2024.02.03 Jumuaiya ya Seminari ya  Madrid imekutana na Papa. 2024.02.03 Jumuaiya ya Seminari ya Madrid imekutana na Papa.  (Vatican Media)

Papa kwa Seminari ya Madrid:jikomboe katika mawazo ya kidunia&mweke Mungu katikati

Akikutana na Jumuiya ya Seminari ya Jimbo Kuu la Madridi,Hispania iliyofuatana na Askofu Mkuu Cobo Cano aliyekuja kukabidhiwa Kanisa la Santiago ya Montserrat,Roma,Papa amejibu maswali ya mapadre wajao na kukabidhi hotuba aliyokuwa ametayarisha akisisitiza kitovu cha Ekaristi katika shughuli zote.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko  Jumamosi tarehe 3 Februari 2024 amekutana  na Jumuiya ya Seminari ya Jimbo Kuu la Madrid nchini Hispania. Katika hotuba yake  aliyowakabidhi, amebainisha jinsi ambavyo wamekuja jijini Roma kwa  tukio la furaha la kumsindikiza Askofu Mkuu José ambaye atakabidhiwa Kanisa la Santiago ya Montserrat, Roma ambalo linaunganisha katika watakatifu wake wenye sifa ya imani ya kitume na upendo kwa Maria ambao ni sifa ya Hispania yote. Na Padre José pia anaambatana na hazina yake ya thamani sana, ambayo ni wao waseminari wake. Maaskofu wengi watakatifu wa Hispania walikabiliwa na ukweli mgumu unaoyakabili makanisa yao, na walifikiri juu ya seminari kama mahali ambapo ndoto yao ya kichungaji ingekita mizizi na kupanuka. Kiukweli, ikiwa tunataka kuwa Kanisa, Mwili wa Kristo, ni rahisi kwa sababu, kama vile Mungu alivyomwambia Musa, inatubidi tu kuweka kielelezo tulichoona mlimani(taz Kut 26:30).

Papa amekutana na  Jumuiya ya Seminari Kuu ya Madrid
Papa amekutana na Jumuiya ya Seminari Kuu ya Madrid

Katika hotuba hiyo Papa anasema kuwa msemo unakuja akilini kutoka kwa mmoja wa maaskofu hawa watakatifu, ambaye pengine wanawafahamu, alitaka “seminari ambamo Ekaristi ilikuwa: kwa utaratibu wa ufundishaji, kichocheo chenye ufanisi zaidi; katika kisayansi, mwalimu wa kwanza na somo la kwanza; katika nidhamu mkaguzi makini zaidi; katika mfano wa kusisimua zaidi; katika uchumi riziki kubwa; na katika usanifu jiwe la msingi” (Mtakatifu Manuel González, Un sueño pastoral). Papa Francisko katika hayo amependa kuzingatia mambo haya ili kumweka Mungu katikati, yaani kumwacha awe msingi, mradi na mbunifu, jiwe la msingi. Hili linapatikana kupitia ibada tu. Yesu - mtakatifu wetu anatuambia - atakuwa mwalimu wetu, mvumilivu, mkali, mtamu na dhabiti kulingana na kile tunachohitaji katika utambuzi wetu, kwa sababu anatujua bora kuliko sisi wenyewe, na anatungojea, hututia moyo na kutuunga mkono katika safari yetu yote. Ni kichocheo chetu kikubwa zaidi, kwa sababu tumejitolea maisha yetu kufuata.”

Inaonekana kwa Baba Mtakatifu kwamba katika uwanja wa kisayansi Mtakatifu Manuel anachanganya kuwa mwalimu na kuwa jambo. Mungu anataka kuwapa Watu wake wachungaji kulingana na moyo wake (taz Yer 13:15), hatujifunzi mambo kutoka kwa Yesu, tunamkaribisha, tunashikamana naye, ili tuweze kumpeleka kwa wengine. Na funzo kuu ambalo Bwana anatupatia ni ubinadamu, kuwa mwili, dunia, mtu, humus kwa ajili yetu, kutokana na upendo. Na katika jambo hili hakuna mfano mwingine isipokuwa Yeye mwenyewe; ya wema na hali nyingine Yesu atatoa mifano, mlinganisho, tini, mbegu na dhoruba, lakini tunaweza tu kujifunza somo kuu la maisha yake kutoka kwa wale ambao ni wapole na wanyenyekevu wa moyo (Mt 11, 29).

Waseminari wa Seminari Kuu ya Madrid na Papa
Waseminari wa Seminari Kuu ya Madrid na Papa

Kwa nidhamu, kujikabili wenyewe kila asubuhi na Ekaristi, mkaguzi aliye macho zaidi hutufanya tutafakari juu ya ubatili wa mawazo yetu ya kidunia, ya tamaa zetu za kupaa, kuonekana, kusimama nje. Aliye mkubwa anajifanya kuwa zawadi kamili na mikononi mwangu, kabla ya kuwasiliana, ananiuliza: Je, umepatana na ndugu yako? Je, umevaa mavazi yako ya sherehe? Je, uko tayari kuingia kwenye karamu yangu ya milele? Hadi sasa tumeona utambuzi, sayansi na umakini; hakika ni vipengele muhimu katika seminari yao, lakini havingekuwa na manufaa yoyote bila moyo kujinyima; kuiga kielelezo kunahitaji juhudi, kufanya kazi ya sanaa kunahitaji msukumo, lakini pia kazi, Yesu hakukwepa haya yote.

Ni muhimu kuingia jangwani, ili azungumze na mioyo yetu, ikiwa hii imejaa mambo ya kidunia, ya mambo, hata kama yanaweza kuitwa  ya kidini, Mungu hatapata nafasi, wala hatutamsikia wakati anabisha mlango wetu. Kwa hiyo ukimya, maombi, kufunga, toba, kujinyima mambo ni muhimu ili kutuweka huru na yale yanayotufanya kuwa watumwa na kuwa wa Mungu kabisa. Na hili si tu ndani, bali pia nje, katika kazi, katika miradi, tukijiachia kwa Yesu; Bwana atakuwa riziki kuu, tumruhusu apendekeze na kutekeleza, tujiweke tu kwa amri yake kwa unyenyekevu wa roho. Papa Francisko anakazia katika hotuba hiyo kuwa kumwamini yeye aliyewaita kwa ajili ya kazi hiyo nzuri, na kusujudu kwa kuabudu ili kwamba waweze kujenga kwa upole hekalu la Mungu katika watu wao na katika jumuiya zao. Na wanapokuwa katika kusali na kuadhimisha wasisahau kumuombea.

Papa amekutana na Jumuiya ya Seminari ya Madrid
03 February 2024, 16:04