Tafuta

Mji wa Yerusalemu Mji wa Yerusalemu  (Neno Kuzina)

Papa:“Tufanye kazi pamoja kwa ajili ya amani ya Nchi Takatifu"

Papa Francisko amewaandikia kaka na dada wa Kiyahudi wa Israel akielekeza barua kwa Karma Ben Johanan,Mtaalimungu wa mazungumzo ya Wayahudi na Wakristo.

Vatican news

Moyo wangu uko karibu nanyi,kwa Nchi Takatifu,kwa watu wote wanaokaa ndani mwake, Waisrael na Wapalestina,  ninaomba kwamba hamu ya amani itawale juu ya wote. Ninataka mjue kwamba mko karibu na moyo wangu na moyo wa Kanisa. Maneno yao Baba Mtakatifu  Francisko anawaeleza kaka na  dada wa Kiyahudi wa Israel” katika barua iliyotumwa kwa(una lettera inviata a Karma Ben Johanan,), ambaye ni Mtaalimungu wa Mazungumzo ya Kiyahudi-Kikristo, ambaye alikuwa miongoni mwa waendelezaji katika majuma ya  hivi karibuni ya miito kwa Papa, iliyotiwa saini na karibu wakuu wa Wayahudi na wasomi 400, kwa ajili ya uimarishaji wa urafiki wa Kiyahudi-Kikristo baada ya janga la  tarehe 7 Oktoba 2023. Kwa upande wa maneno ya shukrani ya dhati kwa barua ya Papa iliyotolewa na Gazeti la Osservatore Romano, tarehe 3 Februari 2024 huko Yerusalemu na Mtaalimungu wa Israel: “Tunashukuru sana kwa uaminifu na roho ya urafiki ambayo Papa, na pamoja naye Kanisa zima, walitaka kuthibitisha uhusiano maalum unaounganisha jumuiya zetu, Katoliki na Wayahudi”.

Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu katika barua yake ambayo inaonesha tarehe 2 Februari 2024, alikumbuka jinsi ambavyo Nchi Takatifu kwa "bahati mbaya haijatengwa na shida ambayo inashikilia ulimwengu na ambayo ni vita ya ulimwengu vilivyo gawanyika vipande, na ambayo husababisha kwa ujumla uchungu na wasiwas.” Papa Francisko anabainisha katika barua hiyo jinsi vita vinavyoendelea vimezalisha mitazamo ya migawanyiko katika maoni ya umma duniani kote, ambayo wakati mwingine husababisha aina za chuki dhidi ya Wayahudi. “Ninaweza tu kusisitiza kwamba (...) uhusiano unaotuunganisha na ninyi ni wa pekee na wa umoja, bila kuficha, kwa kawaida, uhusiano ambao Kanisa linao na wengine, na kujitolea kwao pia. Njia ambayo Kanisa limeanza nanyi, watu wa kale wa Agano, inakataa kila aina ya chuki dhidi ya Uyahudi na chuki dhidi ya Wayahudi, ikilaani bila shaka udhihirisho wa chuki dhidi ya Wayahudi kama dhambi dhidi ya Mungu, wakitumaini  ushirikiano wa karibu zaidi kutokomeza matukio haya.”

Akirejea barua iliyotumwa kwake na wakuu wa kiyahudi na wasomi wa mazungumzo ya Kiyahudi-Kikristo, ambayo Papa alionesha kuthamini sana, anaandika: “Ninahisi hamu ya kuwahakikishia ukaribu na upendo wangu. Ninawakumbatia kila mmoja wenu, na hasa wale waliomezwa na dhiki, uchungu, hofu na hata hasira,” na kuongeza: “Pamoja nanyi tunaomboleza wafu, waliojeruhiwa, waliopata kiwewe, tukimsihi Mungu Baba aingilie kati na kuweka mwisho wa vita na chuki.”

Papa  Francisko anaonya kwamba katika nyakati hizi za ukiwa ni vigumu kuona “upeo wa mbele ambao mwanga unachukua nafasi ya giza, ambamo urafiki unachukua nafasi ya chuki (….) Hata hivyo, sisi, kama Wayahudi na Wakatoliki, ni mashuhuda wa upeo huo hasa. Na anamalizia kwa kutarajia kuwa: “Bado tuna mengi ya kufanya pamoja ili kuhakikisha kwamba ulimwengu tunawaachia wale wanaokuja baada yetu ni bora, lakini nina hakika kwamba tunaweza kuendelea kushirikiana kwa madhumuni haya.” Karma Ben Johanan, akitoa shukrani kwa Baba Mtakatifu, alikaribisha mwaliko wa Papa Francisko kwa kusema kuwa: “Tuko tayari kushirikiana ili chuki na vurugu viondolewe na milango ya amani ya kweli ifunguliwe kwa sisi sote tunaoishi katika nchi hii: Wayahudi. Wakristo na Waislamu. Tunaungana na Wakristo kwa imani kwamba dini zinaweza kuwa nguvu ya ubunifu inayoweza kufungua njia ambazo zingebaki kufungwa.”

Papa awaandikia Wayahudi
05 February 2024, 09:14