Kama sehemu ya kumbukizi ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa siku hii, Baba Mtakatifu katika ujumbe wake, anakazia umuhimu wa kutembea katika utu, kusikiliza, kuota ndoto na kutenda. Kama sehemu ya kumbukizi ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa siku hii, Baba Mtakatifu katika ujumbe wake, anakazia umuhimu wa kutembea katika utu, kusikiliza, kuota ndoto na kutenda.  (ANSA)

Ujumbe Kwa Siku ya Kimataifa ya Sala na Tafakari Dhidi ya Biashara Haramu ya Binadamu

Kama sehemu ya kumbukizi ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa siku hii Siku ya Kimataifa ya Sala na Tafakari ili kupambana na biashara haramu ya binadamu, Baba Mtakatifu katika ujumbe wake, anakazia umuhimu wa kutembea katika utu, kusikiliza, kuota ndoto na kutenda. Mtakatifu Josefina Bakhita akiwa mtoto mdogo, alitekwa nyara na “watu wasiojulikana” akauzwa utumwani na hatimaye, akaokolewa na huo ukawa ni mwanzo wa maisha mapya katika utu na heshima!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., Vatican.

Mtakatifu Josefina Bakhita, “Mwanamke wa shoka” alibahatika kwa neema na baraka za Mwenyezi Mungu kugeuza mateso na mahangaiko yake yote kuwa ni chemchemi ya Injili ya matumaini iliyogeuka hatimaye, na kuwa ni mbegu ya matumaini.  Mtakatifu Josefina Bakhita “Fortunata” maana yake “Bahati” alizaliwa kunako mwaka 1868 huko mjini Darfur, Sudan Kongwe. Akatekwa nyara na “watu wasiojulikana” akauzwa utumwani, na hatimaye, akanunuliwa na Balozi wa Italia mjini Khartoum aliyempeleka mjini Venezia. Akafundishwa katekesi na hatimaye, kubatizwa. Baadaye alijiunga na Shirika la Mabinti wa Upendo wa Mtakatifu Madgalena wa Canossa akijitoa sadaka bila ya kujibakiza kwa ajili ya huduma. Alifariki dunia tarehe 8 Februari 1947 huko Schio, nchini Italia. Mtakatifu Yohane Paulo II akamtangaza Josefina Bakhita kuwa Mwenyeheri tarehe 17 Mei 1992, na hatimaye, akamtangaza kuwa Mtakatifu tarehe Mosi Oktoba, mwaka 2000 katika maadhimisho ya Jubilei kuu ya Miaka 2000 ya Ukristo. Katika maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mtakatifu Josefina Bakhita, kunako mwaka 2015, Kanisa chini ya uongozi wa Baba Mtakatifu Francisko likaanzisha Siku ya Kimataifa ya Sala na Tafakari ili kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu na mifumo yote ya utumwa mamboleo inayoendelea kudhalilisha: utu, heshima na haki msingi za binadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Huu ni muda muafaka kwa ajili ya kusali na kuwaombea waathirika wa ubidhaishaji wa maumbile ya binadamu.

Siku ya sala na tafakari dhidi ya biashara haramu ya binadamu
Siku ya sala na tafakari dhidi ya biashara haramu ya binadamu

Tarehe 8 Febuari 2024, Mama Kanisa anaadhimisha Kumbukizi ya Miaka 10 tangu Baba Mtakatifu Francisko alipoanzisha Siku ya Kimataifa ya Sala na Tafakari ili kupambana na biashara haramu ya binadamu, ambayo kwa mwaka huu, inanogeshwa na kauli mbiu “Kutembea katika utu, kusikiliza, kuota ndoto na kutenda.” Baba Mtakatifu anapenda kuungana na wadau kutoka sehemu mbalimbali za dunia, ili kusali na kutafakari kuhusu athari za ubidhaishaji wa maumbile ya binadamu. Kama sehemu ya kumbukizi ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwa siku hii Siku ya Kimataifa ya Sala na Tafakari ili kupambana na biashara haramu ya binadamu, Baba Mtakatifu katika ujumbe wake, anakazia umuhimu wa kutembea katika utu, kusikiliza, kuota ndoto na kutenda. Mtakatifu Josefina Bakhita akiwa mtoto mdogo, alitekwa nyara na “watu wasiojulikana” akauzwa utumwani na hatimaye, akaokolewa na huo ukawa ni mwanzo wa maisha mapya. Huu ni mwaliko kwa waamini na watu wote wenye mapenzi mema kuwa na ujasiri wa kufungua macho na nyoyo zao kwa ndugu zao wanaotekwa, ili waweze kuwa ni sauti ya wale wasiokuwa na sauti kwa kutambua na kusimama kidete kulinda, kutetea na kudumisha utu, heshima na haki msingi za binadamu pamoja na kupambana fika na ubidhaishaji wa maumbile ya binadamu pamoja na mifumo yote ya utumwa mamboleo, ambalo ni janga lililofichama sana. Baba Mtakatifu anawawashukuru na kuwapongeza wadau wa tasnia ya mawasiliano ya jamii, ambao kwa ujasiri mkubwa wameanika hadharani ubidhaishaji wa maumbile ya binadamu pamoja na mifumo mbalimbali ya utumwa mamboleo, lakini kutokana na utandawazi usiojali wala kuguswa na mahangaiko ya wengine, ubidhaishaji wa maumbile ya binadamu, hili si jambo la kushangaza tena.

kumbukizi ya Miaka 10 Siku ya Sala na Tafakari Dhidi ya Biashara ya Binadamu
kumbukizi ya Miaka 10 Siku ya Sala na Tafakari Dhidi ya Biashara ya Binadamu

Huu ni mwaliko wa kushikamana na waathirika kwa kuwajibika zaidi dhidi ya biashara haramu ya binadamu kwa: Kutembea katika utu, kusikiliza, kuota ndoto na kutenda dhidi ya ubidhaishaji wa maumbile ya binadamu: Kumbe, watu wajenge utamaduni wa kuwasikiliza waathirika wa biashara haramu ya binadamu na mifumo yote ya utumwa mamboleo, hasa wanawake, wasichana na watoto wadogo, ambao ni waathirika wakuu. Wasikilizwe na kuhamasishwa na simulizi za mateso na mahangaiko yao, ili hatimaye, kuota ndoto ya watu kuishi kwa uhuru pamoja na kuheshimu utu wao. Baba Mtakatifu anasema, kwa nguvu ya Roho wa Kristo Yesu, waamini na wadau mbalimbali watekeleze kwa vitendo mapambano dhidi ya biashara haramu ya binadamu, ili kulinda utu, heshima na haki msingi za binadamu. Vitendo hivi vinaweza kuwa ni katika mfumo wa sala, kwa vishirikisha vyama na mashirika mbalimbali ili kuwatetea waathirika kutoka katika medani mbalimbali za maisha. Kwa hakika, watu wanaweza kushinda vita hii, jambo la msingi ni kutafuta mzizi wa biashara hii haramu na baadaye kufanya mabadiliko makubwa. Mtakatifu Josefina Bakhita ni kielelezo cha watu wanaoweza kukombolewa licha ya hali yao ya utumwa. Kumbe, huu ni wito wa kupambana na ubidhaishaji wa maumbile ya binadamu, ili kuwarejeshea waathirika, utu, heshima na haki zao msingi. Waamini watende na kamwe wasisustwe na dhamiri zao nyofu kwa kushindwa kuwasaidia waathirika. Baba Mtakatifu anawashukuru na kuwapongeza washiriki wote wa Maadhimisho ya Kumbukizi ya Miaka 10 tangu kuanzishwa Siku ya Kimataifa ya Sala na Tafakari ili kupambana na biashara haramu ya binadamu, ambayo kwa mwaka huu, inanogeshwa na kauli mbiu “Kutembea katika utu, kusikiliza, kuota ndoto na kutenda, ili kujenga udugu wa kibinadamu na amani.

Utumwa Mamboleo
08 February 2024, 17:42