Papa,Mabomu ya kutegwa ardhini:vifaa hivi vya kulipuka vinatukumbusha janga la vita
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Njaa, vurugu, mauaji, kuhama, ukiukwaji wa haki za binadamu, na, kana kwamba haitoshi, hata mabomu ya ardhini ya kupambana ambapo uwasababishia vifo na ulemavu wa raia wasio na hatia hata baada ya miaka. Dhidi ya vifaa hivi vya hila ambavyo vinatukumbusha juu ya matokeo makubwa ya vita na katekesi ya Papa kwenye Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican. Akiwa bado na mafua kutokana na homa ya siku za hivi karibuni, Baba Mtakatifu Francisko baada ya mshirika wake Monsinyo Filippo Ciampanelli kusoma katekesi, yake huko akisafisha koo lake na yeye mwenyewe alichukua fursa ya kutoa wito huko akilaani zana za uharibifu na pia vifo.
Maadhimisho ya Mkataba wa Ottawa
Baba Mtakatifu Francisko amefanya hivyo akikumbuka juu ya hafla ya kumbukumbu ya miaka 25 itakayofanyika tarehe Mosi Machi ya kuanza kutumika Mkataba wa kupiga Marufuku kutega mabomu ya ardhini kwa Mkataba unaoitwa Ottawa uliohitimishwa mnamo 1997 na ulianza kutumika mnamo 1999, ambao uliidhinishwa na Mataifa 164, pamoja na 34 ya Mkataba wa Ottawa. Nchi 50 ambazo zilikuwa wazalishaji kabla ya 1997. Kwa njia hiyo Papa Francisko amesema:“Tarehe 1 Machi itakuwa kumbukumbu ya miaka 25 tangu kuanza kutumika kwa Mkataba wa Kupiga Marufuku mabomu ya kutegwa ardhini ambayo yanaendelea kuwalenga raia wasio na hatia, hasa watoto, hata miaka mingi baada ya kumalizika kwa uhasama. Ninaelezea ukaribu wangu kwa waathiriwa wengi wa vifaa hivi vya hila, ambavyo vinatukumbusha ukatili mkubwa wa vita na gharama ambayo raia wanalazimika kuteseka. Katika suala hili, ninawashukuru wale wote wanaotoa mchango wao kusaidia waathirika na kusafisha maeneo yaliyochafuliwa. Kazi yao ni itikio thabiti kwa mwito wa ulimwenguni pote wa kuwa wapatanishi wa amani, tukiwajali kaka na dada zetu.” Kuhusiana na mabomu haya ya kutegwa ardhini ripoti iliyowasilishwa mwaka 2023 huko Geneva Uswiss na Kampeni ya Kimataifa ya Kupiga Marufuku Mabomu ya kutegwa ili Kupambana na Wafanyakazi” (ICBL),kiukweli ilizungumzia kuongezeka kwa idadi pia kutokana na ongezeko la waathrika nchini Ukraine, 608 (58 mwaka 2022), wa pili hata hivyo Siria (834) na baadaye Yemen na Myanmar.
Katika maombi kwa ajili ya Nchi Takatifu, Ukraine, Burkina Faso na Haiti
Katika hali hiyo hiyo, Baba Mtakatifu Francisko kabla ya baraka za mwisho, aliwataka wale waliohudhuria katekesi katika Ukumbi wa Paulo VI na wote waliounganishwa na mkutano wa Jumatano kutosahau watu wanaoteseka kwa sababu ya vita: “Ukraine, Palestina, Israeli na wengine wengi.” Papa hakukosa kuelekeza mawazo na sala kwa waathiriwa wa mashambulio ya hivi karibuni kwenye maeneo ya ibada huko Burkina Faso, ambayo yalikumbwa na umwagaji damu Dominika 25 Februari na shambulio la kigaidi mara mbili la kwanza kwenye Kanisa la Kikatoliki huko Essakane, ambalo lilisababisha vifo vya watu 15 na shambulio la msikiti mmoja huko Natiaboani kwa vifo kumi.
Kwa hivyo Papa ameonesha tena ukaribu kwa wakazi wa Haiti, ambapo uhalifu na utekaji nyara unaofanywa na magenge yenye silaha unaendelea. Chini ya Juma moja iliyopita, Ndugu 6 wa Shirika la Moyo Mtakatifu walitekwa nyara na makundi yenye silaha walipokuwa wakwenda shule, na Padre mwingine alichukuliwa baada ya kuadhimisha Misa katika mji mkuu Port-au-Prince. “Kaka na dada wapendwa, tusiwasahau watu wanaoteseka kwa sababu ya vita: Ukraine, Palestina, Israel na wengine wengi. Na tunawaombea waathriwa wa mashambulizi ya hivi karibuni kwenye maeneo ya ibada nchini Burkina Faso; na vilevile kwa wakazi wa Haiti, ambako uhalifu na utekaji nyara unaofanywa na magenge yenye silaha unaendelea. Kwa wote, baraka zangu!”