Watu zaidi ya 10 wamefariki dunia kutokana na ajali ya moto ambayo imeteketeza nyumba yenye ghorofa 14, iliyokuwa inakaliwa na watu zaidi 350 kwenye vyumba 140 huko mjini Valencia, nchini Hispania. Watu zaidi ya 10 wamefariki dunia kutokana na ajali ya moto ambayo imeteketeza nyumba yenye ghorofa 14, iliyokuwa inakaliwa na watu zaidi 350 kwenye vyumba 140 huko mjini Valencia, nchini Hispania.  (ANSA)

Ajali ya Moto Valencia: Ghorofa 14 Zateketea, 5 Wafariki Dunia, 20 Hawajulikani Mahali Walipo!

Tarehe 22 Februari 2024, watu zaidi ya 10 wamefariki dunia kutokana na ajali ya moto ambao umeteketeza nyumba yenye ghorofa 14, iliyokuwa inakaliwa na watu zaidi 350 kwenye vyumba 140 huko mjini Valencia, nchini Hispnia. Majeruhi 15 walipata matibabu na kuruhusiwa kuendelea na shughuli zao, lakini taarifa zinaonesha kwamba, kuna zaidi ya watu 20 hawajulikani walipo; hao wanahofiwa kuwa waliteketea kwa moto. Uchunguzi wa vifaa vya ujenzi unaendelea!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., Vatican.

Alhamisi jioni, tarehe 22 Februari 2024, watu zaidi ya 10 wamefariki dunia kutokana na ajali ya moto ambao umeteketeza nyumba yenye ghorofa 14, iliyokuwa inakaliwa na watu zaidi 350 kwenye vyumba 140 huko mjini Valencia, nchini Hispnia. Majeruhi 15 walipata matibabu na kuruhusiwa kuendelea na shughuli zao, lakini taarifa zinaonesha kwamba, kuna zaidi ya watu 20 hawajulikani walipo; hao wanahofiwa kuwa waliteketea kwa moto. Uchunguzi wa vifaa vilivyotumika kwenye ujenzi unaendelea. Ni katika muktadha huu, Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa Askofu mkuu Enrique Benavent Vidal wa Jimbo kuu la Valencia, ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican anasema, anafuatilia kwa karibu taarifa za ajli ya moto iliyotokea huko Campanar na kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao.

Ajali ya Moto Jijini Valencia, Hispania: watu zaidi ya 10 Wamefariki Dunia
Ajali ya Moto Jijini Valencia, Hispania: watu zaidi ya 10 Wamefariki Dunia

Baba Mtakatifu amewakabidhi watu wote waliopoteza maisha kutokana na ajali hii kwa huruma ya Mungu na anapenda kuwahakikishia watu wote wa Mungu mjini Valencia uwepo wake wa karibu kwa sala na sadaka yake, na hasa zaidi, wale wote waliokumbwa na kutikiswa na ajali hii mbaya. Baba Mtakatifu anapenda kuwakabidhi wote hawa chini ya ulinzi, tunza na maombezi ya Bikira Maria wa mshikamano na ya Mtakatifu Yosefu. Mwishoni amewapatia baraka zake za kitume kama zawadi ya matumaini kwa Kristo Yesu Mfufuka.

Maafa Valencia
24 February 2024, 14:18