kipapa cha Rio de Janeiro,Brazil.

Barua ya Papa kuhusiana na Sinodi 2-27.10. 2024
17 February 2024, 17:55