Tafuta

Papa Francisko ahimiza ukaribu kama ishara thabiti kwa wadhaifu

Papa kabla ya sala ya Malaika wa Bwana,Dominika 11 Februari amejikita kuelezea matendo ya Yesu katika Injili:huinama,huwashika mkono na kuwaponya wanaoteseka.Mawazo yake ni kwa ulimwengu unaotawaliwa na uhusiano unaopotea,wakati upendo unahitaji uwepo,kujitoa kwani selfies au ujumbe wa haraka havitoshi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican kwa ajili ya kumtangaza Mtakatifu María Antonia wa Mtakatifu Yosefu, "Mama Antula", wa Nchini Argentina, Dominika tarehe 11 Februari 2024, Baba Mtakatifu kupitia dirisha la Jumba la Kitume mjini Vatican ametoa tafakari yake kwa kujikita na Injili ya siku. Papa amesema: “Injili ya leo inawakilishwa uponeshwa wa mkoma(Mc 1,40-45). Kwa mgonjwa aliyeomba Yesu anajibu: Ndiyo ninataka takasika(Mk 1,41). Anatamka sentesi moja rahisi ambayo inawekwa haraka katika matendo. Kiukweli mara moja ukoma ulotoweka na akapona (Mk 1,42) Na tazama mtindo wa Yesu kwa anayeteseka. Maneno machache na matendo ya dhati.

Papa wakati wa Angelusi 11 Februari 2024
Papa wakati wa Angelusi 11 Februari 2024

Baba Mtakatifu amesema kuwa mara nyingi katika Injili, tunaona tabia yake kwa anayeteseka kama vile kipofu(Mk 7,31-37), kiwete (Mk 2,1-12) na wengine wengi wahitaji (Mk 5). Daima anafanya hivyo: anaongea kidogo na mara moja hufuata maneno yake kwa vitendo: anainama, anamshika mkono, anaponya. Hakalii kwenye hotuba au maswali, utauwa na hisia. Badala yake Yeye anaonesha unyeti wa anayesikiliza kwa makini, hutenda mara moja, ikiwezekana bila kuvutia umakini. Ni njia ya ajabu ya kupenda na jinsi gani inakuwa vizuri kuifikiria na kujifananisha nayo! Tufikirie hata wakati inapotokea kukutana na watu ambao wana tabia hivyo: Maneno kiasi, lakini kwa matendo ya ukarimu; kusitasita kujionesha, lakini wako tayari kujifanya kuwa muhimu; ufanisi katika kusaidia kwa sababu wako tayari kusikiliza.

Sala ya malika wa Bwana 11 Februari 2024
Sala ya malika wa Bwana 11 Februari 2024

Baba Mtakatifu akiendelea amesema inawezakana kujiuliza: Unataka kunisaidia? Kwa kusikia anajibu karibu na maneno ya Yesu: 'Ndiyo ninataka, niko hapa kwa ajili yako!' Uthabiti huu ni muhimu katika dunia kama ilivyo. Na badala yake tusikilize jinsi Neno la Mungu linavyotuchokoza: “Ikiwa ndugu au dada yu uchi na kukosa chakula cha kila siku, na mmoja wenu akawaambia: “Nendeni kwa amani, mkaote moto na kushiba,” lakini msiwapatie yafaa nini kwa mwili? ( Yak 2:15-16 ). Alisema hayo Yakobo. Upendo unahitaji uthabiti, uwepo, mkutano, wakati na nafasi iliyotolewa: haiwezi kupunguzwa kuwa maneno mazuri, picha kwenye skrini, selfies ya muda mfupi au ujumbe wa haraka. Ni zana muhimu, lakini havitoshi kwa upendo, haviwezi kuchukua nafasi ya uwepo halisi.

Hata uwepo wa mvua haukuzuia watu katika sala ya Malaika wa Bwana
Hata uwepo wa mvua haukuzuia watu katika sala ya Malaika wa Bwana

Kwa hiyo Papa Francisko amesema tujiulize: "je, ninajua jinsi ya kuwasikiliza watu, je, ninapatikana kwa maombi yao mazuri? Au ninatoa visingizio, kuahirisha mambo, kujificha nyuma ya maneno ya kufikirika na yasiyo na maana? Kwa hakika ni lini mara ya mwisho nilipokwenda kumtembelea mtu mpweke au mgonjwa, au kwamba nilibadilisha mipango yangu ili kukidhi mahitaji ya wale walioniomba msaada? Mama Maria kwa haraka katika kujali, atusaidie kuwa tayari na thabiti katika upendo." Amehitimisha Baba Mtakatifu.

Tafakari ya Papa kwa Angelus
11 February 2024, 12:56