Papa Francisko ametuma ujumbe kwa mahakimu wa Amerika Kusini, huko Argentina akiwahimiza kuwa sheria zimeandikwa zinahitaji utekelezaji wake halisi. Papa Francisko ametuma ujumbe kwa mahakimu wa Amerika Kusini, huko Argentina akiwahimiza kuwa sheria zimeandikwa zinahitaji utekelezaji wake halisi.  (ANSA)

Papa,mahakimu,Argentina:Hakuna mustakabali,maendeleo,haki wala demokrasia katika dunia

Papa ametuma ujumbe kwa njia ya video kwa wajumbe wa Kamati ya Amerika Kusini ya majaji wa haki za kijamii na mafundisho ya kifransiskani nchini Argentina akiwakumbusha umuhimu msingi kwa wale wanaolinda haki katika hali ya kisheria kwa sababu soko na faida mara nyingi hudhulumu walio wadogo na hivyo usawa unahitajika.

Na Angella Rwezaula- Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 28 Februari 2024 ametuma ujumbe kwa njia ya  video kwa  Wajumbe wa Kamati ya Majaji na waamuzi wa Haki za Kijamii na Mafundisho ya Kifransiskani nchini Argentina na kuwatia moyo katika kazi yao ya kulinda haki za walio hatarini na wanaoteseka. Katika ujumbe huo amesema “Wapendwa Kaka na dada wa COPAJU ningependa kushiriki nanyi furaha ya makao makuu yenu mapya huko Buenos Aires na tawi la kwanza la Taasisi ya Ndugu Bartolomew wa Nyumba huko Amerika ya Kusini. Ni jinsi gani haki ilivyo muhimu katika hali hii tata! Ni muhimu sana kuweza kutafakari na kujielimisha tunapokabili changamoto mpya!” Baba Mtakatifu katika ujumbe huo amesema: “Dhamira ya wafanyakazi wa mahakama-wanasheria, majaji, waendesha mashtaka, watetezi - ni ya msingi na muhimu. Mahakama ndiyo njia ya mwisho inayopatikana katika Serikali ya kutatua ukiukaji wa haki na kuhifadhi usawa wa kitaasisi na kijamii.”

Watoto wanakula chakula katika madampo

Papa Francisko aidha amesisitiza kuwa: “Tunaishi katika nyakati za ukosefu mkubwa wa haki: matajiri wachache wanazidi kuwa na nguvu na mamilioni ya watu maskini  huku wakikataliwa na kutupwa. Hakuna mustakabali, hakuna maendeleo, hakuna haki wala demokrasia katika dunia ambayo mamilioni ya watoto kila siku wanaokula tu katika madampo ya taka za wale wanaokula. Haki za kijamii sio za bure. Utajiri wa kuwaunga mkono upo, lakini unahitaji maamuzi ya kisiasa ya kutosha, yenye mantiki na ya haki. Serikali, ambayo leo ni muhimu zaidi kuliko hapo awali, inaitwa kutekeleza jukumu hili kuu la ugawaji upya na haki ya kijamii.

Muungu soko na muungu faida

Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa “Wapendwa Majaji, Sheria, tayari zimeandikwa. Zinatumika. Tatizo ni utekelezaji wake halisi, utekelezaji wake kiukweli. Jukumu lenu linaanzia hapo. Muungu Soko na muungu wa Faida ni miungu ya uwongo ambayo inatuongoza kwenye uharibifu na uharibifu wa sayari. Historia imedhihirisha hili katika matukio mengi, na ya kusikitisha sana. Baba Mtakatifu kwa kufafanua zaidi amesema ni Moloki, (Moloch) aliyekuwa muungu wa Wakanaani aliyehusishwa katika vyanzo vya kibiblia na desturi ya kutoa dhabihu ya watoto,” ambaye hula vizazi vipya vinapozaliwa.”

Uhalali wa awali hautoshi. Hata zoezi lazima  liwe halali

Askifu wa Roma ameendelea kubainisha kuwa "Neno la Yesu ambalo Mafundisho Jamii ya Kanisa yamejikita juu yake, ni njia salama na yenye mwanga wa kuchangia katika utekelezaji wa mahakama. Ndugu, wale wote wanaotumia madaraka ya umma wanapaswa kukumbuka kwamba uhalali wa awali hautoshi. Hata zoezi lazima  liwe halali."

Ninawezaje kuwa hakini ikiwa natazama upande

Baba Mtakatifu akiwageukia tena mahakimu hao amewauliza maswali kwamba: "Je, mamlaka inaweza kuwa na uwezo gani ikiwa itajitenga na ujenzi wa jamii zenye haki na heshima? Je, ninaweza kuwa hakimu mzuri ikiwa nitatazama upande mwingine ninapokabiliwa na mateso ya wengine? Tafadhali, kila siku mbele ya kioo, jiulizeni na mjiulize kuhusu wengine."

Amani ni ujenzi wa kila siku

“Ninawasalimu COPAJU, ninawasalimu Taasisi ya Fray Bartolomé de las Casas, ninawasalimu wote. Ninaibariki nyumba yenu mpya, ninawatakia mafanikio mema katika juhudi zenu. Ninawaomba uthabiti na uamuzi mbele ya mifano isiyo ya kibinadamu na vurugu. Amani ni ujenzi wa kila siku na ninyi ni wafanyakazi wa Amani. Hatimaye ninawaomba mniombee na mimi ninafanya  hivyo kwa ajili yenu.”

UJUMBE WA PAPA KWA MAHAKIMU WA ARGENTINA
28 February 2024, 17:26