Tafuta

Papa:Kuhubiri Ufalme,msamaha wa dhambi,kuponesha na ishara ni cheche za nuru ya Yesu

Katika Dominika II ya Kwaresima,Injili imetuonesha kung'ara kwa Bwana,Papa katika tafakari yake kwa waamini na mahujaji katika Uwanja wa Mtakatifu Petro,Vatican tarehe 25 Februari 2024 alisema:“Kuhubiri Ufalme,msamaha wa dhambi,kuponesha na ishara alizotimiza zilikuwa kiukweli cheche za mwanga mkuu zaidi:mwanga wa Yesu,mwanga ambao ni Yesu."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, akiwa katika dirisha la Jumba la Kitume mjini Vatican, ametoa tafakari yake ya Dominika ya Pili ya Kwaresima, tarehe 25 Februari 2024. Akianza Baba Mtakatifu amesema: “Injili ya Dominika ya Pili ya Kwaresima inatuwakilisha tukio la kung’ara kwa Yesu (Mk 9,2-10). Baada ya kuwatangazia mitume Mateso yake, Yesu alimchukua Petro, Yakobo na Yohane na kwenda nao juu ya mlima mrefu na kujionesha kimwili mwanga wake wote. Na kwa njia hiyo anawaonesha wao maana ya kile ambacho alikuwa ameishi pamoja hadi  wakati huo. Kuhubiri Ufalme, msamaha wa dhambi, kuponesha na ishara alizotimiza zilikuwa kiukweli cheche za mwanga mkuu zaidi: mwanga wa Yesu, mwanga ambao ni Yesu.

Waamini katika uwanja wa Mtakatifu petro 25 Februari 2024
Waamini katika uwanja wa Mtakatifu petro 25 Februari 2024

Na kutoka katika mwanga huo wafuasi hawapaswi kwamwe kuchosha mtazamo wa macho hasa katika vipindi vya majaribu, kama yale ambayo, yanakaribia ya Mateso. Huu ndio ujumbe: kamwe tusiondoe macho yetu kwenye nuru ya Yesu. Kama vile wakulima walivyofanya zamani ambao, walipokuwa wakilima mashamba, walikazia macho yao kwenye sehemu iliyo mbele yao na, wakikazia macho kwa lengo a  haki za alama iliyofuatiliwa. Hiki ndicho ambacho sisi Wakristo tunaitwa kufanya katika safari ya maisha: daima kuweka uso angavu wa Yesu na  tusiondoe kamwe mtazamo kwa Yesu.

Papa akiwa katika dirisha la Jumba la Kitume 25 Februari 2024
Papa akiwa katika dirisha la Jumba la Kitume 25 Februari 2024

Baba Mtakatifu akiendelea ameeleza kuwa tujifungulie katika nuru ya Yesu. Yeye ni upendo, Yeye ni  maisha yasiyo na mwisho. Katika njia ndefu ya maisha, wakati mwingine ngumu, tutafute uso wake, uliojaa huruma, imani, na matumaini. Vinatusaidia kufanya kwa sala, kusikiliza Neno, Sakramenti, hasa ya kitubio na Ekaristi. Kwa kuongezea Papa amesema, kwa sala na kusikiliza Neno na Sakramenti vinatusaidia kukazia macho kwa Yesu.”

Waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro
Waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro

Baba Mtakatifu amesema kuwa lakini pia inatusaidia kuwatazama watu machoni, kujifunza kuona nuru ya Mungu kwa kila mtu na kukuza uwezo wa kustaajabishwa na uzuri huu unaoangaza ndani ya kila mtu, bila ubaguzi: kwa wale walio karibu nasi na kwa  wageni; Kwa mitazamo ya furaha kwa yule aliye na furaha na yale yenye machozi kwa anayelia; katika macho yenye huzuni na yale yaliyozima ambaye anamejaribiwa na maisha na amepoteza shauku; na hata mwenye kuwa na ugumu wa kutazama uso, akipendelea kugeuza kisogo sehemu nyingine.

Waamini katika sala ya Malaika wa Bwana
Waamini katika sala ya Malaika wa Bwana

Na hayo ni mapendekezo  mazuri ya Kwaresima: kukuza mitazamo wazi, kugeuka kwa watatufaji wa mwanga, watafutaji wa mwanga katika Yesu. Katika sala na katika watu. Kwa njia hiyo tujiulize: katika safari yangu, ninakaza macho juu ya Kristo anayenisindikiza? Na kwa kufanya hivyo ninatoa nafasi ya ukimya, katika sala na katika kuabudu? Mwisho ninakwenda kutafuta kila mwale mdogo wa mwanga wa Yesu, ambaye anajiangaza ndani mwangu na kwa kila kaka na dada ninayekutana naye? Na mimi ninakumbuka kumshukuru Bwana kwa hilo ? Maria, anayeng’aa nuru ya Mungu, atusaidie kukazia mtazamo wetu juu ya Yesu na kujitazama sisi wenyewe kwa matumaini na mapendo. Baba Mtakatifu amehitimisha.

Tafakari kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana Februari 25,2024
25 February 2024, 12:12