Tafuta

Watu wasio na mahali pa kukaa katika maeneo ya vita. Watu wasio na mahali pa kukaa katika maeneo ya vita. 

Papa:Ukiukwaji wa haki za binadamu katika maeneo ya vita hauvumiliki!

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana,Papa amekumbusha Siku ya Wagonjwa Duniani,na kwamba watu wengi wanaonyimwa haki ya matibabu na haki ya kuishi.Kwa sababu katika umaskini uliokithiri au kuteswa chini ya mabomu,katika Ukraine,Palestina,Myanmar na katika migogoro mingine.Ameomba kuwa karibu,huruma na upole kwa wagonjwa au watu dhaifu.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Mara baada ya Tafakari na Sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 11 Februari 2024, Baba Mtakatifu Francisko akiwa katika dirisha la Jumba la Kitume mjini Vatican kwa kuwageukia wamini na mahujaji waliokuwa katika uwanja wa Mtakatifu Petro amesema: “Leo ametangazwa Mtakatifu María Antonia wa amani wa Figueroa, mtakatifu wa Argentina, tumpigie makono Mtakatifu Mpya. Papa akiendelea amesema “leo inaadhimishwa kumbukumbu ya Bikira Maria wa Lourdes, sanjari na Siku ya Wagonjwa Ulimwenguni, ambayo mwaka huu inazingatia umuhimu wa uhusiano katika ugonjwa. Jambo la kwanza tunalohitaji tunapokuwa wagonjwa ni ukaribu wa wapendwa wetu, wahudumu wa afya na, katika mioyo yetu, ukaribu wa Mungu.”

Ukaribu na upole

Papa amesisitiza kuwa “Sote tunaitwa kuwa karibu na wale wanaoteseka, kuwatembelea wagonjwa, kama Yesu anavyotufundisha katika Injili. Hii ndiyo sababu leoni ​​nataka kueleza ukaribu wangu na ule wa Kanisa zima kwa wagonjwa wote au watu dhaifu zaidi. Tusisahau mtindo wa Mungu: ukaribu, huruma na upole.” Lakini siku hiti, Papa Francisko ameongeza kusema  “hatuwezi kupuuza ukweli kwamba kuna watu wengi leo hii ambao wamenyimwa haki ya kutunza, na kwa hivyo haki ya kuishi! Ninawafikiria wale wanaoishi katika umaskini uliokithiri; lakini pia nafikiria maeneo ya vita: haki za kimsingi za binadamu zinakiukwa huko kila siku! Haivumiliki. Tunaomba kwa ajili ya Ukraine inayoteswa, kwa ajili ya Palestina na Israel, tunasali kwa ajili ya Myanmar na watu wote wanaoteswa na vita.”

Hatimaye amewasalimia mahujaji wote kuanzia na Warumi na mahujaji kutoka nchi mbalimbali. Hasa, nawasalimu waamini wa Moral de Calatrava na Burgos (Hispania), wale wa Brasilia na Ureno; kwaya ya Vijana ya Mostar na Bendi ya Shule ya Vila Pouca de Aguiar (Ureno). Ninawasalimu waamini wa Enego na Rogno, wajitoleaji Madhabahu ya Mtakatifu  Anna wa Vinadio, Kwaya ya Eraclèa na Chama cha Mtakatifu  Paola Frassinetti cha Mtakatifu Calogero; vijana kutoka Lodi, Petosino na Torri di Quartesòlo; Wa kipaimara kutoka Malta, Lallio na AlmennoMtakatifu  Salvatore; wanafunzi wa Taasisi ya Mtakatifu Ambrogio" ya kisalesiani ya Milano na Watoto wa Coretto ya Piovène Rocchette; pamoja na kikundi cha "Radio Mater", katika hafla ya kuadhimisha miaka 30. Amewatakia Dominika njema na wasisahau kumuombea.

Papa baada ya Angelus
Siku ya Wagonjwa 11 februari
11 February 2024, 16:02