Tafuta

2024.02.28  Papa amekutana na Sinodi ya Kanisa Katoliki la Kiarmenia. 2024.02.28 Papa amekutana na Sinodi ya Kanisa Katoliki la Kiarmenia.  (Vatican Media)

Papa:kuwa karibu na watu wa Nagorno-Karabakh.Ni mauaji mangapi huko nyuma

Papa amekutana na washiriki wa Sinodi ya Kanisa la Kipatriaki wa Kiarmenia la Kilkia.Kutokana na mafua hotuba imesomwa na mshirika wake.Wazo ni familia zilizohamishwa na tumaini kwamba kilio cha amani kitagusa mioyo pia wasiyojali mateso ya maskini.Kwa upande wa maaskofu:“Ninyi mmewakwa wakfu kwa ajili ya kundi,waaminifu wa uchungaji na sio waliofika,kama wafanyabiashara au daima wa kubeba begi mikononi.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumatano tarehe 28 Februari 2024 kabla ya Katekesi ya Papa amekutana na Wajumbe wa Sinodi ya Kanisa la Kiarmenia ya Kilkia walioko mjini Roma katika Hija kwenye makaburi ya Watakatifu Petro na Paulo, mara baada ya maadhimisho ya kumbu kumbu ya  Mtakatifu Gregorio wa Narek,  Mwalimu wa Kanisa.  Katika Jumba la Kitume, Papa kutokana na kuwa na mafua, kwa siku hizi zilizopita na ambapo bado hali yake haijatengamaa, aliomba mshirika wake Monsinyo Filippo Ciampanelli kusoma hotuba. Baada ya kuwakaribisha amesema  wao ni wachungaji na kwa sababu hiyo, katika siku ya kuwekwa wakfu kwa Maaskofu, walijitolea kuhifadhi imani, kuimarisha tumaini na kueneza mapendo ya Kristo. Kwa njia hiyo, moja ya jukumu kubwa la Sinodi ni kulipatia Kanisa lao Maaskofu wa kesho.

Papa amewasihi wachague kwa uangalifu, ili wajitolee kwa kundi, wawe waaminifu kwa uchungaji na sio kuongozwa na tamaa ya kibinafsi.” Kwa hiyo hawapaswi kuchaguliwa kwa msingi wa mawazo au matakwa yao wenyewe na tahadhari kubwa itumike kwa wale walio na pua ya biashara au wale ambao “kila wakati wakiwa na begi  mkononi huku wakiwaacha watu wao yatima.” Katika ujumbe huo unabainisha kuwa Askofu ambaye anaona Upatriaki kama msingi wa  hatua hadi nafasi nyingine ya kifahari zaidi anasahau kwamba ameolewa na Kanisa na hatari, ambapo ameomba aruhusiwe kutumia usemi wa ‘uhasherati wa kichungaji.’ Na kwamba “Jambo hilo hilo hutokea mtu anapopoteza muda huku akipanga njama ili kupata kazi mpya au kupandishwa vyeo. Maaskofu hawanunuliwi sokoni; ni Kristo anayewachagua kuwa Warithi wa Mitume wake na Wachungaji wa kundi lake.

Maskofu katoliki wa kiarmenia
Maskofu katoliki wa kiarmenia

 

“Katika ulimwengu uliojaa upweke na utupu lazima tuhakikishe kwamba wale waliokabidhiwa uangalizi wetu wanahisi ukaribu wa Mchungaji Mwema, kujali kwetu sisi wenyewe kwa baba, uzuri wa udugu na huruma ya Mungu. Watoto wa watu wao wapendwa wanahitaji ukaribu wa Maaskofu wao.” Katika hotuba hiyo Papa anawakikishia kutambua kwamba watu wao  wako ughaibuni ulimwenguni  kote kwa wingi na nyakati nyingine katika maeneo makubwa, ambako ni vigumu kwao kutembelewa. Hata hivyo Kanisa ni Mama mwenye upendo na haliwezi kushindwa kutafuta kila njia iwezekanayo ya kuwafikia na kuwapa upendo wa Mungu katika mapokeo yao ya kikanisa. Si suala la miundo, ambayo ni njia tu ya kusaidia kueneza Injili, lakini zaidi ya yote ni upendo wa kichungaji, kutafuta na kukuza mema kwa mtazamo wa kiinjili na moyo wazi: hapo Papa anadhani pia umuhimu wa ushirikiano wa karibu zaidi na Kanisa la Kitume la Kiarmenia.

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe anabainisha kuwa: “katika kipindi hiki kitakatifu cha Kwaresima tunaalikwa kuutafakari msalaba na kujenga juu ya Kristo anayeponya majeraha yetu kwa msamaha na upendo. Tumeitwa kuwaombea wote, kwa upana wa akili na roho. Kama Mtakatifu Gregory wa Narek, ambaye aliomba: Bwana, “kumbuka...  wale walio katika jamii ya wanadamu ambao ni adui zetu, lakini kwa ajili yao uwape msamaha na rehema”. Akiwa na maono ya kinabii yenye kutokeza, aliongeza hivi: “Msiwaangamize wale wanaonipiga taya zao, bali wabadilisheni! Ondoeni mwenendo mbaya wa kidunia na mpande wema ndani yangu na ndani yao” (Kitabu cha maombolezo, LXXXIII).

Baba Mtakatifu  katika hotuba hiyo amesisitiza kwa viongozi hao kuwa “pamoja na makuhani, mashemasi, wanaume na wanawake waliowekwa wakfu na waamini wote wa Kanisa lanu, mna jukumu kubwa. Mtakatifu Gregory Nareck alileta nuru ya Kristo kwa watu wa Armenia, ambao walikuwa wa kwanza, kama vile, kukaribisha nuru hiyo katika historia yao.” Kwa sababu hiyo, “ninyi ni mashahidi na kana kwamba ni “mzaliwa wa kwanza” wa nuru hiyo, mapambazuko yaliyoitwa kuangaza miale ya unabii wa Kikristo katika ulimwengu ambao mara nyingi unapendelea giza la chuki, migawanyiko, vurugu na kisasi. Mnaweza kunikumbusha kwamba Kanisa lenu si kubwa kwa idadi. Hata hivyo tukumbuke kwamba Mungu anapenda kufanya maajabu na wale walio wadogo. Kwa mantiki hiyo, tafadhali msiache kuwajali wadogo na maskini, kwa kuiga maisha ya kiinjili yaliyo mbali na fahari ya utajiri na majivuno ya madaraka, kwa kuwakaribisha wakimbizi na kuwasaidia walioko ughaibuni kama kaka na dada, wana na mabinti.”

Papa amesali na maaskofu wa kiarmenia
Papa amesali na maaskofu wa kiarmenia

Papa Francisko amependa kushirikisha nao jambo lingine ambalo aliona ni la kupewa kipaumbele: “kusali sana, si kidogo  ili kuhifadhi mtazamo wa mambo ya ndani unaokuwezesha kufanya kazi kwa upatano unapotambua vipaumbele vya Injili, wale wapendwao na Bwana. Kwa maneno ya msemo wa kale wa Kilatini: ‘Hifadhi utaratibu na utaratibu utakuhifadhi.’ Kwa njia hiyo maaskofu hao wajihadhari kwamba Sinodi zao zimeandaliwa vyema; masuala yaliyosomwa kwa uangalifu na kutathminiwa kwa busara; na kwamba maamuzi, daima na yanayolenga tu manufaa ya nafsi, hutumiwa na kujaribiwa kwa busara, uthabiti na uwezo, kuhakikisha, juu ya yote, uwazi kamili, pia ambapo fedha zinahusika. Sheria lazima zijulikane na zitumike si kwa roho ya ushikaji sheria bali kwa sababu ni vyombo vya eklesiolojia vinavyoruhusu hata wale wasio na mamlaka kukata rufaa kwa Kanisa kwa haki kamili na zilizoratibiwa waziwazi, na wasijikute kwa matakwa ya wenye mamlaka.”

Wazo lingine ambalo  Papa alipenda kukuaminisha na kuwakabidhi linahusiana na uchungaji wa miito. Katika ulimwengu wetu wa kilimwengu, waseminari na wale wanaofundwa katika maisha ya kidini wanahitaji, leo zaidi ya hapo awali, kuwa na msingi thabiti katika maisha ya kweli ya Kikristo, mbali na ‘majina ya kifalme.’ Vivyo hivyo, mapadre, hasa mapadre vijana, wanatakiwa kujisikia kuwa karibu na Maaskofu wao, ambao watakuza ushirika wao wa kidugu, ili wasikatishwe tamaa na magumu, bali wakue kila siku katika utiifu kwa ubunifu wa Roho Mtakatifu, wakiwahudumia watu wa Mungu kwa furaha iliyozaliwa na upendo, si kwa tabia ya kutokuinama na kutojali ya watendaji wa serikali. Katika mambo yote na tuwe na tumaini, ingawa mavuno ni mengi sikuzote na watenda kazi ni wachache, tumtegemee Bwana atendaye maajabu kwa wale wanaomtumaini.”

Picha ya Pamoja na maaskofu wa kiarmenia
Picha ya Pamoja na maaskofu wa kiarmenia

Papa Francisko aidha amesema  hawezi hatimaye kutoelekeza mawazo yake kwa Armenia, si kwa maneno tu bali zaidi ya yote katika sala zetu, hasa kwa wale wote wanaokimbia Nagorno-Karabakh na kwa ajili ya familia nyingi zilizohamishwa zinazotafuta kimbilio. Vita vingi, na mateso mengi! Vita vya Kwanza vya Ulimwengu vilipaswa kuwa vya mwisho; iliongoza kwenye kufanyizwa kwa Ushirika wa Mataifa, “mtangulizi” wa Umoja wa Mataifa, kwa kuamini kwamba hilo lingetosha kuhifadhi zawadi ya amani. Hata hivyo tangu wakati huo, ni migogoro mingapi na mauaji ambayo tumeshuhudia, daima ya kusikitisha na yasiyo na maana. Mara nyingi nimesihi: “Inatosha!” Sote tuchukue kilio cha amani, ili kiguse mioyo, hata mioyo isiyoguswa na mateso ya maskini na wanyonge. Na zaidi ya yote, tuombe. Ninawaombea ninyi  na Armenia; na ninawaomba, tafadhali, mniombee!”

Papa amewashukuru kwa uwepo wao na kwa huduma yao. Kabla ya kutoa baraka zake, alipenda kusali sala ya Mtakatifu Nerses Mwenyeheri. Na aliwaomba wasali pamoja naye, kwa kutarajia siku ambayo, Mungu akipenda, kuweza kumwadhimisha katika madhabahu moja na kaka  na dada zetu wa Kanisa la Mitume la Armenia: “Mungu  mwingi wa rehema, uwarehemu wale wote wanaokuamini; juu ya wapendwa wangu, na juu ya hao wageni kwangu; juu ya wale wote ninaowajua, na juu ya wale wasiojulikana kwangu; juu ya walio hai na juu ya wafu; hata uwasamehe adui zangu, na wale wanaonichukia, wasamehe makosa waliyonitenda; na uwaondolee ubaya wanaoniwekea, ili wapate kustahiki rehema yako. Virehemu viumbe vyako, na juu yangu mimi mwenye dhambi nyingi” (Maungamo ya Imani 24, XXIII). 

Maaskofu Katoliki wa kiarmenia ya Kilkia wakutana na Papa Francisko
28 February 2024, 15:57