Tafuta

2024.02.01 Uwakilishi wa Chuo Kikuu cha  Notre Dame" Marekani. 2024.02.01 Uwakilishi wa Chuo Kikuu cha Notre Dame" Marekani.  (Vatican Media)

Papa:Dini ni muhimu zinasaidia kujenga ulimwengu uwe bora

Papa akikutana na rais na bodi ya wadhamini wa Chuo Kikuu Katoliki cha Notre Dame,cha huko Indiana,Marekani amewakumbusha juu ya lugha tatu za:kichwa,moyo na mikono ili kutekeleza utume wao.Amehimiza juhudi za kuhamasisha miongoni mwa wanafunzi kujitolea katika mshikamano na mahitaji ya jamii zilizo katika hali mbaya zaidi.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 1 Februari 2024 amekutana na kuwakaribisha kwa moyo mkunjufu, Padre John Jenkins Rais na  wajumbe wa Bodi ya  Wadhamini wa Chuo Kikuu Katoliki  cha Notre Dame na kwa maafisa wa Chuo Kikuu, Kutoka Indiana nchini Marekani. Papa amesema kwamba tangu.  Kuanzisha kwa  Chuo Kikuu cha Notre Dame kimejitolea kuendeleza utume wa Kanisa wa kutangaza Injili kwa njia ya malezi ya kila mtu katika vipimo vyake vyote. Hakika, kama Mwenyeheri Basil Moreau alivyosema, kuwa: “Elimu ya Kikristo ni sanaa ya kuwasaidia vijana kufikia ukamilifu.” Katika suala hili,Papa Francisko amependa kutoa natatafakari kwa ufupi juu ya ‘lugha’ tatu, kama ilivyo: zile za kichwa, moyo na mikono. Kwa pamoja, vinatoa upeo ambao jumuiya za wasomi wa Kikatoliki zinaweza kujitahidi kuunda viongozi imara na waliounganishwa vyema ambao maono yao ya maisha yanahuishwa na mafundisho ya Kristo.

Wawakilishi kutoka Chuo Kikuu Katoliki cha Notre Dame, Marekani
Wawakilishi kutoka Chuo Kikuu Katoliki cha Notre Dame, Marekani

Baba Mtakatifu akianza la kwanza, kichwa. Kwa asili yake, vyuo vikuu vya Kikatoliki vimejitolea kutafuta maendeleo ya ujuzi kupitia masomo ya kitaaluma na utafiti. Katika dunia ya leo ya utandawazi, hii itahusisha mbinu ya ushirikiano na ya kinidhamu, kuunganisha nyanja mbalimbali za usomi na uchunguzi. Kwa hakika, juhudi hizi za kielimu zinazofanywa na taasisi za Kikatoliki zimejikita katika usadikisho thabiti wa maelewano ya ndani ya imani na akili, ambayo kwayo hutiririka umuhimu wa ujumbe wa Kikristo katika nyanja zote za maisha ya kibinafsi na ya kijamii. Kwa hiyo, waelimishaji na wanafunzi kwa pamoja wanaitwa kuthamini Zaidi, si tu thamani ya kujifunza kwa ujumla, bali pia utajiri wa mapokeo ya kiakili ya Kikatoliki hasa.

Kazi ya chuo kikuu cha Kikatoliki, hata hivyo, si tu kupanua akili, katika kichwa; ni lazima kupanua pia moyo. Jumuiya nzima ya chuo kikuu inaitwa kusindikizana na wengine, hasa vijana, kwa hekima na heshima katika njia za maisha na kuwasaidia kukuza uwazi kwa yote ambayo ni kweli, mema na mazuri. Hii inahusisha uanzishaji wa mahusiano ya kweli kati ya waelimishaji na wanafunzi ili waweze kutembea pamoja na kuelewa maswali, mahitaji na ndoto za ndani kabisa zinazopatikana katika maisha ya mwanadamu.

Papa Francisko akihutubia uwakilishi wa Chuo Kikuu Katoliki  cha Notre Dame, Marekani
Papa Francisko akihutubia uwakilishi wa Chuo Kikuu Katoliki cha Notre Dame, Marekani

 

Baba Mtakatifu anabainisha kuwa inamaanisha pia kukuza mazungumzo na utamaduni wa kukutana, ili wote waweze kujifunza kukiri, kuthamini na kumpenda kila mtu kama kaka au dada, na kimsingi zaidi, kama mtoto mpendwa wa Mungu. Hapa, hatuwezi kupuuza jukumu muhimu la dini katika kuelimisha mioyo ya watu. Kwa hiyo, nina furaha kwamba Chuo Kikuu cha Notre Dame kina alama ya mazingira ambayo yanawawezesha wanafunzi, kitivo na wafanyakazi kukua kiroho na kushuhudia furaha ya Injili, uwezo wake wa kufanya upya jamii na uwezo wake wa kutoa matumaini na nguvu katika kukabiliana na changamoto za wakati huu kwa busara.

Hatimaye, ni mikono.  Baba Mtakatifu Francisko katika kipengele hiki amesema kuwa Elimu ya Kikatoliki inatuweka pamoja na mambo mengine katika ujenzi wa ulimwengu bora kwa kufundisha kuishi pamoja, mshikamano wa kidugu na amani. Hatuwezi kukaa ndani ya kuta au mipaka ya taasisi zetu, lakini lazima tujitahidi kwenda pembezoni na kukutana na kumtumikia Kristo katika jirani yetu. Katika suala hili, ninahimiza juhudi zinazoendelea za Chuo Kikuu cha kukuza katika wanafunzi wake ari ya kukidhi mahitaji ya jamii zisizo na uwezo. Kwa hiyo Papa Francisko ametoa shukrani zake  kwa huduma yao ya  ukarimu katika kusaidia Notre Dame kubaki mwaminifu kwa tabia na utambulisho wake wa kipekee kama taasisi ya Kikatoliki ya elimu ya juu.

Vile vile ni matumaini yake kwamba michango yao katika maisha ya taasisi hiyo itaendelea kuimarisha urithi wake wa elimu dhabiti ya Kikatoliki na kuwezesha Chuo Kikuu kuwa, kama mwanzilishi wao Padre Edward Sorin alivyotamani “njia yenye nguvu kwa ajili ya wema” katika jamii. Baba Mtakatifu Francisko amewashukuru kwa mara nyingine kwa ziara yao. Akiipongeza jumuiya nzima ya Notre Dame na wote wanaounga mkono utume wao kwa maombezi ya Mama Yetu, anawaombea wao na familia zao zawadi za Bwana za hekima, furaha na amani, na amewapatia baraka zake  kwa moyo mkunjufu. Na kuwaomba, tafadhali, wakumbuke kumuombea.

Papa na wawakilishi wa Chuo Kikuu cha Notre Dame, Marekani
01 February 2024, 16:52