2024.02.17 Papa amakutana na wajumbe wa Bondo ya ujenzi wa Basilika ya Familia Takatifu ya Barcellona 2024.02.17 Papa amakutana na wajumbe wa Bondo ya ujenzi wa Basilika ya Familia Takatifu ya Barcellona   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa:Katika Basilika ya Familia Takatifu wanahija wapokelewe kwa sala!

Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake mjini Vatican kwa lugha ya kihisipania kwa wajumbe wa Bodi ya Ujenzi wa Basilika ya Familia Takatifu ya Barcelona nchini Hispania ya Jumamosi tarehe 17 Februari 2024,amesisitizia juu ya mada kuu ya sala katika Mwaka Sala kuelekea Jubilei ya 2025.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika hotuba ya Baba Mtakatifu alipoktana mjinimVatican Jumamosi tarehe 17 Februari 2024  na Wawakilishi wa Bodi ya Ujenzi ya Kanisa kuu la Familia Takatifu ya mji wa  Barcelona nchini Hispania amefurahi kukutana nao  wakiwa na familia zao ambapo amesema kama alivyorudia mara nyingi katika fursa ya mwaka wa sala wa kujiandalia Mwaka wa Jubilei 2025 kuwa mwaka mzima ni katika maombi kwa ajili ya hiyo. Ni muhimu kwamba hali halisi ya maombi isipotee kwenye mahekalu, lazima iwe moja ya vipaumbele kwa wale, kama wao, ambao wamepokea jukumu la kutunza mahekalu.

Papa amekutana na wajumbe wa Bodi ya Ujezi wa Basilika ya Familia Takatifu Barcelona
Papa amekutana na wajumbe wa Bodi ya Ujezi wa Basilika ya Familia Takatifu Barcelona

Kwa hakika Papa amesema wao wameona kwamba Basilika ya Familia ya Sagrada imeundwa ili kila ukumbi uwe na mada, inayooneshwa na vifungu vya Maandiko na kuandaliwa kwa maombi. Hivyo mlango wa kwanza, ni ule wa imani, nyuma ya sura ya Yesu akiwahubiria madaktari, unatuonesha Utatu Mtakatifu. Imani inayohubiriwa lazima iwe maombi. Kila mara.

Wajumbe wa Bondi ya Ujenzi wa Basilika ya Familia Takatifu Barcellona
Wajumbe wa Bondi ya Ujenzi wa Basilika ya Familia Takatifu Barcellona

Mlango wa kati wa upendo, ambao sura yake kuu hasa ni ile ya Familia Takatifu, inatualika kuinua mitazamo yetu kuelekea fumbo la Umwilisho na kutoka hapo tuchambue shanga za rozari inayoshuka kando ya madirisha, tukitengeneza nyota ya Bethlehemu, karibu kama kusema: “hapa kuna nuru yetu.” Na ni hasa katika kuabudu, katika sala ya kutafakari ya mafumbo, kwamba tunajifungua wenyewe katika mwanga huo, kama dirisha kubwa la hekalu lao.

Ndani ya Basilika ya Familia Takatifu Barcellona
Ndani ya Basilika ya Familia Takatifu Barcellona

Kwa hivyo Baba Mtakatifu Francisko amewaalika kuwakaribisha mahujaji wanaokaribia kwenye Basilika, ili kuwatambulisha kwa mtazamo wa sala kutafakari mpango wa picha ya mtumishi wa Mungu Antoni Gaudí katika ukamilifu, ili kwamba kama vile vilele na minara ya kengele, mitazamo yao iinuliwe juu na sauti zao zitangaze pamoja na Malaika: “Mtakatifu, Mungu wetu hafi.” Asante kwa kila kitu unachofanya, asante. Mungu awabariki.

Uzuri wa Basilika ya Familia Takatifu, Barcellona
Uzuri wa Basilika ya Familia Takatifu, Barcellona
Papa kwa wajumbe wa Bodi ya Ujenzi wa Basilika ya Familia Takatifu
17 February 2024, 15:18