Ujumbe wa Kwaresima 2024,Papa:'Kupitia jangwa Mungu hutuongoza'
Na Angella Rwezaula – Vatican
Fikirieni kwa upya mitindo ya maisha pamoja ili kufanya sehemu ya ulimwengu tunayoishi kuwa bora zaidi na kuzuia kulilia yaliyopita yasiyoweza kuelezeka ya utumwa na usibaki ndani mwetu, ambao ni, hali inayotokana na kujitolea kwa mifano ya maisha na ukuaji ambayo hugawanya, kuwatenga na kuwakosea haki. Haya ni baadhi ya dhana zilizomo kwenye Ujumbe wa Baba Mtakatifu wa Kwaresima 2024 wenye kuongozwa na kauli mbiu: “Kupitia jangwa Mungu hutuongoza kwenye uhuru." Kama vile Waisraeli, wakiongozwa na Musa, walivyotamani sana kurudi Misri wakati wakiwa jangwani, ndivyo hivyo hata leo hii watu wa Mungu na jamii zetu wanadumisha vifungo vya kukandamiza huko wakingoja kukatwa. Tofauti na Farao, Mungu hataki mafunzo, lakini anataka watoto, kuwa uhuru ambao ni wito wa nguvu na hukomaa baada ya muda."
Kwaresima ni wakati wa neema kutoka kifo hadi uzima
Katika ujumbe huo Baba Mtakatifu anabainisha kuwa "ishara ya kuendelea kwa utumwa ndani yetu ni kwa ukosefu ulioenea wa tumaini, kutangatanga bila nchi ya ahadi ambayo tunaweza kujitahidi pamoja. Kipindi muhimu cha Kwaresima kinatupatia fursa ya kuanza safari ya uhuru. Ni wakati wa neema ambapo jangwa linarudi kuwa mahali pa upendo wa kwanza", kama nabii Hosea anavyotangaza. Mungu huwaelimisha watu wake, ili watoke katika utumwa wao na wapate mpito kutoka katika kifo hadi uzima.
Kutazama ukweli na kusikiliza kilio cha ndugu
Hatua ya kwanza ya kuchukua ili kuifanya safari ya Kwaresima iwe thabiti Baba Mtakatifu anainisha ni kutaka kuona ukweli. Kama vile Mungu anavyomwambia Musa: “Nimeyaona mateso ya watu wangu (...), nimesikia kilio chao”. "Hata leo kilio cha kaka na dada wengi wanaokandamizwa kinafika mbinguni. Hebu tujiulize?: je, inatufikia sisi pia? Ikiwa tumeshindwa na kutojali, lazima tukiri kwamba hata leo tuko chini ya mamlaka ya Farao. Ni utawala unaotufanya tuchoke na kufa ganzi. Ni kielelezo cha ukuaji ambacho hutugawanya na kuiba maisha yetu ya baadaye. Dunia, hewa na maji vimechafuliwa, lakini pia roho zimechafuliwa. Kiukweli, ingawa ukombozi wetu ulianza na ubatizo, hamu isiyoelezeka ya utumwa inabaki ndani yetu. Ni kama kivutio kuelekea usalama wa mambo ambayo tayari yameonekana kwa madhara ya uhuru."
Utawala unaozima uwezo wa kuota ndoto
Papa Francisko katika ujumbe wa Kwaresima anasisitiza kwamba "utawala unaotukandamiza hata hivyo huzima hamu ya mabadiliko katika ulimwengu tunamoishi. Kuna upungufu wa tumaini, ambao leo lazima ushutumiwe, wa kizuizi cha kuota ndoto, kilio cha kimya kinachomfikia Mungu. Kinafanana na ile tamaa ya utumwa ambayo ililemaza Waisrael jangwani na kuizuia kusonga mbele. Hii ni kwa sababu msafara huo uliweza kuingiliwa: vinginevyo isingewezekana kueleza ni kwa nini ubinadamu ambao umefikia kizingiti cha udugu wa ulimwengu wote na viwango vya maendeleo ya kisayansi, kiufundi, kiutamaduni na kisheria wenye uwezo wa kuhakikisha utu kwa wote unapapasa katika giza la ukosefu wa usawa na migogoro. Ikiwa huu ndio ukweli, hakika mwingine ni kwamba “Mungu hajatuchoka” na bado anataka kutuongoza kwenye uhuru. Tofauti na Farao, Mungu hataki raia, bali watoto, na Kwaresima ni wakati wa uongofu, wakati wa uhuru, ambamo mtu anapaswa kufanya uamuzi wa kibinafsi wa kutokuwa watumwa tena." Papa anakazia.
Miungu ya nguvu, pesa na ubinafsi vinalemaza
Katika hatua hiyo ya maandishi ya Ujumbe wa Kwaresima 2024, Papa Francisko anaelezea kwamba kuna hatua nyingine inayotufunga: Ni miungu ambayo, tunaweza kuizingatia kama sauti ya Farao ndani yetu, ambayo inatupotosha, ikitusukuma kukuza maisha yya itakadi, nguvu zote, kutambuliwa na wote, kuwa bora ya kila mtu." Papa anabainisha kwamba hiyo ni njia ya zamani. Kwa hivyo tunaweza kushikamana na pesa, kwa miradi fulani, maoni, malengo, msimamo wetu, mila, hata kwa watu fulani. Badala ya kutuhamasisha, wanalemaza. Badala ya kutuleta pamoja, watatugombanisha sisi kwa sisi. Hata hivyo, kuna ubinadamu mpya, watu wali wadogo na wanyenyekevu ambao hawajashindwa na mvuto wa uwongo.
Tunawalea Ujumbe mzima wa Papa Francisko wa Kwaresima 2024 unaoongozwa na kauli mbiu: "Kupitia jangwa Mungu anatuongoza katika uhuru."