Baba Mtakatifu Francisko amewatumia ujumbe wa matashi mema, washindi wa Tuzo ya Sheikh Zayed Bin Sultan Al Nahyan ya Udugu wa kibinadamu kwa mwaka 2024. Baba Mtakatifu Francisko amewatumia ujumbe wa matashi mema, washindi wa Tuzo ya Sheikh Zayed Bin Sultan Al Nahyan ya Udugu wa kibinadamu kwa mwaka 2024.  

Ujumbe wa Papa Francisko Kwa Washindi wa Tuzo ya Zayed Kwa Mwaka 2024

Baba Mtakatifu Francisko amewatumia ujumbe wa matashi mema, washindi wa Tuzo ya Sheikh Zayed Bin Sultan Al Nahyan ya Udugu wa kibinadamu kwa mwaka 2024. Hawa ni watu waliojipambanua katika ujenzi wa mshikamano, ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Ni watu ambao wameendelea kuhamasisha amani na utulivu sehemu mbalimbali za dunia. Tuzo hii ilitolewa kwa mara ya kwanza tarehe 4 Februari 2021 kwa heshima ya Papa Francisko na Dr. Ahmad A.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., Vatican.

Waraka wa Kitume wa Baba Mtakatifu Francisko wa: "Fratelli tutti": Yaani “Wote ni Ndugu”: Kuhusu Udugu na Urafiki wa Kijamii” ni kitovu cha Mamlaka Matakatifu ya Ufundishaji katika Kanisa, mintarafu masuala ya kijamii kadiri ya Baba Mtakatifu Francisko. Huu ni muhtasari wa mafundisho, hotuba na mawazo yake tangu alipochaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki kunako mwaka 2013. Waraka huu wa kijamii unachota amana na utajiri mkubwa kutoka katika Hati ya Udugu wa Kibinadamu kwa Ajili ya Amani na Utulivu uliotiwa mkwaju kati ya Baba Mtakatifu Francisko na Dr. Ahmad Al-Tayyib, Imam Mkuu wa Msikiti wa Al- Azhar, ulioko mjini Kairo, nchini Misri, tarehe 4 Februari 2019 huko Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu. Katika kipindi cha Mwaka 2019 Baba Mtakatifu alifanya hija ya kitume nchini Morocco na Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu ambako kuna idadi kubwa ya waaamini wa dini ya Kiislam. Lengo lilikuwa ni kukuza na kudumisha majadiliano ya kidini, ili waamini wa dini hizi mbili waweze kufahamiana, kuheshimiana na kuthaminiana kama sehemu ya kumbukumbu ya miaka 800 tangu Mtakatifu Francisko wa Assisi alipokutana na Sultan Al Malik al-Kamil kunako mwaka 1219. Tuzo ya Sheikh Zayed Bin Sultan Al Nahyan, Muasisi wa Umoja wa Falme za Kiarabu ilianzishwa kunako mwaka 2019. Haya ni matunda ya ushirikiano na majadiliano ya kidini kati ya Baba Mtakatifu Francisko na Dr. Ahmad Al-Tayyib, Imam Mkuu wa Msikiti wa Al- Azhar, ulioko mjini Kairo, nchini Misri. Tarehe 4 Februari 2021 kwa mara ya kwanza Tuzo ya Sheikh Zayed Bin Sultan Al Nahyan, Muasisi wa Umoja wa Falme za Kiarabu ulioanzishwa tarehe 2 Desemba 1971 ilitolewa kwa heshima ya Baba Mtakatifu Francisko pamoja na Dr. Ahmad Al-Tayyib, Imam Mkuu wa Msikiti wa Al- Azhar, ulioko mjini Kairo, nchini Misri.

Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko ukosomwa wakati wa kutoa Tuzo
Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko ukosomwa wakati wa kutoa Tuzo

Viongozi hawa ndio waasisi pia wa Hati ya Udugu wa Kibinadamu kwa Ajili ya Amani na Utulivu. Tuzo hii pamoja na mambo mengine, inataka kunogesha jitihada za watu binafsi, vikundi na taasisi mbalimbali zinazojipambanua katika kutafuta, kujenga na kukuza mahusiano na mafungamano ya kibinadamu. Tuzo hii pamoja na mambo mengine, inalenga kujenga madaraja ya majadiliano ya kidini sehemu mbalimbali za dunia; umoja, mshikamano na ushirikiano wa Jumuiya ya Kimataifa. Kimsingi Tuzo hii ni alama ya ushirikiano na mshikamano kati ya waamini wa dini mbalimbali wanaojipambanua katika huduma kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Ni katika muktadha huu, Baba Mtakatifu Francisko amewatumia ujumbe wa matashi mema, washindi wa Tuzo ya Sheikh Zayed Bin Sultan Al Nahyan ya Udugu wa kibinadamu kwa mwaka 2024. Hawa ni watu waliojipambanua katika ujenzi wa mshikamano, ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Ni watu ambao wameendelea kuhamasisha amani na utulivu. Hawa wanakuwa ni watu wanaoendelea kuwahamasisha jirani zao na hivyo kuzaliwa mtandao wa ushirikiano na mafungamano ya kijamii kati ya waamini wa dini mbalimbali, kwa ajili ya huduma, pamoja na kuendelea kuheshimu utu, heshima na haki msingi za kila mt una hivyo kuendelea kumwilisha tunu msingi zinazobainishwa na Waraka wa Kitume wa: "Fratelli tutti": Yaani “Wote ni Ndugu”: Kuhusu Udugu na Urafiki wa Kijamii.” Baba Mtakatifu anawahamasisha waamini na watu wote wenye mapenzi mema kujenga na kudumisha utamaduni wa amani unaosimikwa katika majadiliano ya kidini; huruma, mshikamano, maendeleo endelevu na fungamani.

Papa Francisko alipokutana na washindi wa Tuzo ya Zayed kwa Mwaka 2024
Papa Francisko alipokutana na washindi wa Tuzo ya Zayed kwa Mwaka 2024

Baba Mtakatifu anapenda kutoa shukrani zake za dhati kwa Dr. Ahmad Al-Tayyib, Imamu Mkuu wa Al-Azhar, na kwa Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan, Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu, kwa mchango wao muhimu unaopania pamoja na mambo mengine kukuza na kudumisha maadili na utu wema; udugu wa kibinadamu na urafiki wa kijamii unaojengwa juu ya ukweli kwamba, binadamu katika tofauti zao msingi, lakini wote wanaunganishwa pamoja kama watoto wa Baba wa Mbinguni. Baba Mtakatifu anawapongeza washindi watatu wa Tuzo ya Zayed, ambayo sasa imeingia katika toleo lake la tano: Mashirika ya Kiindonesia Nahdlatul Ulama na Muhammadiyah, Dokta Magdi Yacoub, daktari wa upasuaji wa moyo kutoka Misri pamoja na Sr. Nelly León, kutoka nchini Chile. Idadi kubwa ya watahiniwa ni kielelezo kwamba kanuni maadili na utu wema; mambo yanayosherehekewa na kukuzwa katika siku hii yanasikika katika familia ya binadamu. Itakumbukwa kwamba, Kamati Kuu ya Utekelezaji wa Hati ya Udugu wa Kibinadamu tarehe 4 Desemba 2019 iliwasilisha mapendekezo ya kuwa na Siku ya Udugu wa Kibinadamu Kimataifa kwa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana António Guterres na matunda yake ni Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Udugu wa Kibinadamu. Tarehe 21 Desemba 2020 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa likapitisha Azimio Kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Udugu wa Kibinadamu inayoadhimishwa tarehe 4 Februari ya kila mwaka. Lengo kuu ni kudumisha majadililiano ya kidini na kitamaduni; umoja, mshikamano na ushirikiano wa Kimataifa, ili kujielekeza zaidi katika ujenzi wa utamaduni wa amani, maridhiano, mshikamano wa kidugu na upatanisho wa Kitaifa na Kimataifa. Mambo makuu yanayopaswa kupewa kipaumbele cha kwanza ni: Udugu wa kibinadamu, Mshikamano na Amani. Yote haya yanapania “kufyekelea” mbali “ndago” za uchoyo na ubinafsi, ili kujenga utamaduni wa majadiliano ya kidini katika ukweli na uwazi; kwa kukazia utu, heshima na haki msingi za binadamu. Siku hii inawakumbusha watu wote wa Mungu kwamba, ni ndugu wamoja!

Tuzo ya Udugu 2024
05 February 2024, 14:35