Papa:Kanisa la Kisinodi ni uwanja wa Ujenzi unaoendelea kwa makuhani na walei
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican na Jumuiya ya Seminari za Jimbo Kuu la Napoli, Italia na wanajumuiya wengine tarehe 16 Februari 2024. Katika hotuba yake aliyowakabidi wajisomee,Papa anaanza kuwashukuru kufika kwao asubuhi hiyo kukutana naye katika fursa ya kuadhimisha miaka 90 tangu kuanzishwa kwa Seminari yao ya “Alessio Ascalesi.” Amemshukuru Askofu Mkuu,Domenico Battaglia,wa Jimbo Kuu Katoliki la Napoli,ndugu Maaskofu,Mkuu wa Shule, Waelimishaji na Mababa wa Kiroho na kuwashukuru kila mtu kwa huduma yao ya thamani. Amewasalimia kwa furaha wale wote ambao,kwa njia tofauti,wanachangia malezi yao kuanzia na Watawa,Mkuu wa Kitivo,Masista na pia wanandoa,ambao uwepo wao amesema ni ishara muhimu,inayotukumbusha ukamilishano kati ya Daraja Takatifu na Sakramenti ya Ndoa:“katika malezi ya kipadre tunahitaji mchango wao ambao walichagua njia ya ndoa.” Na kuwashukuru kwa kile ambacho wanafafanya.
Baba Mtakatifu lakini pia hata shukrani kwa washauri wa kisaikolojia,wafanyakazi wa utawala na huduma. Baba Mtakatifu Francisko amewageukia waseminari kwamba amehisi ulazima wa kutoa shukrani kwao kwa kuitikia wito wa Bwana na kwa utayari wao wa kutumikia Kanisa lake;na kukuhimiza kukuza uzuri wa uaminifu kila siku,kwa shauku na kujitolea,kukabidhi maisha yao kwa kazi isiyokoma ya Roho Mtakatifu,anayewasaidia kuchukua mtindo wa Kristo. Baba Mtakatifu katika hotuba hiyo amewaomba wakumbuke hili kwamba kwa sababu mafunzo hayana mwisho,hudumu katika maisha yote. Baba Mtakatifu kwa kufikiria tu kuhusu kazi hiyo “ya ndani inayoendelea ambayo ni malezi ya kipadre na ukumbusho wa Seminari yao uwanja wa ujenzi umemjia akilini.
Kanisa kwanza kabisa ni uwanja wa ujenzi uliyo wazi kila wakati. Hili ni,na linabaki daima katika harakati,wazi kwa upya wa Roho,kushinda jaribu la kujihifadhi lenyenyewe na maslahi yake. Kazi kuu ya uwanja wa ujenzi wa Kanisa ni kutembea pamoja na Msalaba,wa aliyefufuka,kuleta uzuri wa Injili yake kwa wanadamu. Hili ndilo jambo la muhimu. Hivi ndivyo njia ya kisinodi inatufundisha,ndivyo jinsi ya kumsikiliza Roho na wanadamu wa wakati wetu hutuomba,si bila maelewano;bali pia ndilo linaloombwa kwao:kuwa watumishi. Na hii ni maana ya wahudumu ambao wanajua kuchukua mtindo wa utambuzi wa kichungaji katika kila hali,kwakujua kwamba sisi “sote,makuhani na walei,tuko njiani kuelekea utimilifu na ni wafanyakazi kwenye ujenzi wa kiwanja cha ujenzi. Hatuwezi kutoa majibu ya pekee na yaliyotengenezwa na kupakuliwa awali kiukweli wa changamato za leo hii,lakini ni lazima tuwekeze nguvu zetu katika kutangaza umuhimu,ambao ni huruma ya Mungu na kuidhihirisha kupitia ukaribu,ubaba,upole na kusafisha sanaa ya utambuzi.
Kwa sababu hiyo,hata njia ya malezi kwa ukuhani ni mahali pa ujenzi,Papa amesisitiza. Hatupaswi kamwe kufanya makosa ya kujiona tumefika,kujiona tayari kwa changamoto. Mazoezi ya ukuhani ni mahali pa ujenzi ambapo kila mmoja wao ameitwa kujihusisha katika kweli,kumwacha Mungu ajenge kazi yake kwa miaka mingi. Kwa hiyo Papa amesema wao wasiogope kuruhusu Bwana atende maishani mwao;kama kwenye eneo la ujenzi Roho atakuja kwanza kubomoa vipengele hivyo,imani hizo,mtindo huo na hata yale mawazo yasiyolingana kuhusu imani na huduma ambayo yanawazuia kukua kulingana na Injili;basi Roho huyo huyo,baada ya kuusafisha uwongo wa ndani,atawapa moyo mpya,atayajenga maisha yao sawasawa na mtindo wa Yesu,atawafanya kuwa viumbe wapya na wanafunzi wa kimisionari. Atawafanya shauku yao kukomaa kupitia msalaba,kama ilivyokuwa kwa Mitume.
Papa ameongeza kuwa lakini wasiogope hii:kwa hakika inaweza kuwa kazi ya kuchosha,lakini ikiwa wataendelea kuwa watulivu na wa kweli,waliotayari kwa utendaji wa Roho bila kipingamizi na kujitetea,watagundua huruma ya Bwana ndani ya udhaifu wao na ndani yao furaha safi ya utumishi. Katika uwanja wa ujenzi ambao ni malezi yao,kwa hiyo wachimbe kwa undani,‘kufanya ukweli’ndani yao kwa uaminifu,kukuza maisha ya ndani,kutafakari Neno,kusoma masuala ya wakati wetu na masuala ya kitaalimungu na kichungaji kwa kina. Na katika kufanya hivyo Papa Francisko ameomba ruhusa ya kupendekeza jambo moja kwao kwamba wafanye kazi juu ya ukomavu wa kihemko na wa kibinadamu. Bila hivyo hawawezi kwenda popote!
Hatimaye,muundo wa Seminari yenyewe ni kama uwanja mkubwa wa ujenzi. Na ni wazi kwamba hazungumzii sekta ya ujenzi. Kuhusu mafunzo ya ukuhani,mchakato unaendelea unaojumuisha masuala mapya muhimu sana:ratiba za mafunzo yanapitia mabadiliko mengi,kusikiliza changamoto zinazosubiri huduma ya ukuhani na zinahitaji kujitolea,shauku na ubunifu mzuri kutoka kwa kila mtu. Baba Mtakatifu katika hotuba hiyo anabinisha kuwa uzoefu mpya wa kichungaji na wa kimisionari unajaribiwa,kwa lengo la kuhimiza kuingizwa taratibu katika maisha ya kihuduma ya siku zijazo;Nyakati za kukatizwa katika mchakato zinabuniwa ili kuhimiza ukomavu wa mtu binafsi. Ni jambo zuri kukaribisha na kutathmini maendeleo haya mapya,tukiyapitia kama fursa za neema na huduma na tukitambua uwepo wa Mungu ndani yake.
Papa Francisko anakazia kusema kuwa:“Tumeanza muda mfupi mchakato wa safari ya Kwaresima ambayo,kama nilivyosema ni wakati wa maamuzi madogo na makubwa dhidi ya kwenda kinyume na[...] ambamo kutafakari upya mitindo ya maisha(Ujumbe wa Kwaresima 2024).” Kwa njia hiyo Papa ameomba kwamba Jumuiya yao pia inaweza kufuata njia hii ya uongofu na kujipyaisha. “Je kwa namna gani? Tukijiruhusu tushindwe kwa mshangao upya wa upendo wa Mungu,msingi wa wito unaokaribishwa na kugunduliwa tena hasa katika kuabudu na kuwasiliana na Neno;kwa furaha ya kugundua tena ladha ya kiasi na kuepuka upotevu; kujifunza mtindo wa maisha” ambao utawasaidia“kuwa makuhani wenye uwezo wa kujitoa kwa wengine na kuwa makini kwa maskini zaidi;”wasijiruhusu kudanganywa na ibada ya sura na kuonekana,lakini kutunza maisha yao ya ndani;kutunza haki na kazi ya uumbaji, masuala ya sasa na ya motomoto katika nchi yao,ambayo kwa maana hiyo inasubiri maneno ya ujasiri na ishara za kinabii kutoka kwa Kanisa; kuishi kwa amani na maelewano,kushinda migawanyiko na kujifunza kuishi udugu kwa unyenyekevu. Na udugu ni hasa leo,mojawapo ya shuhuda kuu tunazoweza kutoa kwa ulimwengu.
Baba Mtakatifu aidha amekazia kuwa kazi inayoendelea ya eneo lao la ujenzi iambatane na maombezi ya watakatifu:na Mlinzi wao Mtakatifu Gennaro ambaye uwepo wake na damu yake inaendelea kumwagilia katika ardhi wanayoishi na Mtakatifu Vincenzo Romano,paroko wa parokia aliyefundwa katika Seminari yao,mfano wa ari ya kitume na roho ya kimisionari na kwa Mwenyeheri Mariano Arciero,ambaye alikuwa baba yao wa kiroho,ambaye kumbukumbu yake ya kiliturujia inafanyika kila tarehe 16 Februari ya kila mwaka. Papa kwa kuhitimisha amewatakia kila la kheri katika safari yao na na kwamba anawasindikiza katika maombi. Nao pia tafadhali wasisahau kumuombea.