Papa:Kuna hitaji la kuponya ukoma wa kiroho,ubinafsi,ubaguzi na kutovumilia
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko katika Dominika ya VI ya Kipindi cha Kawaida cha Mwakaambapo ilikuwa ni Siku ya Bikira Maria wa Lourdes sanjari na Siku ya Wagonjwa duniani iadhimishwayo kila ifikapo tarehe 11 Februari ya kila mwaka, ameongoza Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya Kumtangaza Mwenyeheri María Antonia wa Mtakatifu Yosefu wa Nchini Argentina kwa kuudhuriwa na maelefu ya waamini na mahujaji kutoka pande za dunia, lakini pia rais wa Nchi hiyo Mileli. Katika mahubiri yake, Papa kwa kuongozwa na masomo ya siku kutoka Walawi (13, 1-2.45-46) na Injili (Mk 1,40-45,) yalielezea ukoma: ugonjwa ambao unapelekea taratibu uharibifu wa kimwili wa mtu na ambao mara nyingi, kwa bahati mbaya bado upo leo hii katika baadhi ya maeneo na tabia za kutengwa. Ukoma na kutengwa ni magonjwa mawili mabaya ambayo Yesu anataka kumkomboa mtu ambaye anakutana katika Injili.
Baba Mtakatifu Francisko ameanza kuelezea hali yake kwamba Mkoma huyo alilazimaka kuishi nje ya mji. Mdhaifu kwa hali yake ya ugonjwa, kinyume cha kusaidiwa na raia wenzake anaachwa peke yake, zaidi amejeruhiwa kwa kina kwa kuwekwa mbali na kukataliwa. Kwa nini ? Kwa sababu ya kuogopa, awali ya yote hofu ya kuambukizwa na mwisho kugeuka kama yeye: “Ni jambo ambalo linatuangukia hasa sisi! Hatuthubutu, tunakuwa mbali! Kuogopa. Baadaye hukumu: “ Ikiwa kuna magonjwa mabaya sana, kulikuwa na mawazo ya kawaida ya pamoja,- hakika ni kwa sababu Mungu amemwadhibu kwa sababu ya makosa aliyotenda:kwa wakati ule kwa hakika walikuwa wakifikiria kuwa kugusa mtu aliyekufa unakuwa najisi, na wakoma walikuwa watu ambao mwili wao “ulikuwa umekufa.” Kwa njia hiyo, walifikiri kumgusa ni sawa na kugeuka najisi kama wao: Na ndiyo tazama dini potovu ambayo inaamsha kuta na kukosa huruma, Papa Francisko amesisitiza.
Hofu, ubaguzi na udini wa uwongo: hapa kuna sababu tatu za ukosefu mkubwa wa haki, “ukoma wa roho” magonjwa matatu ambayo humfanya mtu dhaifu kuteseka, na kumtupa kama taka. Papa amesema tusifikirie kuwa haya ni mambo ya zamani tu. Ni watu wangapi wanaoteseka tunakutana nao kando ya barabara za miji yetu! Na ni hofu ngapi, chuki na kutofautiana, hata miongoni mwa wale wanaoamini na kujidai kuwa Wakristo, na hofu hizi zinaendelea kuwaumiza zaidi! Hata katika wakati wetu kuna kutengwa sana, kuna vikwazo vya kuvunja, kuna "ukoma" wa kuponya. Lakini jinsi gani? Tunawezaje kufanya hivyo? Yesu anafanya nini? Yesu anafanya ishara mbili: anagusa na kuponya. Katika hilo Baba Mtakatifu ameanza kufafanua ishara ya kwanza ya kugusa kwamba: “Yesu kwa kusikia kilio cha kuomba msaada wa mtu huyo (Mk 1, 40) alihisi huruma, alisimama, aliinua mkono na kugusa (Mk 1, 41) licha ya kujua kuwa kwa kufanya hivyo atageuka “kukataliwa.” Kinyume chake sehemu hizi zitaguswa: mgonjwa atakapopona ataweza kwenda kujionesha kwa makuhani ili aweze kurudishwa kwenye jumuiya; Na Yesu kinyume chake, hasingeweza kuingia tena katikati ya wakazi (Mk 1, 45). Bwana angeweza kwa hiyo kuzuia kugusa mtu huyo, kwani “ingetosha kumtibu kwa mbali.”
Kristo lakini hakufanya hivyo, njia yake ni ile ya upendo ambao inakuwa karibu na yule anayeteseka, ambaye anaingia katika mawasiliano, ambaye anagusa majeraha. Mungu wetu, hakubaki mbali huko mbinguni, lakini katika Yesu ambaye alijifanya mtu ili kugusa umasikini wetu. Na mbele ya “ukoma mbaya zaidi, ule wa dhambi, hakusita kufa msalabani, nje ya ukuta wa mji, kwa kutupwa kama mdhambi, kwa kugusa hadi ndani ya ukweli wa ubinadamu wetu. Mtakatifu mmoja aliandika “”alijifanya mkoma kwa ajili yetu.” Na sisi ambao tunapenda na kumfuata Yesu, tunajua kufanya kwa “mguso wake?” Siyo rahisi na tunapaswa kukesha wakati katika moyo tunakumbana na hisia tofauti na “kuwa karibu “ na kujifanya “zawadi yake:” kwa mfano tunapopunguza ulimwengu kuwa wa kuta ili “kukaa kwetu vizuri,” tunapoamini kuwa tatizo daima ni juu ya wengine… Katika kesi hizi tuwe makini kwa sababu vipimo ni wazi “ni ukoma wa moyo:” Ugonjwa ambao unatufanya kuwa wagumu katika upendo, katika huruma, unaotuharibu kwa njia ya “saratani” ya ubinafsi, dhana ya awali, kutojali na kutovumilia. Tuwe makini hata kwa sababu kama ilivyo madoa ya kwanza ya ukoma, yanayojitokeza juu ya ngozi katika hatua za kwanza ugonjwa, ikiwa hatuingilii kati haraka, ugonjwa unakua na kusambaa. Mbele ya hatari hiyo na uwezekano wa roho yetu, tiba yake ni ipi?
Tunasaidiwa na ishara ya pili ya Yesu ambaye anaponesha (Mk 1, 42). Ile ya “kugusa” kiukweli haielekeza ukaribu tu, bali ni mwanzo wa kuponesha. Ni kwa sababu ya kujiachia tuguswe na Yesu ambaye anatupenosha ndani ya moyo. Ikiwa tunaacha tuguswa naye katika sala, katika kuabudu, ikiwa tunamruhusu atende ndani mwetu kwa njia ya Neno lake na Sakramenti, mguso wake unatubadili kiukweli, unatutakasa na dhambi, unatukomboa dhidi ya kujifungia kwetu, unatubadili mbali na kile ambacho tungefanya peke yetu na kwa nguvu zetu. Sehemu zetu zilizojeruhiwa, magonjwa ya roho lazima yaletwe kwa Yesu: sala hufanya hivi; lakini isiwe sala ya kufikirika, zinazofanywa tu kwa kanuni za kurudiwa, bali sala ya dhati na hai, ambayo huweka taabu, udhaifu, uwongo na hofu miguuni pa Kristo. Na tunaweza kujiuliza: je, ninamruhusu Yesu auguse “ukoma” wangu ili aweze kuniponya? Kwa hakika, kwa “mguso," wa Yesu, kiukweli huzaliwa upya ubora wetu: tishu za moyo zinafanywa upya; damu za msukumo wa ubunifu wetu huanza kutiririka tena zilizojaa upendo; majeraha ya makosa ya zamani huponya na ngozi ya mahusiano hupata uthabiti wake wa afya na asili.
Hivyo unarudi uzuri tulionao na uzuri wa jinsi tulivyo; kwa kupendwa na Kristo, tugundue tena furaha ya kujitoa kwa wengine, bila woga na chuki, tukiwa huru kutokana na aina za dini zenye kutia ganzi na zisizo na mwili wa ndugu yetu; uwezo wa kupenda hurejesha nguvu ndani yetu, zaidi ya mahesabu yote na urahisi. Kwa njia hiyo kama vile ukurasa mzuri wa Maandiko unavyosema (rej. Ez 37:1-14), kutoka kwenye kile kilichoonekana kama bonde la mifupa iliyonyauka, miili iliyo hai inafufuka tena na watu wa waliookolewa, jumuiya ya ndugu, wanazaliwa upya. Lakini itakuwa ni kupotosha kufikiri kwamba muujiza huu unahitaji aina kuu na za kuvutia kutekelezwa. Inatokea hasa katika upendo uliofichwa wa kila siku: ambao ni uzoefu katika familia, kazini, katika parokia na shuleni; mitaani, katika ofisi na maduka; yule ambaye hayatafuti utangazaji na hayahitaji makofi, kwa sababu upendo unatosha kwa upendo (rej. Mtakatifu AGOSTINO, na katika Zab. 118, 8, 3). Yesu anasisitiza hili leo, anapomwamuru mtu aliyeponywa “asiseme neno kwa mtu yeyote” (Mk 1, 44): ukaribu na busara.
Baba Mtakatifu amewaambia waamini wote kuwa “Mungu anatupenda hivi na tukijiachilia tuguswe naye, sisi pia, kwa nguvu za Roho wake, tutaweza kuwa mashahidi wa upendo uokoao!” Baba Mtakatifu Francisko akigeukia sura ya Mtakatifu Mpya amesema kuwa “Na leo tunamfikiria María Antonia dwa Mtakatifu Yosefu "Mama Antula". Alikuwa msafiri wa Roho. Alisafiri maelfu ya kilomita kwa miguu, katika majangwa na barabara za hatari, ili kumpeleka Mungu. Leo yeye kwetu sisi ni kielelezo cha ari na ujasiri wa kitume. Wakati Wajesuti walipofukuzwa, Roho aliwasha ndani yake mwali wa kimisionari ulioegemezwa kwenye imani katika riziki na ustahimilivu. Aliomba maombezi ya Mtakatifu Joseph, na ili asimchoshe sana pia yale ya Mtakatifu Gaetano Thiène. Kwa sababu hii alianzisha ibada na picha yake ya kwanza ilifika Buenos Aires katika karne ya XVIII. Shukrani kwa Mama Antula Mtakatifu huyu, mwombezi wa Majaliwa ya Mungu, aliingia katika nyumba, vitongoji, usafiri, maduka, viwandani na mioyoni, ili kutoa maisha ya heshima kwa kazi, haki, mkate wa kila siku, kwenye meza ya maskini. Leo hii tunaomba kwa María Antonia, Mtakatifu Maria Antonia de Paz de San José, atusaidie sana. Bwana atubariki sisi sote.