Papa Francisko atatembelea Venezia mwishoni mwa Aprili 2024
Vatican News
Atakuwa ni Papa wa nne kutua kati ya mifereji na mitaa ya Venezia, nchini Italia. Baada ya Papa Paulo VI mnamo mwaka 1972, Yohane Paulo II mnamo mwaka 1985 na Papa Benedikto XVI mnamo mwaka 2011, itakuwa sasa ni zamu ya Papa Francisko kutembelea Mji wa Venezia, Dominika tarehe 28 Aprili 2024 ambapo itakuwa ni siku tatu baada ya sikukuu ya Mtakatifu Marko Msimamizi wa Mji huo.
Baadhi ya hatua za ziara hiyo
Katika taarifa ya pamoja kutoka Baraza la Utamaduni na Elimu na Upatriaki wa Venezia unabainisha juu ya “matukio ambayo yatakuwa na sifa ya ziara ya upapa kwamba yanatangazwa. Hata hivyo kutakuwa na kituo katika Banda la Vatican kwenye Maonyesho ya 60 ya Kimataifa ya Sanaa ya Biennale, kwenye gereza la wanawake la Giudecca, na mkutano na jumuiya ya kikanisa ya Upatriaki. Ratiba nzima ya uhakika, itawasilishwa hivi karibuni.”