Baba Mtakatifu Francisko amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Prof. Antonio Paolucci aliyewahi kuwa ni Mkurugenzi mkuu wa Makumbusho na Urithi wa Utamaduni wa Vatican. Baba Mtakatifu Francisko amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Prof. Antonio Paolucci aliyewahi kuwa ni Mkurugenzi mkuu wa Makumbusho na Urithi wa Utamaduni wa Vatican. 

Papa Francisko Asikitishwa na Kifo cha Prof. Antonio Paolucci: Makumbusho ya Vatican

Prof. Antonio Paolucci amefariki dunia, tarehe 4 Februari 2024, huko Florence, akiwa na umri wa miaka 84. Katika salam za rambirambi zilizoandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican kwenda kwa Dr. Fabrizio Paolucci, anapenda kuonesha uwepo wake wa karibu kwa njia ya sala, kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote. Baba Mtakatifu anamkumbuka Prof. Antonio Paolucci kwa ukarimu, sadaka, majitoleo na huduma yake kwa Vatican.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Prof. Antonio Paolucci aliyewahi kuwa ni Mkurugenzi mkuu wa Makumbusho na Urithi wa Utamaduni wa Vatican, kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka 2016. Prof. Antonio Paolucci amefariki dunia, Dominika tarehe 4 Februari 2024, huko Florence, akiwa na umri wa miaka 84. Katika salam za rambirambi zilizoandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican kwenda kwa Dr. Fabrizio Paolucci, anapenda kuonesha uwepo wake wa karibu kwa njia ya sala, kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote. Baba Mtakatifu anamkumbuka Prof. Antonio Paolucci kwa ukarimu, sadaka, majitoleo na huduma yake kwa Vatican kama Mwanahistoria wa Sanaa na Mkurugenzi wa zamani wa Makumbusho na Urithi wa Utamaduni wa Vatican.

Prof. Antonio Paolucci akizungumza na Papa Francisko
Prof. Antonio Paolucci akizungumza na Papa Francisko

Baba Mtakatifu anapenda kutolea sala na sadaka yake kwa ajili ya roho ya Marehemu Prof. Antonio Paolucci, ili aweze kupumzika kwa amani. Baba Mtakatifu amewapatia baraka ya kitume wale wote wanaomboleza kwa msiba huu mkubwa. Kardinali Pietro Parolin naye anapenda kuungana na wale wote wanaoomboleza kwa msiba huu mzito. Naye Barbara Jatta, Mkurugenzi mkuu wa Makumbusho na Urithi wa Utamaduni wa Vatican anasikitika kusema kwamba, amefariki Mwanahistoria wa Sanaa, aliyekuwa na ufahamu mpana sana wa uzuri wa sanaa, akabahatika kuwa na kipaji cha kuwafafanulia watu, kiasi kwamba walijisikia kuwa ni sehemu ya tukio lenyewe. Ni kiongozi aliyekazia ukarabati wa Makumbusho ya Vatican, ili kulinda na kutunza urithi na amana ya wengi. Aliipenda sana Sanaa, uzuri wake pamoja na amana na urithi wa Kitamaduni.

Rambirambi
06 February 2024, 14:41