Ratiba ya Mikutano ya Papa Jumatatu 26 imefutwa kwa sababu ya mafua. Ratiba ya Mikutano ya Papa Jumatatu 26 imefutwa kwa sababu ya mafua.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Ratiba za mikutano ya Papa imeharishwa kwa sababu ya mafua

Kama ilivyotokea Jumamosi iliyopita tarehe 24 Februari,tahadhari imechukuliwa pia kwa siku ya Jumatatu tarehe 26 Februari 2024 kwa kufuta ratiba ya mikutano ya Papa kwa sababu ya mafua lakini yasiyo na homa.

Vatican News

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican ilisasisha asubuhi ya Jumatatu tarehe 26 Februari 2024 kuhusu uamuzi wa Papa wa kusitisha vikao vilivyokuwa vimepangwa “kama tahadhari”, kama ilivyokuwa pia  Jumamosi tarehe 24 Februari iliyopita,  wakati ilipotolewa taarifa  ya kuwa Papa  Francisko alikuwa na homa, japokuwa siku ya Jumatatu wamebainisha kwamba ni “Dalili za mafua kidogo” ambazo haziambatani na homa.

Katika sala ya Malaika wa Bwana

Hata hivyo licha ya udhaifu huo,  Domenika  tarehe 25 Februari ulimruhusu Papa Francisko kuweza kuchungulia dirishanai na kutoa tafakari yake na sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican.


Na mara baada ya sala hiyo, Askofu wa Roma aligusia juu ya miaka miwili tangu kuzuka kwa vita nchini Ukraine na kurejea kutoa miito ya kusitisha vita  huko  Palestina na Israel na pia kuzungumzia  juu ya utekaji nyara nchini  Nigeria na vurugu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, lakini pia ahakusahau kuwakumbuka watu wa Mongolia wanaoteseka kwa baridi sana, huku akisisitizia juu ya mgogoro wa Tabianchi.

Papa Francisko alisitisha mikutano Jumatatu 26 Februari 2024
26 February 2024, 15:13