Papana Shirikisho la Kitaifa la Italia na China:endelea kujitoa kwa ukarimu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Papa Franciko amekutana na kutoa Salamu kwa Shirikisho la Kitaifa la Italia-China tarehe 2 Februari 2024. Katika hotuba yake amewakaribisha wote na kuwashukuru kwa ziara yao, ambayo imefanyika katika kumbukumbu ya miaka kumi ya kuanzishwa kwa Shirikisho la Kitaifa kati ya Italia-China na wakati wa sherehe za kuadhimisha Mwaka Mpya wa China. Kwa muda sasa, pamoja na kuandaa matukio ya sikukuu ya Mwaka Mpya, wameunga mkono juhudi kadhaa zinazolenga kukuza mazungumzo kati ya Italia na China, na kutafuta kujibu changamoto zinazoletwa na ushirikiano wa kiutamaduni, elimu na uendelezaji wa pamoja maadili ya kijamii.
Baba Mtakatifu Francisko ametoa “shukrani zangu kwa juhudi hizi, na ninawasihi muendelee na njia mliyofuata, mkifuatilia malengo haya kwa kujitolea kwa ukarimu.” Kwa njia hiyo, “kadiri jumuiya za Kiitaliano na Kichina zinavyofahamiana zaidi, hii inaweza kusababisha kukubalika zaidi na moyo wa kidugu. Katika kuwapatia salamu hizi njema za maombi,
Baba Mtakatifu amependa pia kushukuru Chuo cha Sanaa ya Vita cha China cha Vercelli kwa ngoma zilizochochewa na Simba na Joka. Katika utamaduni wa watu mashuhuri wa China, ngoma hizi zinaonesha matumaini kwamba Mwaka Mpya utakuwa wa mafanikio na wenye tija. “Wanasarakasi, kama tujuavyo, wana utaalam wa kuvutia na hata hatari sana za kuthubutu. Mtazamo wa sarakasi hizi unaniongoza kuwahimiza ninyi nyote kuendelea kuchukua hatari kwenye njia ya mazungumzo, na kwa njia hii kuwa sarakasi za amani na udugu.” Papa amewahakikishia maombi yake na kuwashuru tena.
Papa amesema "Ninawasindikiza ninyi nyote kwa maombi yangu, na ninawaomba, tafadhali, mniombee. Asante.” Amehitimisha apa Francisko.